{"title":"Utamaduni na Udhibiti wa Nyimbo za Bongo Fleva Nchini Tanzania (2000-2019)","authors":"Edson Z. Thomas, J. Bulaya","doi":"10.56279/jk.v86i2.6","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.6","url":null,"abstract":"Udhibiti wa nyimbo ni changamoto inayowakumba wasanii wa nyimbo za Bongo Fleva. Hali hiyo imechangiwa na kukua kwa tasnia hiyo pamoja na kukua kwa TEHAMA ambapo wasanii wanaweza kujifunza na kuiga kwa haraka mitindo kutoka nje ya utamaduni wa Watanzania pamoja na kufikisha kazi zao kwenye hadhira kwa haraka kabla upungufu wa nyimbo hizo haujagunduliwa. Makala hii imechunguza suala hili kwa kuangalia chimbuko, usuli pamoja na sababu zinazochochea udhibiti wa nyimbo hizo. Data za makala hii zilikusanywa kwa njia ya hojaji na usaili. Wasanii wa Bongo Fleva na viongozi wa taasisi za udhibiti wa sanaa nchini Tanzania walihojiwa. Aidha, baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliosomea masuala ya udhibiti wa sanaa walijaza hojaji ili kutoa mawazo yao kuhusu utamaduni na udhibiti. Data zilichambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Maadili iliyoasisiwa na Plato. Kutokana na uchunguzi uliofanyika, sababu za kitamaduni za kudhibitiwa kwa nyimbo za Bongo Fleva ni: mosi, kuiga tamaduni za kigeni zilizo kinyume na mila na desturi za Kitanzania. Pili, matumizi ya lugha isiyo na staha katika miktadha mbalimbali pamoja na sababu za kidini. Mjadala wa makala hii umejikita katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000-2019 kutokana na wimbi kubwa la udhibiti wa nyimbo hizo ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"350 3","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140719365","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Riwaya za Euphrase Kezilahabi kama Nyenzo Mwafaka za Ukuzaji wa Stadi ya Tafakuri Tunduizi: Mfano wa Nagona na Mzingile","authors":"Wallace Kapele Mlaga, Laurien Tuyishimire","doi":"10.56279/jk.v86i2.4","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.4","url":null,"abstract":"Lengo kuu la makala hii ni kujadili namna riwaya za Euphrase Kezilahabi zinavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza stadi ya tafakuri tunduizi. Ili kufanikisha lengo hili, makala imeshughulikia malengo mahususi mawili: kwanza, makala inajadili namna stadi ya tafakuri tunduizi inavyosawiriwa katika riwaya teule za Kezilahabi na hivyo kuzifanya riwaya husika kuwa nyenzo mwafaka za ukuzaji wa tafakuri tunduizi. Pili, kubainisha namna riwaya teule zinavyosawiri umuhimu wa stadi ya tafakuri tunduizi. Ili kufanikisha malengo haya, data zilikusanywa kupitia mbinu ya uchambuzi wa matini. Data hizi zilichambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Uhalisia na Nadharia ya Semiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba riwaya za Nagona na Mzingile ni nyenzo mwafaka za kukuza tafakuri tunduizi kwa sababu riwaya hizi zinasawiri matendo mbalimbali yanayofanywa na wahusika kutokana na kutokuwa na stadi ya tafakuri tunduizi: kuyumbayumba kiimani kwa waumini na watu kutotatua changamoto zinazowakabili na badala yake kupendelea kumuachia Mungu. Aidha, umuhimu wa tafakuri tunduizi umesawiriwa katika riwaya teule. Tafakuri tunduizi imeonekana kuwa na umuhimu ufuatao: kuwezesha ufanyaji wa maamuzi sahihi na kusaidia kutengeneza maarifa mapya. Makala inahitimisha kuwa riwaya teule ni nyenzo mwafaka za ukuzaji wa tafakuri tunduizi kwa kuwa zinaonesha sio tu madhara ya kutokuwa na tafakuri tunduizi bali pia umuhimu wake.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"12 2","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140720404","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"The Role of Nyakyusa Proverbs in Behavioural Development","authors":"Gerephace Mwangosi","doi":"10.56279/jk.v86i2.5","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.5","url":null,"abstract":"This article examines the role of sayings in developing human behaviour in the Nyakyusa community in Tanzania. The primary data for this article were obtained by interview method in Luteba (Ipuguso), Kandete (Ipelo) and Mpombo (Lulasi) wards in Rungwe district, Mbeya region. Those areas met the data requirements presented in this article. The Sociological Theory was used in the analysis and discussion of data by looking at literature as a special unit that reflects both the science and culture of the society. Selected community sayings were examined as a special link to social relations. This article has revealed that the sayings of the selected community are a special link of social relations considering its history, philosophy, culture and economy. The sayings serve as a specific reference library for social issues, and a strong indigenous link that builds a system to train, strengthen and keep the community together in the foundations of culture and the whole philosophy of life from tradition until now. This article concludes that sayings are used as a special warehouse for reference to social issues that keep the community together in the foundations of culture and the whole philosophy of life from ancient times until now.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"1 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140717267","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Dosari za Kisarufi katika Maandishi ya Kiswahili Sanifu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Nchini Burundi","authors":"Dieudonné Butoyi, Zelda Elisifa","doi":"10.56279/jk.v86i2.1","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.1","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza utamalaki wa dosari za kisarufi zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kwenye vyuo vikuu vya Burundi. Uchunguzi huu uliozingatia matini za kimaandishi ulifanyika kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi Makosa (UM) ya Corder (1967) ambayo imeboreshwa na wanaisimu wa siku za karibuni kama Gass na Selinker (2008), Mahmoodzadeh (2012) na Al-khreshen (2015) ili kuchunguza na kutathmini makosa. Sampuli ya wanafunzi mia moja (100) ilitumika na data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunguzi matini. Matokeo ya uchunguzi huu yamedhihirisha jumla ya dosari za kisarufi 981 zilizogawanyika katika aina nne ambazo ni: (a) dosari za kifonolojia kwa kiasi cha 37.2%, (b) dosari za kimaumbo kwa kiasi cha 21.8%, (c) dosari za kisintaksia na kimofosintakisia kwa kiasi cha 30.1%, na (d) dosari za kimsamiati 10.9%. Viwango vya utamalaki wa dosari katika matumizi ya kimaandishi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Burundi hasa ya kifonolojia na kimofosintaksia vimedhihirisha kuwa kunahitajika hatua za haraka za uboreshaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, walimu na mbinu thabiti katika ufundishaji wa somo la Kiswahili.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"14 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140717402","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uhawilishaji wa Lafudhi ya Kihehe na Athari zake katika Mawasiliano ya Wajifunzaji wa Kiswahili Sanifu kama Lugha ya Pili","authors":"Mwaija Ngenzi","doi":"10.56279/jk.v86i2.2","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.2","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza uhawilishaji wa lafudhi ya Kihehe na athari zake katika mawasiliano ya wajifunzaji wa Kiswahili sanifu kama lugha ya pili (L2). Sababu iliyochochea kufanyika kwa utafiti huu ni kuwa uhawilishwaji wa lafudhi ya Kihehe umebainika kupotosha maana na kukwamisha mawasiliano miongoni mwa wajifunzaji lugha ya Kiswahili sanifu wa jamii ya Wahehe. Data za makala hii zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili sanifu wa jamii ya Wahehe ambao Kihehe ni lugha mama yao. Data za msingi za makala hii zilikusanywa kwa mbinu za masimulizi ya hadithi na uchambuzi wa nyaraka. Uchambuzi wa data uliongozwa kwa Nadharia za Usasanyuzi Linganishi na Arifu ya Mawasiliano. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa uhawilishwaji wa lafudhi ya Kihehe katika Kiswahili sanifu husababisha athari za kifonolojia na kisemantiki. Athari zilizobainika ni udondoshaji, uchopekaji, ubadilishanaji na urefushwaji wa fonimu katika maneno ya Kiswahili sanifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa michakato ya udondoshaji, uchopekaji, ubadilishanaji na urefushwaji wa fonimu katika maneno ya Kiswahili sanifu husababisha mabadiliko ya maneno kimatamshi na kimaana.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"267 2‐3","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140719707","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Iktibasi katika Methali za Waswahili","authors":"Lina Akaka, Sheila Wandera-Simwa","doi":"10.56279/jk.v86i2.3","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v86i2.3","url":null,"abstract":"Makala hii inalenga kuchunguza namna iktibasi inavyojitokeza katika methali za Waswahili. Iktibasi ni dhana ya Kiarabu kwa mujibu wa Karisa na Mwinyifaki (2013). Ni mbinu ya kuchota mafundisho ya Kurani Tukufu na Sunnah na kuyatumia katika fasihi bila kuonesha yametoka katika Kurani Tukufu na Sunnah (Karisa na Mwinyifaki, 2013). Maisha ya Waswahili licha ya kuongozwa na maadili yaliyomo katika mafundisho ya dini ya Kiislamu, methali zinazotumiwa na Waswahili hao katika mazungumzo yao ya kila siku pia huchangia kutilia nguvu mafundisho ya dini. Uchunguzi huu umechochewa na methali za jamii ya Waswahili ambazo zinaelekea kusheheni mafundisho ya dini. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uislamu kwa mujibu wa mawazo ya Hashi (2011) katika kubainisha namna mafundisho ya Kurani na Hadith yanavyojitokeza katika methali za Waswahili. Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba methali za Waswahili zilisheheni mafundisho ya maadili ambayo yalipatikana pia katika Kurani na Hadith. Uhusiano mwema kati ya binadamu na binadamu na binadamu na Mungu unapatikana katika methali, na Kurani na Hadith vilevile.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"275 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140719961","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Usawiri wa Unyanyasaji wa Kiuchumi dhidi ya Wanawake katika Riwaya ya Kiswahili","authors":"Ernesta S. Mosha","doi":"10.56279/jk.v85i1.13","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v85i1.13","url":null,"abstract":"Makala hii inajadili unyanyasaji wa kiuchumi kwa wanawake kama ulivyosawiriwa katika riwaya ya Kiswahili. Makala inatumia dhana ya vilongo zoeleka katika unyanyasaji wa wanawake ili kuweka bayana namna unyanyasaji wa kiuchumi unavyochochewa na mambo kama vile ubabedume na mila na desturi. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika riwaya teule tatu za Kiswahili ambazo ziliteuliwa kutokana na kusawiri aina mbalimbali za unyanyasaji wa kiuchumi kwa wanawake. Makala inabainisha namna vilongo zoeleka katika unyanyasaji wa wanawake vilivyotumika kuonesha jinsi baadhi ya wanaume wanavyofanikisha azma yao ya kuwanyanyasa wanawake kiuchumi. Aidha, makala imebainisha jinsi kilongo cha mfumo wa kijamii na ujifunzaji kitabularasa kilivyotumiwa na waandishi kuonesha kuwa wanaume wanyanyasaji hawana makosa kwa kuwa hawakufanya unyanyasaji huo kwa makusudi. Makala inaweka wazi kuwa usawiri wa aina hii una athari ya kuchochea unyanyasaji wa kiuchumi dhidi ya wanawake na kuimarisha mtazamo kuwa unyanyasaji wa aina hii ni jambo la kawaida na haliwezi kuepukika. Kwa upande mwingine, kilongo cha ukombozi wa binadamu wa kiharakati kimetumiwa kuonesha wazi kuwa baaadhi ya wanaume wanawanyanyasa wanawake kiuchumi kwa makusudi kwa hiyo wanastahili kuwajibishwa kutokana na unyanyasaji huo. Kwa kuwa riwaya zina nafasi kubwa ya kutambulisha njia mbadala za kukabiliana na aina mbalimbali za unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kiuchumi, ni muhimu vilongo mbadala vikatumika katika riwaya ya Kiswahili ili kusaidia kubadili tabia za wanaume wanyanyasaji pamoja na mtazamo kuhusu unyanyasaji wa kiuchumi dhidi ya wanawake.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"28 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-12-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128358771","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Dhima ya Kialami Pragmatiki ‘Hivi’ katika Mawasiliano ya Kiswahili","authors":"Magreth J. Kibiki","doi":"10.56279/jk.v85i1.16","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v85i1.16","url":null,"abstract":"Makala hii inahusu dhima za kialami pragmatiki hivi katika mawasiliano ya Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yanayofanywa katika vijiwe vya mamalishe, vipindi vya televisheni na kutoka katika soga za mtandao wa WhatsApp. Uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Umuktadhaishaji ya Gumperz (1982) na kwa kutumia mbinu ya uchambuzi kilongo. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kwamba kialami pragmatiki hivi kina dhima tofautitofauti kinapotumiwa katika mawasiliano. Miongoni mwa dhima hizo ni kutumika kama kianzilishi cha swali, kusisitiza jambo, kunukuu mazungumzo, kuashiria wakati uliopo au muda si mrefu, kudokeza makadirio au kutokuwa na hakika ya jambo na kutumika kama kiolezi. Kwa ujumla, makala hii inadokeza kwamba lugha ya Kiswahili ina utajiri wa kimaana unaotokana na matumizi ya vialami pragmatiki. Hivyo, tafiti zaidi zinaweza kufanyika kuchunguza dhima za vialami pragmatiki vingine katika lugha hii.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"102 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-12-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"132968711","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Miaka 60 ya Ufundishaji wa Kiswahili nchini China","authors":"Zhao Lei","doi":"10.56279/jk.v85i1.8","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v85i1.8","url":null,"abstract":"Kozi ya Kiswahili ilianza kufundishwa nchini China tangu mwaka 1960. Katika miaka 60 iliyopita, kozi hiyo imepitia kipindi cha ukuaji (1960-1977), kipindi cha mdororo (1978-1999) na kipindi cha upanuzi (2000-Sasa) pamoja na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ya ndani pamoja na uhusiano baina ya China na Tanzania. Makala hii imepitia historia ya ufudishaji wa Kiswahili nchini China kwa ujumla. Pia, imehakiki maendeleo na changamoto zake katika masomo, vitabu vya kiada, walimu na wanafunzi na kutoa mapendekezo ya kuukuza ufundishaji na utafiti wa lugha hii nchini China.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"18 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-12-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"125361240","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uhusiano wa China na Afrika Mashariki kama Ilivyobainishwa katika Fasihi ya Kiswahili","authors":"Wael Nabil Ibrahim Othman","doi":"10.56279/jk.v85i1.14","DOIUrl":"https://doi.org/10.56279/jk.v85i1.14","url":null,"abstract":"Makala hii inalenga kuangazia uhusiano wa China na Afrika Mashariki kama ilivyobainishwa katika fasihi ya Kiswahili. Ili kufikia lengo hilo, makala hii imegawanywa katika sehemu kuu tano. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao unaonesha lengo la makala hii na data zake zilizokusanywa kutoka katika fasihi simulizi na andishi ya Kiswahili. Sehemu ya pili inafafanua Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyotumika katika makala haya. Sehemu ya tatu inajadili historia ya uhusiano wa China na Afrika Mashariki, vipindi ulivyopitia na nyanja zake kwa jumla. Sehemu ya nne ambayo ndiyo kiini cha makala haya, inaeleza uhusiano wa China na Afrika Mashariki kupitia tanzu za fasihi ya Kiswahili. Sehemu ya tano ni hitimisho ambalo linaelezea kwa muhtasari matokeo ya uchunguzi wa makala hii.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-12-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130075425","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}