{"title":"Wingilugha na Maendeleo Endelevu katika Kaunti Nchini Kenya: Hali Halisi katika Kaunti ya Machako","authors":"Peter Willington Kilonzo, Nabeta K. N. Sangili","doi":"10.37284/jammk.5.2.991","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.991","url":null,"abstract":"Ulimwenguni kote, lugha imekuwa na bado inaendelea kuwa raslimali muhimu katika maendeleo ya sehemu yoyote ile. Kwa watu wengine, lugha ni mtaji katika shughuli zozote za kimaendeleo kwa sababu bila lugha inayoeleweka na washiriki husika hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na iwapo yatafanyika, kasi yake itakuwa ya chini sana. Katiba ya 2010 ilifanya mabadiliko mengi na mojawapo ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi sawa na Kiingereza. Katiba hii pia ilitengeneza serikali 47 za magatuzi ambazo zina upekee wake wa utamaduni, lugha ikiwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kaunti hizi. Hivyo, angalau kila Kaunti ina lugha tatu zinazozungumzwa humo. Zaidi ya lugha husika tatu, shughuli tofauti zimechangia watu wa jamii mbalimbali kuhamia na kutagusana katika Kaunti tofauti na za kwao, jambo linalosababisha wingilugha dhahiri katika Kaunti zote nchini Kenya. Katika hali hii, swali kuu linakuwa ni: je, lugha ikiwa ni raslimali na mtaji muhimu katika maendeleo, wingilugha unaweza kutumika vipi katika muktadha wa Kaunti ili kuhakikisha maendeleo endelevu? Swali hili linakuwa msingi mkuu wa makala haya kuangazia jinsi wingilugha (Kiswahili, Kiingereza, Lugha asili, na lugha nyinginezo) unavyoweza kutumika katika muktadha wa Kaunti nchini Kenya ili kuhakikisha maendeleo endelevu katika kila Kaunti. Utafiti umejikita katika Kaunti ya Machakos.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-12-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"126310992","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Changamoto Zinazowakumba Vijana katika Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga","authors":"John Kennedy Mwangi","doi":"10.37284/jammk.5.2.959","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.959","url":null,"abstract":"Katika ulimwengu wa sasa, kuna mabadiliko chungu nzima yanayoshuhudiwa duniani yanasababishwa na masuala anuwai kama vile maendeleo ya kiteknolojia pamoja na utandarithi yanayoathiri pakubwa maisha ya vijana. Nchini Kenya, vijana wana umuhimu wa kipekee kwani wanatekeleza majukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi. Isitoshe, idadi ya vijana kote ulimwenguni imeendelea kuongezeka kila uchao na imepiku ile ya wazee. Kwa hivyo, ni nyema kujadili changamoto zinazowakabili na kupendekeza hatua za kukabiliana nazo. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua changamoto zinazowakumba vijana pamoja na athari zake katika ya tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya S.A Mohamed (2000). Mada hii ilichaguliwa kwa misingi kwamba vijana wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao zinazowaathiri kwa kiasi cha haja na kutinga juhudi za kuafikia jaala zao. Utafiti huu ulilenga kubainisha changamoto zinazowakumba vijana katika tamthilia hii na kutambua mbinu ambazo vijana hawa wanazua ili kukabiliana nazo. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kwa sababu ilionekana kufaa zaidi kuchanganua changamoto zinazowakumba vijana. Hii ni kwa sababu changamoto hizi zina uhalisia mkubwa katika maisha yao. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza na kueleza namna changamoto za vijana zinavyojitokeza katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga na kisha kubainisha hatua zinazochukuliwa kuzitatua changamoto hizo. Utafiti huu ni wa kimaelezo na kiudhamano kwani ulihusisha kuchanganua matini zinazohusiana na mada husika. Sampuli katika utafiti huu iliteuliwa kimakusudi kwani ndiyo ingempa mtafiti data aliyonuia kuipata. Ni bayana kuwa utafiti huu utaifaa jamii ya wasomi wanaoshughulikia maswala ibuka katika jamii.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"52 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-14","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"115980391","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mdhihirisho wa Mahusiano ya Uwezo katika Vikatuni vya Shujaaz: Uchanganuzi Makinifu wa Kidiskosi","authors":"Sammy Liana Dimbu","doi":"10.37284/jammk.5.2.946","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.946","url":null,"abstract":"Vikatuni ni chombo muhimu cha mawasiliano katika Karne ya 21. Huenda ndio sababu vimeendelea kukumbatiwa katika uwasilishaji wa masuala yanayohusu vijana. Makala hii inahusu Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi katika vikatuni vya Shujaaz ili kubainisha uzalishaji wa mahusiano ya uwezo katika vikatuni hivi. Utafiti huu ni wa kiisimu na ni hatua kutokana na tafiti tangulizi zilizotafitia vikatuni hivi katika taaluma ya fasihi. Nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi iliongoza utafiti huu. Kwa mujibu wa nadharia hii changamoto za kijamii hubainika katika uzalishaji wa matumizi mabaya ya mamlaka au udhalimu wa wenye mamlaka katika diskosi. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 za diskosi ya Shujaaz zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika katika kuchanganua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Matokeo ni kuwa mahusiano ya uwezo katika Shujaaz ni baina ya: wahusika mashujaa na wahusika wa kawaida, wahusika mashujaa na vijana, wadhamini na vijana, hadhira lengwa ambao ni vijana na mtu mashuhuri na mahusiano ya uwezo ya kiuana. Makala hii inatoa mchango katika taaluma ya isimu kwa kubainisha namna mahusiano ya uwezo yanavyotumiwa kuangazia masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, na namna yanavyoweza kutumiwa kuwashirikisha vijana katika masuala yanayowakumba katika jamii. Utafiti huu unapendekeza tafiti zaidi za baadaye zifanywe kwa kuzingatia mikakati ya uhalalishaji na uharamishaji inayodhihirika kupitia mahusiano ya uwezo katika diskosi ya Shujaaz","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"28 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"127168666","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Nafasi ya Muktadha katika Utendaji wa Mivigha ya Olubeko Miongoni mwa Abanyala wa Kakamega, Kenya","authors":"Benard Waswa, Furaha Chai, A. Buliba","doi":"10.37284/jammk.5.2.898","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.898","url":null,"abstract":"Mivigha mara nyingi huangaziwa kwa mtazamo wa kidini au swala la imani. Mtazamo huu umejengwa kwa imani kwamba binadamu hutamani bila kifani kuhusiana na wahenga wake, Mungu wake, na mwishowe nguvu zaidi zilizoko juu yake. Matambiko katika jamii ya Kiafrika ni mengi. Kuna matambiko ya kuzaliwa, matambiko ya kupeana majina, matambiko ya tohara, matambiko ya harusi, matambiko ya kifo, matambiko ya kidini, na matambiko ya kisiasa miongoni mwa mengine katika jamii pana za Kiafrika. Olubeko ni tambiko la kifo linalofanyika siku tatu baada ya mazishi ya mwanamume mwenye umri au mwenye hadhi ya kutambuliwa miongoni mwa Abanyala wa Kakamega. Mivigha hii huhusisha utendaji mbalimbali. Mojawapo ya utendaji unaohusishwa katika tambiko hili ni nyimbo. Kazi hii inapambanua nafasi ya muktadha katika uteuzi na uwasilishaji wa nyimbo husika kwa kuzingatia miktadha mahususi ya utendaji wa mivigha ya Olubeko miongoni mwa Abanyala wa Kakamega. Nadharia ya utendaji ndio kurunzi ya kazi hii. Nadharia hii inasisitiza kuwa kupitia utendaji, ujumbe huwafikia watu wengi. Matokeo yanaonyesha kuwa kuna miktadha tano mahususi katika mivigha ya Olubeko: omusee (baraza), khusirindwa (kaburi), olukendo (safari) na hango (nyumbani). Kutokana na miktadha hii fanani aliweza kuteua na kuwasilisha nyimbo faafu za kila hatua ya mivigha hii. Muktadha ndio uliongoza fanani katika uteuzi wa wimbo husika","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"109 4","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-10-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"133171068","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari","authors":"Winnie Musailo Wekesa","doi":"10.37284/jammk.5.2.886","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.886","url":null,"abstract":"Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii imetokana na mpango wa kufanyia mtaala wa elimu mabadiliko ili kumudu mahitaji ya jamii katika karne ya ishirini na moja. Silabasi ya sasa ya Kiswahili kwa shule za upili inaeleza kwa wazi vipengele vya kufundishwa katika sarufi na matumizi ya lugha. Sentensi ni mojawapo ya vipengele vya sarufi vinavyofundishwa katika shule za upili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kuna aina tatu kuu za sentensi kimuundo; miongoni mwazo ikiwa ni sentensi changamano Makala haya itaangazia aina hii ya sentensi kwa msingi wa uchanganuzi wake kutumia mikabala mbalimbali. Pengo lililopo ni kwamba vitabu vya kiada vilivyopendekezwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Mtaala kisha kuidhinishwa na wizara ya elimu nchini; vimerejelea mada hii kwa mtazamo tofauti tofauti. Hali ambayo inazua mkanganyo na kuathiri mchakato wa ufunzaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi. Mada ya uchanganuzi wa sentensi inapasa kutiliwa msingi katika kidato cha kwanza na pili kisha kusisitizwa katika kidato cha tatu na nne. Kinyume na inavyojitokeza katika vitabu hivi vya kiada ambapo ufundishaji wa mada hii unaanzia kidato ha tatu na kukamilishwa katika kidato cha nne. Masebo (2002), anasema uchanganuzi wa sentensi ni kipengele cha sarufi miundo ambacho ni utanzu unaoshughulikia maneno katika tungo na uhusiano wa vipashio vyake. Ni muhimu mwanafunzi kupata mwelekeo faafu wa mada hii kwa kuelekezwa kwa njia na namna moja sio kwa kuhitilafiana. Lugha kando na kuwa ni chombo muhimu cha kujieleza, pia ina jukumu la kupitisha elimu faafu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"2002 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-10-14","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128316829","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mabadiliko Ya Hadithi Fupi Teule Za Kiswahili : Mkabala Wa Usasaleo","authors":"Paul I. Mwiti Bundi, O. Ntiba, Allan Mugambi","doi":"10.37284/jammk.5.2.882","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.882","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza mabadiliko katika hadithi fupi kwa mkabala wa usasaleo. Inaangazia athari za usasaleo katika hadithi fupi za kimapokeo. Kwa kuwa athari ya kiusasaleo inaendelea kujitokeza katika hadithi fupi za kisasa kila kukicha, kulikuwepo na haja ya kutafiti juu ya mabadiliko haya. Katika makala hii mtafiti alichunguza vile baadhi ya hadithi zilivyoegemea uhalisia na umapokeo na jinsi waandishi wengine walivyotumia majaribio ya kimuundo, kimtindo na kimaudhui kuandika hadithi fupi za kisasa. Mtafiti alikusanya data katika diwani tatu za hadithi fupi za: Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine, Mizungu ya Manabii na Hadithi Nyingine na Homa ya Nyumbani na Hadithi Nyingine. Data iliteuliwa, kupangwa na kujadiliwa kulingana na maswali na madhumuni ya utafiti. Makala hii iliongozwa na nadharia ya umuundoleo iliyoasisiwa na Jacques Derrida na Michel Foucalt mwaka wa 1960. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa: Kubainisha mabadiliko ya kimuundo ya kiusasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili, kudhihirisha mabadiliko ya kimtindo yaliyosababishwa na usasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili na kufafanua mabadiliko ya kimaudhui yaliyotokana na usasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili. Katika hadithi sita teule zenye mbinu za kiusasaleo waandishi walitumia mabadiliko majaribio na upya katika muundo mtindo na maudhui. Sampuli maksudi ilitumika kuteua hadithi zilizofaa utafiti huu. Madhumuni na maswali ya utafiti yalitumika kuteua kupanga na kueleza data. Matokeo ya utafiti yalitolewa kimaelezo katika sura ya nne, tano na sita na hitimisha kutolewa katika sura ya saba. Matokeo ya utafiti yanatarajiwa kufaa wanafunzi wa fasihi wa shule za upili,watafiti wa baadaye, wahakiki na wasomi wa fasihi kwa kuwapa uelewa mpana wa mabadiliko yanayotokea katika uandikaji wa hadithi fupi za Kisasa. Zaidi ya haya, utafiti huu ulichangia kuziba pengo lililopo katika utafiti juu ya mabadiliko katika hadithi fupi mkabala wa usasaleo. Maarifa yanayotokana na utafiti huu ni mchango muhimu katika fasihi andishi hasa hadithi fupi za Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"92 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-10-12","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"133144739","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Raphael Mwaura Gacheiya, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu
{"title":"“Gari ni Testing”: Uhalalishaji wa Mahusiano ya Kingono Miongoni mwa Wazulufu Nchini Kenya","authors":"Raphael Mwaura Gacheiya, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu","doi":"10.37284/jammk.5.1.878","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.878","url":null,"abstract":"“My friend always tells me of how good it is... how sweet it is... when will I know these things?” \u0000Ulimwenguni, tafiti kuhusu tabia za wazulufu zimebainisha kuwa wazulufu hushiriki ngono za mapema licha ya ujamianaji kabla ya ndoa kukashifiwa. Imegunduliwa kuwa utamaduni, matumizi ya lugha na miktadha ya kijamii huwa na nafasi muhimu katika kuelewa na kuthibiti mahusiano na ushiriki wa ngono. Hata hivyo, ni kweli kuwa kutokana na mabadiliko ya jamii kiuchumi, kisiasa na kijamii, tamaduni hizi zimeasiwa na kupelekea itikadi ya kujihini na ubikira kutozingatiwa na wazulufu. Makala haya yanalenga kuangazia jinsi wazulufu kwa kuegemea peo za kimazungumzo wanavyohalalisha ngono za mapema miongoni mwao. Hili litaafikiwa kupitia Nadharia ya Uchanganuzi wa Peo kama ilivyoasisiwa na E. Goffman mwaka wa 1974. Data inatokana na mazungumzo katika vikundi kiini miongoni mwa wazulufu katika shule za upili nchini Kenya. Kwa kutumia nadharia ya uchanganuzi peo, inabainika kuwa wazulufu huhalalisha tabia za kujamiana na ngono za kabla ya ndoa kupitia peo nne za mazungumzo: upeo wa udharura, upeo wa kujihini, upeo wa mamlaka na upeo wa uanishi na utambulisho. Peo hizi za mazungumzo zaweza kuwa kiingilio muhimu cha kuwaelewa wazulufu na kuunda mbinu na sera mwafaka za kukabiliana na changamoto zinazowakumba","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"6 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-10-07","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130521722","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’","authors":"Jotham Muyumba, David Kihara","doi":"10.37284/jammk.5.1.872","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.872","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kueleza muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na jinsi yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (2003). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"6 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-10-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"125451520","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uchanganuzi wa Sitiari Muono katika Mashairi Ruwaza ya Kiswahili","authors":"Nabeta K. N. Sangili","doi":"10.37284/jammk.5.1.861","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.861","url":null,"abstract":"Mashairi ruwaza ni dhana tunayotumia kurejela mashairi ya ‘kimaajabu’ katika taaluma ya ushairi wa Kiswahili. Mashairi haya yamekuwepo tangu miaka ya elfu mbili, hasa katika diwani za Kithaka wa Mberia. Yakilinganishwa na mashairi ya kawaida, mashairi ruwaza yanadhihirisha uchangamano mkubwa katika uwasilishaji maudhui na ufumbuaji wa maana. Hii ni kwa sababu yanatumia vipengele kama vile picha zinazoruwazwa kwa upekee wa maneno, taipografia na sitiari muono kinyume na mashairi ya kawaida yanayotumia maneno pekee na sitiari za kiisimu. Vipengele hivi vinatatiza ufasiri na welewa wa maana ya shairi ruwaza. Hivyo, kazi hii inanuia kuyajadili kwa undani huku tukichanganua mashairi teule ambayo yanapatikana katika diwani za kimapinduzi. Lengo la uchanganuzi huu ni kutajirisha stadi za usomaji na ufasiri wa mashairi ruwaza miongoni mwa wanafunzi na walimu wa ushairi wa Kiswahili. Kazi hii inalenga kujadili namna au mbinu za kufasiri sitiari muono katika mashairi haya","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"59 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"132615903","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi
{"title":"Uhusiano wa Kifahiwa katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Leksika Pragmatiki","authors":"Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi","doi":"10.37284/jammk.5.1.859","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.859","url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kubainisha jinsi fahiwa zinavyohusiana katika leksia za Kîîtharaka kwa kuzingatia mtazamo wa leksika pragmatiki.Ubadili maana katika leksia mbalimbali husababisha kutokea uhusiano wa kifahiwa katika leksia moja, na kati ya leksia mbili au zaidi. Katika makala haya, ubadili maana unaozua uhusiano wa kifahiwa katika leksia za Kîîtharaka umeangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Matokeo yanabainisha kwamba ubadili maana ukitokea katika leksia za Kîîtharaka, mahusiano ya kifahiwa yafuatayo hutokea: uhusiano wa kipolisemia, kihomnimia, kisinonimia, kihaiponimia, kimeronimu na kiantonimu. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na uhusiano na maana nyingine ya leksia iyo hiyo au leksia nyingine tofauti. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha ya leksia.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"34 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"121595594","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}