{"title":"Tathmini ya Aina za Ujumbe Unaoibuliwa Kutokana na Matumizi ya Lugha katika Kuwasilisha Habari za Mazingira katika Gazeti la Taifa Leo, Kenya","authors":"Nelly Nzula Kitonga","doi":"10.37284/jammk.7.1.1936","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1936","url":null,"abstract":"Utafiti huu unahusu aina za ujumbe unaoibuliwa kutokana na matumizi ya lugha katika kuwasilisha habari za mazingira kwenye gazeti la Taifa Leo nchini Kenya. Gazeti la Taifa Leo huwasilisha habari kwa wasomaji kwa lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inatambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya Taifa na pia lugha rasmi sambamba na lugha ya Kiingereza. Mazingira ni suala mtambuko na nyeti kitaifa na kimataifa. Mazingira yanaathiri maisha ya kila kiumbe kila siku kwa njia moja au nyingine. Jamii hupata takriban kila kitu kinachohusiana na mazingira yake kupitia vyombo vya habari. Moja kati ya njia zinazotumiwa na vyombo vya habari kupitisha ujumbe kuhusu mazingira kwa watu ni lugha. Inatarajiwa kwamba, kwa vile vyombo vya habari, Gazeti la Taifa Leo likiwemo, vimetwikwa jukumu la kuwapasha wanajamii yale yanayoendelea duniani kuhusiana na mazingira, vitafanya hivyo kwa namna ambayo itawawezesha watu kufahamu umuhimu wa mazingira na hivyo kuingiliana nayo kwa njia chanya. Hoja hii inatokana na imani kwamba mtu huelewa ujumbe kulingana na jinsi mwasilishi wa ujumbe husika anavyoteua lugha ili kuwasilisha anachokusudia. Madhumuni ya mwandishi wa matini ndiyo yanamwongoza katika uteuzi wa kipengele cha lugha atakachozingatia katika kuandika anachokusudia kuandika. Aidha, lengo la mwandishi wa matini ndilo huamua jinsi atakavyokiwasilisha kile anachokiandika kwa wasomaji. Kwa hivyo, matumizi ya lugha kwa namna tofauti humwezesha mwandishi wa matini kuibua aina tofauti za ujumbe ili kutimiza madhumuni yake. Uchunguzi huu ulidhamiria kubainisha aina za ujumbe uliowasilishwa na waandishi wa habari katika gazeti la Taifa Leo. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo taarifa kuhusu habari za mazingira zilizochapishwa katika gazeti la Taifa Leo zilichanganuliwa. Data ilikusanywa kwa kudondoa matumizi ya lugha katika uwasilishaji wa taarifa za mazingira kutoka magazeti ya Taifa Leo teule pamoja na aina za ujumbe uliojitokeza katika habari hizo.Utafiti huu ulibainisha kwamba kuna aina tofauti za ujumbe katika taarifa za mazingira zilizochunguzwa: maana dhamirifu, maana akisifu, maana athirifu, maana kimtindo, maana halisi na maana ashirifu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"41 2","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141117399","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Dhana ya Kifo katika Mashairi Pepe ya Kumwomboleza Ken Walibora kwenye Kumbi za Kulikoni za Wataalam wa Kiswahili, Africa Mashariki","authors":"Fred Wanjala Simiyu","doi":"10.37284/jammk.7.1.1855","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1855","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza usawiri wa dhana ya kifo katika mashairi pepe yaliyotumiwa na malenga mbalimbali katika kuomboleza kifo cha hayati Ken Walibora. Kifo kinapotokea, wanajamii huomboleza kwa namna tofautitofauti kutegemea mila na desturi za jamii husika Barani Afrika. Kifo cha Ken Walibora kilivuta hisia za malenga wengi ambao walimwomboleza mtunzi mwenzao kwa kutunga mashairi mbalimbali. Katika huko kuomboleza, malenga hawa walieleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora kwa jamii nzima ya Waswahili. Katika makala hii, mashairi pepe sita (6) yalikusanywa kutoka kwenye kumbi za kulikoni za wataalam wa Kiswahili, Afrika Mashariki. Mashairi haya teule yamechambuliwa ili kujibu maswali kama vile; Je kifo cha Ken kilisababishwa na nani? Je, kifo chake kilikuwa kizuri au kibaya? Je, Ken ataendelea kuishi miongoni mwa Waswahili hata baada ya kifo chake? Kifo chake kimesababisha madhara gani katika jamii ya Waswahili? Masuala haya na mengine yamedadavuliwa kwa kuchanganua mashairi teule yaliyotungwa kwa ajili ya kuomboleza kifo cha marehemu Ken Walibora. Uchambuzi huu ulifanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Jazanda. Kwa ujumla, Nadharia ya Jazanda ilitumika katika kupasua istiari zilizotumiwa na malenga katika kueleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora katika mashairi teule","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 28","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-07","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140732725","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Maana za Majina ya Asili ya Watoto katika Jamii ya Waasu","authors":"Janeth Jafet, Perida Mgecha","doi":"10.37284/jammk.7.1.1826","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1826","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza maana za majina ya asili ya watoto katika jamii ya Waasu. Malengo mahususi yakiwa kwanza kubaini majina ya asili ya watoto, na pili kueleza maana zilizobebwa na majina hayo. Utafiti huu ni wa kitaamuli hivyo umetumia usanifu wa kifenomenolojia. Watoataarifa waliohusika katika kutoa data ni 18 ambao wamepatikana kwa mbinu ya usampulishaji tabakishi na usampulishaji tajwa. Data za makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na majadiliano ya vikundi lengwa; kisha zikachanganuliwa kwa mbinu ya kusimba maudhui. Nadharia ya Uumbaji iliyoasisiwa na Sapir (1958) ndiyo iliyotumika katika makala hii. Matokeo yamebainisha majina ya asili ya watoto 145. Maana za majina haya zimegawanyika katika makundi yafuatayo: majina yenye maana zitokanazo na imani kwa Mwenyezi Mungu, mahali mtoto alipozaliwa, wanyama, misimu ya miaka na siku, majanga, vyakula na matukio ya furaha. Utafiti huu una mchango mkubwa katika kuhifadhi historia, na utamaduni uliojificha katika lugha ya Kichasu. Hata hivyo, tafiti zaidi kuhusu majina zifanyike katika jamii nyingine kwani jamii zinatofautiana katika asili, historia, shughuli za kijamii na utamaduni","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"25 63","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-15","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140240188","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"TEHAMA na Athari zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Nchini Rwanda","authors":"Stanislas Munyengabire","doi":"10.37284/jammk.7.1.1795","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1795","url":null,"abstract":"Katika enzi hizi, TEHAMA inatazamwa kama kifaa cha kurahisisha maisha. Inarahisisha maisha kwa kuathiri kila uwanja wa maisha ya mwanadamu (Mikre, 2011). Athari hizi zinajitokeza katika shughuli zote za mtu wa kisasa. Katika uga wa elimu, ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya pili nao uliathiriwa sana kutokana na TEHAMA. Hali hii ilisababisha kuibuka kwa makala haya kutokana na malengo mahsusi matatu. Lengo la kwanza lilikuwa kubainisha mchango wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la pili lilikuwa kuchambua hasara za matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda. Lengo la tatu nalo lilikuwa kubainisha namna ya kutumia TEHAMA katika ufundishaji wa Kiswahili nchini Rwanda. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, usaili, na upitiaji wa maandiko. Sampuli ilikuwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika kidato cha nne katika shule teule za sekondari nchini Rwanda pamoja na wazazi wa wanafunzi hao. Sampuli ilipatikana kwa mbinu ya sampuli lengwa. Utafiti ulioibua makala haya uliongozwa na Nadharia ya Uunganisho. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba TEHAMA ni nyenzo mwafaka katika ufundishaji wa Kiswahili. Hii ni kwa sababu hutumiwa kufundisha msamiati, sarufi na stadi nne za lugha hasa kwa kutumia nyeno kadhaa za kiteknolojia. Aidha, utafiti huu umebaini kwamba TEHAMA inapotumiwa vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wanafunzi. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na kuamini lugha ya mtandaoni zaidi, maandishi ya mkononi (kalamu) mabaya, kuathiriwa na tabia na damaduni za nje, na kutokubaliana kati ya mwalimu na wanafunzi juu ya masomo. Mwishoni, makala imejadili namna ya kuitumia TEHAMA katika ufundishaji wa lugha ya pili hususan nchini Rwanda","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"5 6","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-15","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140241229","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Mercy Moraa Motanya, Boniface Ngugi, Stephen Njihia Kamau
{"title":"Mikakati ya Udumishaji wa Lugha ya Kishona Nchini Kenya","authors":"Mercy Moraa Motanya, Boniface Ngugi, Stephen Njihia Kamau","doi":"10.37284/jammk.7.1.1824","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1824","url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kuchunguza mikakati mbalimbali inayotumiwa na Washona katika kudumisha lugha ya Kishona nchini Kenya. Washona ni Wabantu ambao asili yao ni nchi ya Zimbabwe na walifika nchini Kenya kuanzia mwaka wa 1959 kwa lengo la kuhubiri injili kupitia kwa dhehebu la Gospel of God. Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya hasa katika kaunti ya Kiambu iliyo na hali ya wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai ambayo ni makazi ya Washona wengi wanaoishi nchini Kenya. Mtagusano wa lugha mbalimbali waweza kuhatarisha uthabiti wa kiisimujamii wa lugha ambayo ina idadi ndogo ya wazungumzaji na ambayo haina usaidizi kutoka asasi mbalimbali za kiserikali. Hali hii ndiyo inayoikabili jamiilugha ya Washona nchini Kenya. Makala haya yaliongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977) ambayo iliendelezwa na O’Riagain (1994). Kupitia kwa mhimili wake wa kwanza unaosema kwamba kila kizazi hubuni na kuweka mikakati ya kurithisha kizazi kinachofuata utamaduni wake, nadharia hii inasisitiza mikakati ambayo jamiilugha huweka ili kudumisha lugha ambayo ni kipengele muhimu cha utamaduni. Utafiti huu ulifanyikia maktabani na nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyikia kwenye maeneo ambayo wanajamiilugha wa Kishona huishi ili kupata data iliyobainisha mikakati ambayo Washona wanatumia ili kudumisha lugha yao ya Kishona nchini Kenya. Jumuiya ya utafiti ilikuwa jamiilugha ya Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji wa data ni mahojiano, uchunzaji na mijadala ya vikundi vidogovidogo. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na kuongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ni wa manufaa kwa Washona wenyewe, taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi lugha ya Kishona nchini Kenya","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 4","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-14","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140241783","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Helina Wanjiku Njuguna, G. K. King'ei, R. M. Wafula
{"title":"Hali ya Kipindi cha Kupigania Uhuru na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili Kati ya Miaka 1930 Hadi 1960 Nchini Tanzania","authors":"Helina Wanjiku Njuguna, G. K. King'ei, R. M. Wafula","doi":"10.37284/jammk.7.1.1804","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1804","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza jinsi hali ya kipindi cha kupigania uhuru ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia kipindi cha kupigania uhuru nchini Tanganyika. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”, Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa kuwa washairi walishiriki katika siasa. Vyama vya kisiasa vilitumia Kiswahili kama chombo cha kuunganisha Watanganyika kisiasa. Mashairi yaliandikwa katika magazeti ili kuhamasisha na kuzindua watu wapiganie uhuru. Mashairi yalibeba maudhui ya dhuluma za kikoloni, utetezi wa haki, umoja wa Waafrika, uzalendo, chama cha TANU, uhuru, sifa za viongozi bora, madaraka na utamaduni wa Waafrika","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"21 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-06","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140262417","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mikabala Tofauti ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada kuhusu Kipengele cha Mtindo wa Uandishi Insha za Kiswahili Nchini Kenya","authors":"Nester Ateya, Eric W. Wamalwa, S. A. Kevogo","doi":"10.37284/jammk.7.1.1803","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1803","url":null,"abstract":"Makala haya yanabainisha mikabala ya waandishi wa vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili kwa shule za upili nchini Kenya. Mikabala tofauti ya waandishi aghalabu huwa chanzo cha utata miongoni mwa walimu na wanafunzi na hivyo kuathiri matokeo ya mtihani wa kitaifa. Uchunguzi huu umekitwa kwa mihimili ya Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Louis Tonko Milic. Nadharia hii inashikilia kuwa mtindo hutegemea mtu binafsi. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo, mkabala wa kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ni walimu wa somo la Kiswahili 73, wanafunzi 2,000 na vitabu vya kiada 7 vya shule za upili. Kwa hivyo, usampulishaji wa kimakusudi ulitumiwa kuteua walimu 22, wanafunzi 320 na vitabu vya kiada 6. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo, mahojiano na hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia asilimia, majedwali na kuwasilishwa kiufafanuzi. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kwamba, matumizi ya vitabu vya kiada tofauti tofauti yanazua mikabala tofauti katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha. Hali hii inatokana na waandishi wa vitabu kiada kuwa na mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha za Kiswahili. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, viwango vingine vya elimu na wakuza mitaala pamoja na waandishi wa vitabu vya kiada. Wizara ya Elimu pamoja na vyuo vya walimu kupitia warsha na maarifa zaidi ya yale ya vitabu vya kiada, watafaidi mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa somo la insha","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"94 12","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-06","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140261213","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili","authors":"N. N. Musembi, Fred Wanjala Simiyu","doi":"10.37284/jammk.6.2.1617","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1617","url":null,"abstract":"Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed. Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuata ili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao. Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu. Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongoni mwa vijana kote duniani. Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee. Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee. Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii. Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii. Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia. Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo. Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data. Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teule na kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti. Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 3","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-12-09","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"138585671","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili.","authors":"Christine Nyougo, Peter Githinji","doi":"10.37284/jammk.6.1.1564","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1564","url":null,"abstract":"Makala hii inadhamiria kuonyesha athari ya viarudhi vya Ekegusii kwa matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu. Wasailiwa wetu ni wanafunzi wa shule tatu za upili zinazopatikana katika eneo la Kisii. Tulijikita katika nadharia ya Mennen (2015) ya ujifunzaji wa kiimbo katika lugha ya pili. Nadharia hii huchunguza matatizo ambayo wajifunzaji wa lugha ya kwanza hupata wakati wa kujifunza kiimbo cha lugha ya pili. Tumejikita kwa mantiki kuwa mtagusano baina ya lugha moja na nyingine huweza kuibua kufanana au kutofautiana kimatumizi katika uenezaji wa viimbo tofauti. Tumetumia mihimili minne katika uchanganuzi wa data tuliyopata nyanjani. Mhimili wa kimfumo unashughulikia vipengele vya kiarudhi katika lugha husika na usambazaji wake, mhimili wa utekelezaji unashughulikia utaratibu wa namna ambavyo vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotekeleza majukumu yavyo katika lugha husika. Mhimili wa ujirudiaji unaangazia kiwango cha matumizi ya vipengele hivi vya fonolojia ambapo lugha hutofautiana katika kiwango cha matumizi ya vipengele vyake na mhimili wa kisemantiki unaoshughuklika maana inayopatikana kutokana na matumizi ya viarudhi husiaka. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumiwa katika kuteua wanafunzi wa vidato tofauti katika shule tatu teule na walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizo. Data yetu ilitokana na hojaji, mahojiano usomaji wa sentensi pamoja na kifungu ambacho kilikuwa na aina nne za viimbo ambapo wasailiwa walizisoma kwa sauti. Data ya ziada ilitokana na usomaji wa sentensi nane za Ekegusii zenye kiimbo cha taarifa, swali, amri na mshangao ambazo zilisomwa na walimu wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza katika shule hizo tatu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kupitia ufasili wa data ya hojaji, mahojiano na uchunzaji wa kushiriki. Matokeo tuliyopata yalibainisha kuwa uhawilisho wa viarudhi hivi kwa kiwango kikubwa huathiri matumizi sahihi ya kiimbo cha Kiswahili ambapo wasailiwa wa lugha ya kwanza hurudufu baadhi ya vipengele vya lugha hiyo katika kiimbo cha lugha ya pili. Matokeo haya pia yalidhihirisha kuwa maumbo ya silabi katika Ekegusii, shadda, toni na wakaa huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"113 22","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135138110","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Taswira ya Distopia katika Riwaya ya Kimajaribio ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Bina-Adamu na Dunia Yao","authors":"Mwove Phyllis Mwende, Alex Umbima Kevogo","doi":"10.37284/jammk.6.1.1556","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1556","url":null,"abstract":"Mustakabali wa Bara la Afrika umekuwa suala la msingi katika maudhui ya riwaya ya kisasa ya Kiswahili. Fasihi ya kimajaribio inayoakisi hali za kidistopia inachora taswira hasi za mustakabali wa Bara la Afrika. Mazingira ya kidistopia ni mandhari yanayokabiliwa na kila aina ya matatizo au uovu uliokithiri ambayo huwa ya kiubunifu. Dhana hii hutumiwa kueleza jamii ambayo sheria zake hubadilishwa na kuishia kuwa za kuwadhalilisha wanajamii kupita kiasi. Kwa ujumla, wanajamii wanaojipata kwenye ulimwengu wa aina hii huwa kwenye njiapanda. Wanajamii hao huwa wamekwisha poteza tumaini la kuishi kutokana na dhuluma zinazowakabili. Baadhi yao hutamaushwa na ugumu wa maisha na kutamani kuangamia au kujiangamiza ili kuepuka ulimwengu huo wa shida. Kazi za fasihi zinazofuata mkondo wa kidistopia hudhamiria kutoa tahadhari au kuhamasisha jamii kuwajibika ili kuepuka maangamizi yanayokuja. Kazi hizo ni za utabiri wa mambo yanayoweza kutokea baadaye. Makala hii inakusudia kuonyesha jinsi taswira ya kidistopia inavyojitokeza katika riwaya ya kimajaribio ya Kiswahili kwa kutumia Nadharia ya Usasabaadaye ilioasisiwa na Linda Hutcheon na kufafanuliwa zaidi na Patricia Waugh. Riwaya mbili za kimajaribio; Dunia Yao (2006) ya Said Ahmed Mohamed na Bina-Adamu! (2002) ya Kyallo Wadi Wamitila zilitueliwa kimaksudi ili kuonyesha jinsi taswira ya distopia inavyobainika. Utafiti ulifanywa maktabani. Data ilikusanywa kutokana na usomaji wa kina wa riwaya teule ulioongozwa na mihimili ya Nadharia ya Usasabaadaye. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo kwa mujibu wa Nadharia ya Usasabaadaye. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa waandishi wana sababu za kimsingi za kusawiri mandhari ya kidistopia ili kutoa taswira kamili ya nchi za Kiafrika katika muktadha wa baada ya ukoloni chini ya utandawazi, mfumo wa soko huria, ubeberu mpya, ubinafsi, taathira za kigeni na uporomokaji wa kasi wa nguzo za maisha ya Kiafrika","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"81 4","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135725271","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}