East African Journal of Swahili Studies最新文献

筛选
英文 中文
Uchunguzi wa Mielekeo ya Walimu na Wanafunzi Kuhusu Mbinu na Nyenzo za Kufundishia Kiswahili Katika Shule za Upili za Umma, Kaunti za Kisumu na Kakamega, Kenya Uchunguzi wa Mielekeo ya Walimu na Wanafunzi Kuhusu Mbinu na Nyenzo za Kufundishia Kiswahili Katika Shule za Upili za Umma, Kaunti za Kisumu na Kakamega, Kenya
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-11-03 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1551
Linnah Apondi Okeyo, John N. Kimemia, Sophia M. Ndethiu
{"title":"Uchunguzi wa Mielekeo ya Walimu na Wanafunzi Kuhusu Mbinu na Nyenzo za Kufundishia Kiswahili Katika Shule za Upili za Umma, Kaunti za Kisumu na Kakamega, Kenya","authors":"Linnah Apondi Okeyo, John N. Kimemia, Sophia M. Ndethiu","doi":"10.37284/jammk.6.1.1551","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1551","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza mielekeo ya walimu na wanafunzi kuhusu mbinu na nyenzo zlizotumiwa wakati wa kufunza Kiswahili katika shule za upili katika Kaunti za Kisumu na Kakamega nchini. Lengo la utafiti huu lilikuwa kutambua mbinu na nyenzo zilizotumiwa na walimu pamoja na wanafunzi wao kufunza na kujifunza Kiswahili pamoja na mielekeo yao kuzihusu.Utafiti ulilenga idadi ya walimu na wakuu wa idara 12 katika kila Kaunti pamoja na wanafunzi 960. Data ilikusanywa kupitia hojaji za wanafunzi na walimu, mwongozo wa usaili kwa wakuu wa Idara ya Kiswahili pamoja na uchunguzi wa darasani. Data zilichanganuliwa kwa kutumia Toleo la takwimu 13 kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi.Mbinu walizochangamkia wanafunzi masimulizi, mihadhara na maonyesho) sizo zilizotumiwa na walimu kila mara kuwafunza. Mbinu za kikoa, na mseto pamoja na usomaji mpana na wa kina (vitabu vya ziada, viteule na gazeti la Taifa Leo) zilitumika sana Kakamega hali iliyochangia matokeo yao kuwa bora kiasi kuliko ya Kisumu. Mbinu za jadi zilichangamkiwa zaidi katika kaunti zote madjhali mbinu za kidijitali hazikutumiwa sana.Ilibainika kuwa pana uhusiano kati ya mielekeo, utendakazi na matokeo ya wanafunzi somoni; mielekeo chanya iliathiri utendakazi na matokeo kwa namna chanya bali mielekeo hasi ikiathiri haya yote kwa namna hasi. Walimu waboreshe mbnu na nyenzo wanazozitumia kufunza Kiswahili ili matokeo yake yapate kuimarika zaidi katika shule zote, kaunti zote na nchini","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"36 4","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-03","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135868388","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Uchunguzi wa Changamoto za Walimu na Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya Uchunguzi wa Changamoto za Walimu na Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-10-26 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1538
Linnah Apondi Okeyo, John N. Kimemia, Sophia M. Ndethiu
{"title":"Uchunguzi wa Changamoto za Walimu na Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya","authors":"Linnah Apondi Okeyo, John N. Kimemia, Sophia M. Ndethiu","doi":"10.37284/jammk.6.1.1538","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1538","url":null,"abstract":"Lengo la utafiti ni kuchunguza changamoto walizokabiliana nazo walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili nchini. Kiswahili ni lugha rasmi na ya taifa nchini Kenya tena ni somo la lazima linalofundishwa na kutahiniwa katika shule za msingi na za upili. Kimataifa, ni lugha inayotambuliwa kama chombo cha mawasiliano. Kuimudu lugha hubainika kupitia ujuzi wa mtu katika stadi zake kuu; kusoma, kuandika, kusikiliza, na kuongea. Umilisi na utendaji katika lugha hata hivyo huweza kuathiriwa pakubwa na mambo kadhaa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Utabia na Utambuzi. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya na ulinganishi, vifaa vilivyotumiwa kukusanya data vilikuwa hojaji, mahojiano, mtihani wa insha na uchunguzi darasani. Sampuli lengwa ilifikiwa kwa kutumia usampulishaji maksuudi na nasibu. Data ilichanganuliwa kitakwimu kwa kutumia uchanganuzi wa tarakimu na maelezo. Utafiti huu uligundua kuwa wanafunzi pamoja na walimu walipata shida kadhaa hali iliyoathiri kwa njia hasi ufunzaji na ujifunzaji wao. Licha ya kutambua umuhimu wa mwelekeo mseto katika ufunzaji, walimu wengi hawakutumia mbinu hii kufunza kutokana na ukosefu wa vifaa na nyenzo za kufunzia, uhaba wa muda, idadi kubwa ya wanafunzi madarasani mwao, uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa ujuzi maalum katika mbinu mseto. Pana haja kuu walimu waelekezwe vilivyo katika mbinu mwafaka za kufunzia, wanafunzi wahamasishwe kuhusu umuhimu wa somo hili, wachapishaji kuelekezwa vilivyo katika maswala yanayofunzwa katika kila kiwango na ukaguzi wa kina kufanywa ili kuondoa mambo yanayoweza kuwakanganya walimu na wanafunzi. Utafiti zaidi unaweza kufanywa katika vipengele vya Lugha na Fasihi ya Kiswahili ili kutambua changamoto zinazoshuhudiwa katika ufunzaji wao ili kuzitatua ipasaavyo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"22 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-10-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"134908368","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mabadiliko katika Maudhui, Mtindo na Muundo Katika Fasihi 马巴迪里科(Mabadiliko katika Maudhui)、姆廷多(Mtindo)和穆恩多(Muundo)(Katika Fasihi)。
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-10-22 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1531
Simon Kiarie Mwangi, Naomi Ndumba Kimonye
{"title":"Mabadiliko katika Maudhui, Mtindo na Muundo Katika Fasihi","authors":"Simon Kiarie Mwangi, Naomi Ndumba Kimonye","doi":"10.37284/jammk.6.1.1531","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1531","url":null,"abstract":"Fasihi na jamii ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutenganishwa. Kwamba fasihi humulika yaliyo katika jamii na kwa upande mwingine jamii hutumia fasihi kuendeleza amali zao. Hivyo basi fasihi huwa kama kioo cha jamii kwa kuangazia tamaduni za jamii husika. Tamaduni za jamii husika hubadilika zinapoathiriwa kidaikronia. Kwa msingi huu fasihi hubadilika kulingana na mabadiliko yatokeao katika jamii hiyo. Makala haya yanadhamiria kuchunguza mabadiliko hayo ya kimaudhui, kimutindo na kimuundo katika fasihi ya kisasa kwa kuilinganishwa na fashi ya kale. Mabadiliko ni hali ambayo jamii fulani huchukua mambo mapya yanayotokea na kuyakubali kama sehemu ya utamamdi wayo. Kuna mabadiliko anuwai ambayo yameshuhudiwa katika uandishi wa kazi za fasihi za Kiswahili katika maudhui, wahusika, muundo na mtindo. Kazi za fasisi zitakazochunguzwa ni fasihi andishi hasa mashairi, riwaya, hadithi fupi na tamthilia. Lengo kuu la makala haya ni kutathimini mabadiliko hayo kwa kuchunguza asili yake na athari zake katika fasihi ya kisasa. Fasihi huwakilisha yanayotokea katika jamii na waandishi hutumia ubunifu wao kuyaangazia. Maudhui, wahusika, ploti na mtindo katika fasihi andishi hutokana na mambo yaliyo katika jamii. Kimsingi, utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Msambao wa Uvumbuzi. Nadharia hii inatambua hatua tatu kuu zinazohusishwa na usambazaji wa maudhui. Hatua hizi ni uvumbuzi, usambaaji na ukubalifu. Hatua hizi tatu za nadharia hii zilitumiwa kuendeleza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilitoka maktabani na iliteuliwa kwa njia ya kimakusudi kutoka vitabu teule vya Kiswahili. Data ilikusanywa kwa kusoma vitabu, majarida na kusakura mtandaoni kupata data inayohusiana na kazi hii. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kimaelezo kwa kulinganisha kazi za fasihi za kale na kisasa. Matokea ya utafiti huu yalionyesha kuwa kuna mabadiliko yanayoshuhudiwa katika fasihi ya sasa hasa katika maudhui, mtindo na wahusika. Kwa mfano, imebainika kuwa mashairi ya kisasa yanalenga zaidi kupitisha ujumbe kuliko kubanwa na muundo wa mashairi arudhi. Matokea ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa waandishi wa kazi za fasihi, wanafunzi katika viwango tofauti vya elimu na wasomi katika nyanja tofauti kama anthropojia","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"20 4","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-10-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135461693","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008) Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili:Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-10-18 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1524
Felix Musyoka Kalingwa, Titus Musyoka Kaui
{"title":"Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)","authors":"Felix Musyoka Kalingwa, Titus Musyoka Kaui","doi":"10.37284/jammk.6.1.1524","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1524","url":null,"abstract":"Makala hii inashughulikia athari za Katama Mkangi kwa John Habwe kwa kujikita katika riwaya teule za Kiswahili za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008). Utanzu wa riwaya ya Kiswahili umeendelea kupanuka kimaudhui na kifani kutokana na juhudi za watunzi mbalimbali kama vile Katama Mkangi na John Habwe. Japo tafiti za awali zimetafitia suala la mwingiliano matini, tafiti nyingi zimejikita katika kazi za mtunzi mmoja. Utafiti wa kina ulihitajika kuchunguza namna utunzi wa Mafuta (1984) ulivyoathiri John Habwe alipoitunga riwaya yake ya Cheche za Moto (2008). Katama Mkangi aliandika riwaya ya Mafuta katika wakati wa chama kimoja cha kisiasa ambapo uhuru wa kujieleza ulikuwa umebanwa sana. Habwe ameandika kazi yake katika mazingira yaleyale lakini katika kipindi ambapo uhuru wa kujieleza umepanuliwa. Kwa hivyo, amekwepa mtindo wa kimajazi alioutumia Mkangi na kuyaangazia masuala anayoyaibua kwa njia wazi. Makala hii ililenga kuonyesha kuwa maudhui katika riwaya ya Cheche za Moto ni mwangwi unaotokana na riwaya ya Mafuta (1984). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1969). Mihimili mikuu ya nadharia hii iliyoongoza utafiti huu ni pamoja na: hakuna matini ya fasihi yenye sifa za pekee, matini hubainisha sifa mbalimbali za matini tangulizi, na mwisho, matini ya baadaye huweza kufafanua dhana fulani kutoka matini tangulizi kwa njia inayoeleweka. Nadharia hii ya mwingiliano matini ilisaidia pakubwa kuonyesha namna kazi ya awali, Mafuta (1984) ilivyomwathiri John Habwe katika utunzi wa Cheche za Moto (2008) kimaudhui. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi ili kupata sampuli faafu yenye data ya kujaza pengo la utafiti. Data ilikusanywa kupitia kwa usomaji wa maktabani na vilevile kusakura mitandaoni kuhusu vipengele vya mwingiliano matini katika riwaya ya Kiswahili. Data hii imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti wa makala hii unatarajiwa kutoa mchango katika uhakiki wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili, hususan kuhusu kipengele cha kuathiriana baina ya watunzi wa riwaya za Kiswahili","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"47 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-10-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135884889","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mbinu Za Lugha Katika Nyimbo Teule Za Mapenzi Kwenye Kipindi Cha Mambo Mseto Cha Redio Citizen Mbinu Za Lugha Katika Nyimbo Teule Za Mapenzi Kwenye Kipindi Cha Mambo Mseto Cha Redio Citizen
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-27 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1468
Lydia Chelagat, Rebecca Wanjiku-Omollo, Margan Adero
{"title":"Mbinu Za Lugha Katika Nyimbo Teule Za Mapenzi Kwenye Kipindi Cha Mambo Mseto Cha Redio Citizen","authors":"Lydia Chelagat, Rebecca Wanjiku-Omollo, Margan Adero","doi":"10.37284/jammk.6.1.1468","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1468","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza mbinu za lugha katika nyimbo za mapenzi kwenye kipindi cha Mambo mseto cha Redio Citizen. Nadharia iliyotumika ni Nadharia ya mtindo iliyoasisiwa na Buffon (1930) na kuendelezwa na watafiti wengine. Muundo uliotumika ni mkabala mseto kuegemea muundo wa QUAL-quan. Sampuli za maksudi zilitumika kukiteua kipindi cha Mambo mseto na wanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika Mashariki. Wanafunzi 83 kutoka chuo kikuu cha Kikatoliki cha Afrika mashariki walifanyiwa utafiti. Nyimbo saba kuashiria asilimia 30 kutoka jumla ya nyimbo ishirini na nne za mapenzi zilizochezwa ziliteuliwa. Uteuzi wa nyimbo hizo saba uliongozwa na maoni ya Fink (2003) anayesema kuwa, kwa watafitiwa chini ya 1000, jumla ya asilimia 30 ya usampulishaji hutumika. Hivyo katika utafiti huu, mtafiti alichukua ailimia 30 ya nyimbo 24 alizosikiza akapata nyimbo saba. Matokeo ya utafiti yalibaini kuwa mbinu za lugha zinazodhihirika katika nyimbo za mapenzi zilizochunguzwa ni kuchanganya ndimi, takrikiri, Chuku, tasfida, sitiari na tashbihi. Utafiti huu ulipendekeza watunzi wa nyimbo za mapenzi watumie pia mbinu nyingine za lugha kama vile methali ambayo haikujitokeza sana. Watafiti wengine pia wafanye utafiti kuhusu mbinu za lugha kwenye aina nyingine za nyimbo. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa vyombo vya habari haswa stesheni za redio ili wafahamu mchango wao kwa ujenzi wa lugha ya Kiswahili kwani wao ndio husambaza na kucheza nyimbo hizi za mapenzi. Vilevile utafiti huu utakuwa na mchango katika kuleta ushirikiano mzuri wa kiakademia katika jumuiya ya Afrika mashariki kwa vile ilitafiti nyimbo kutoka Kenya, Uganda na Tanzania","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"42 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135537162","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Dhima za Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo za Singeli: Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo Dhima for Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo for Singeli:Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-27 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1470
Baraka Sikuomba, Lina Godfrey
{"title":"Dhima za Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo za Singeli: Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo","authors":"Baraka Sikuomba, Lina Godfrey","doi":"10.37284/jammk.6.1.1470","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1470","url":null,"abstract":"Kutokana na ufinyu wa tafiti zilizofanyika kuhusu tasifida katika muktadha wa nyimbo za singeli kumejengeka mtazamo hasi hasa kwenye lugha inayotumika katika muktadha wa nyimbo za singeli miongoni mwa wanajamii. Kutokana na umuhimu wa tasifida katika kuendeleza utamaduni wa jamii kulikuwa na haja ya kuchunguza na kuweka bayana dhima za matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli. Kwa hiyo, makala hii imeangalia dhima za tasifida kimuktadha katika nyimbo za singeli kwa kutumia nyimbo ziitwazo “Siponaye”, “Dada Asha”, “Spesho”, “Mtoto Mdogo” za msanii Msaga Sumu na “Chawa”, “Hainogi”, “Kitasa”, “Mashine” “Kipusa”, “Muacheni Adange” za msanii Manfongo. Nadharia ya Semiotiki imetumika kufafanua dhima za tasifida katika nyimbo za wasanii teule. Katika nyimbo hizo tasifida mbalimbali zimetumiwa na wasanii teule kuwasilisha maudhui yao. Nyimbo hizi za singeli, licha ya kuimbwa kwa lugha inayoonekana ni ya mtaani, zimezingatia sana matumizi ya tasifida katika kupunguza ukali wa maneno. Matokeo ya utafiti huu yameonesha wazi kuwa matumizi ya lugha ya tasifida katika nyimbo za singeli, yameonesha wazi kwamba nyimbo za singeli zina dhima kadha wa kadha zinazowasilishwa kwa njia ya matumizi ya tasifida. Kupitia matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli, ni bayana kwamba tasifida zina dhima za msingi katika nyimbo za singeli katika kuendeleza mila, utamaduni na desturi za mawasiliano katika jamii. Dhima hizo ni pamoja na kubainisha kazi zisizo halali katika jamii, kuibua tabia zisizokubarika katika jamii, kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii, kuhimiza umuhimu wa mapenzi ya dhati katika jamii na kuweka bayana uhalisia wa mwanaume. Hivyo basi, watafiti wengine wanaweza kufanya utafiti kama huu kwa kuchunguza kwa kina tofauti ya tasifida na taswira kimuktadha katika nyimbo teule za utafiti huu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"52 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135537186","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-27 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1469
Nelly Bonareri Karoli, Leonard Chacha Mwita
{"title":"Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya","authors":"Nelly Bonareri Karoli, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.6.1.1469","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1469","url":null,"abstract":"Lugha na utamaduni wa watu ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Mifumo ya lugha huathiri namna binadamu anavyofikiri kuhusu ulimwengu wake na husababisha matendo ambayo ni kiini cha changamoto za kiikolojia wanazokabiliana nazo. Katika makala hii, tulichambua namna leksimu za mitishamba zinachukuliwa kama ishara za uhifadhi wa mazingira katika mifumo ya ikolojia katika jamii ya Waswahili. Data ilikusanywa kwa mbinu ya mahojiano kutoka kwa Waswahili wa Mvita. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki ikolojia iliyotusaidia kuelewa kuwa kile kilichotambuliwa kama athari kwa ikolojia mara nyingi huwa na sababu za kisemiotiki na tofauti katika kufasiri ishara au misamiati. Tulibainisha kuwa kuna leksimu za mitishamba kama ‘mpambamwitu’ ambayo Waswahili walitumia kuonyesha ile hali ya kurembesha misitu yao kwa kuleta taswira ya kiasili na mwonekano mzuri wa kipekee, ‘linda ziwa’ iliakisi uhifadhi wa vyanzo vya maji. Mahali ambapo ulimea, maji yalikuwa safi na tayari kutumika katika shughuli za pale nyumbani. Mti huu ulifananishwa na jokofu kwani hata nyakati za joto ulipoenda mtoni ungepata maji hayo ni baridi na safi. Waswahili ambao walikuwa ni watumiaji wa leksimu hizi walionyesha kuwa ilipofikia suala la uhifadhi wa mazingira, wanajamii walijitahidi kutunza mazingira yao. Jinsi tunavyochagua misamiati yetu katika mawasiliano kuhusu mazingira kunaweza kubadilisha jinsi wanajamii wanavyoyaona mazingira hayo. Ikolojia inategemea mawazo yaliyopo, kanuni, na sheria za jamii. Makala hii imapendekeza kuwa kwa kubadilisha jinsi tulivyoyatazama mazingira yetu ya asili tunaweza kutambua thamani yake halisi. Kwa kuiweka thamani hiyo katika sera zetu mipango na mifumo ya uchumi, tunaweza kuelekeza uwekezaji katika shughuli ambazo zinarejesha uasili wa mazingira yetu na tukapata faida. Kwa kutambua kuwa mazingira yetu ni mshirika wetu mkubwa basi tutayafanya kuwa endelevu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"117 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135537151","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Sifa Za Wahusika Za Kisimulizi Katika Ngano Za Wachuka Sifa Za Wahusika Za Kisimulizi Katika Ngano Za Wachuka
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-27 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1467
Rebecah Wanja Kirimi, Martin Mugambi Allan, Onesmus Gitonga Ntiba
{"title":"Sifa Za Wahusika Za Kisimulizi Katika Ngano Za Wachuka","authors":"Rebecah Wanja Kirimi, Martin Mugambi Allan, Onesmus Gitonga Ntiba","doi":"10.37284/jammk.6.1.1467","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1467","url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kujadili sifa za wahusika wa kisimulizi zilivyoendelezwa kiujumi katika ngano simulizi za Wachuka, kwa kuongozwa na nadharia ya Ujumi wa Kinudhuma inayotetea upekee wa kiujumi wa kazi za kisanaa. Madhumuni ya Makala yalikuwa kuchanganua sifa za wahusika wa kisimulizi katika ngano za Wachuka na namna wanavyoendeleza ujumi katika ngano husika. Makala haya yalibaini kwamba wahusika katika ngano za wachuka hugawika mara mbili yaani wahusika wawi na wahusika wema ili kujenga ujumi katika ngano. Mbinu elezi ilitumika kuwasilisha na kuchanganua data","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"49 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135537189","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo 在肯尼亚的 Shule za Upili 中使用斯瓦希里语,在肯尼亚的 Mawasiliano 中使用 Uongozi wa Kidini:肯尼亚的 "Wasichana ya Itigo "计划
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-11 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1422
Joachim Kipchirchir Melly, Ernest Sangai Mohochi
{"title":"Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo","authors":"Joachim Kipchirchir Melly, Ernest Sangai Mohochi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1422","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1422","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake Dell Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidini wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"55 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-11","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"135982244","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2023-09-09 DOI: 10.37284/jammk.6.1.1419
John Muriuki Ireri, Onesmus Ntiba
{"title":"Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki","authors":"John Muriuki Ireri, Onesmus Ntiba","doi":"10.37284/jammk.6.1.1419","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1419","url":null,"abstract":"Makala hii inahusu utathmini wa maudhui katika nyimbo teule za msanii Newton Kariuki. Nyimbo ni moja wapo ya njia zinazotumiwa na wasanii kuwaslisha ujumbe unaowahusu jamii. Utafiti huu ulitumia nadharia ya mseto, yaani nadharia ya umtindo ile ya udenguzi. Nadharia ya umtindo inasisitiza kuwa lugha ina sehemu mbili zinazodhihirika katika usemaji; lugha ni dhahiri na dhahania. Aidha, nadharia ya udenguzi huashiria mgogoro usiosuluhika uliopa baina ya usemi balagha na mawazo kwamba kuna pengo kati ya inachokusudia kusema kazi ya fasihi na inacholazimika au kuelekezwa kusema. Hivyo kuna mvuto katika ya usemi na mantiki. Utafiti ulichukua muundo wa kimaelezo. Mtafiti aliteua kimakusudi jumla ya nyimbo kumi zilizoimbwa na mwanamuziki Newton Kariuki, yaani tano za Kiswahili na tano za Kimbeere. Kutokana na jumla ya nyimbo hamsini alizokuwa ameimba kufikia muda wa kufanya utafiti. Data ilikusanywa kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Waaidha, data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya utafiti ni kuwa sampuli iliyoteuliwa ilisheheni maudhui ya mapenzi, ndoa na familia, migogoro katika ndoa, kuporomoka kwa maadili, uongozi na siasa, umaskini, uhalifu, mawaidha, UKIMWI na dini na imani. Maudhui haya yaliakisi maisha katika ulimwengu wa kiuhalisia. Umuhimu wa makala hii ni kuwa matokeo haya yanadhihirisha kuwa mwimbaji yeyote halengi tu kuburudisha bali kuelimisha. Hivyo makala hii inapendekeza utafiti wa baadae ufanywe kwa kuzingatia mahusiano ya uwezo wa kiuana katika sampuli teule","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"7 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-09-09","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"136107793","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
相关产品
×
本文献相关产品
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信