{"title":"Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000","authors":"Elihaki Yonazi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1395","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1395","url":null,"abstract":"Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika. Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi. Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake. Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika. Makala hii imetumia data za maktabani. Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika. Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule. Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule. Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili. Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura. Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"342 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-08-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"115400997","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo","authors":"Jemima Lenjima, Julius Edmund Frank","doi":"10.37284/jammk.6.1.1396","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1396","url":null,"abstract":"Miaka ya hivi karibuni majina ya asili katika jamii nyingi za kitanzania yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya kupotea kwa kasi hasa kwa vijana kutokana na ujio wa sayansi na teknolojia pamoja na dini. Makala haya yamekusanya na kubainisha majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo. Makala yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali hilo linauliza; Majina yapi ya asili ya watu yanayotumika katika jamii-lugha ya Wagogo? Mbali na kujadili swali hilo muhimu, Makala haya pia yametoa mapendekezo kuhusu njia za kuendeleza matumizi ya majina ya asili ya watu katika jamii-lugha husika. Data za makala zimekusanywa kwa mbinu ya mahojiano na majadiliano ya kundi lengwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali kwa ufafanuzi zaidi. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Uumbaji ya (Sapir-Whorf, 1958) inayosisitiza kwamba, lugha ndio msingi wa kuuelewa ulimwengu. Unapojifunza lugha hiyo hata dunia unayoiumba akilini mwako itatokana na dunia iliyoratibiwa na wasemaji wake. Matokeo ya uchunguzi wa makala haya yamedhihiridha kuwa, majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo yapo katika makundi kulingana na jinsi yanavyotolewa au kupatikana. Makundi yamebainishwa kwa kuzingatia sifa zinazofanana katika makundi mbalimbali","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-08-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128691387","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Tamthilia ya Kiswahili katika Ukuaji na Ustawi Endelevu wa Ujasiriamali Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari","authors":"Furaha J Masatu","doi":"10.37284/jammk.6.1.1377","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1377","url":null,"abstract":"Ujasiriamali ni wimbo unaozidi kurindima masikioni mwa wanajamii. Wimbo huu unatokana na changamoto ya fursa funge za ajira miongoni mwa vijana. Tatizo linaonekana kuwa kubwa kwa sababu vijana wengi hawaonekani kuwa na msukumo wa ndani na wa kimazingira wa kujiajiri. Vijana wengi bado wanaamini katika kuajiriwa badala ya kujiajiri ilhali fursa za ajira rasmi wazitakazo ni chache kuliko idadi yao. Serikali na wadau wa maendeleo, wanazidi kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii ya ajira miongoni mwa vijana. Mojawapo ya mapendekezo ya kutatua changamoto hii, ni kwa serikali na wadau kuwawezesha vijana kujikomboa kifikra kupitia elimu na mazingira rafiki kwa ujasiriamali. Baadhi ya wadau, wanaamini elimu rasmi ya ujasiriamali katika shule ya msingi na sekondari ndiyo suluhu kwa vijana kufikiria kujiajiri. Hata hivyo, kuna hoja kuwa wadau wa elimu wamechelewa sana kuiteua tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari kuwa tamthilia ya kiada miongoni mwa tamthilia rasmi zinazopaswa kufundishia na kujifunza uhakiki wa fasihi na ujasiriamali katika ngazi ya sekondari na vyuo. Hivyo, makala haya yanawasilisha sehemu ya matokeo ya uchunguzi tulioufanya kuhusiana na maudhui ya tamthilia ya Safari ya Chinga ili kuonesha nafasi adhimu ya Tamthilia ya Kiswahili katika ukuaji na ustawi endelevu wa ujasiriamali nchini Tanzania.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"10 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-08-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"129763863","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Kuchambua Mbinu za Kiaristotle na Zisizo za Kiaristotle katika Tamthiliya ya Sadaka ya John Okello","authors":"Emmanuel Oscar Msangi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1371","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1371","url":null,"abstract":"Uandishi wa tamthiliya kwa mwega wa Kiaristotle umekuwa na athari kubwa sana kwa waandishi wa Kiafrika. Katika fasihi ya Kiswahili, baadhi ya waandishi wa mwanzo walioathiriwa na mkabala huo ni Ebrahim Hussein na Penina Mlama (Wafula na wenzake, 2020). Makala haya yanachambua mbinu za Kiaristotle na zisizo za Kiaristotle katika tamthiliya ya Sadaka ya John Okello (Mbogo, 2015). Mbinu ya usomaji makini ndiyo imetumiwa kukusanya data. Data zimewasilishwa kwa Mkabala wa Kimaelezo. Ukusanyaji, uchambuzi na mjadala katika makala haya umeongozwa na Nadharia ya Kiaristotle. Kimsingi, Emmanuel Mbogo, mtunzi teule ametumia mbinu za Kiaristotle na zisizo za Kiaristotle katika tamthiliya ya Sadaka ya John Okello (2015). Mbinu za Kiaristotle zimejidhihirisha kupitia vipengele vya msuko, wahusika, lugha za kishairi, uteuzi wa misamiati, na dhamira. Mbinu zisizo za Kiaristotle zimejidhihirisha kupitia mbinu za monolojia, kuchanganya nathari na ushairi, pamoja na dayalojia. Makala haya yanaeleza kuwa tamthiliya ya Sadaka ya John Okello ni drama tanzia. Drama hii imebeba sifa nyingi za Kiaristotle na sifa chache zisizo za Kiaristotle. Mhusika mkuu John Okello amepitia mambo mazito na magumu ambayo mtu yeyote akikutana na kazi hii lazima ahisi huzuni moyoni mwake na amwonee mhusika huyu huruma kwa mateso na malipo mabaya aliyoyapata. Kutokana na mikondo mbalimbali ambayo drama tanzia inapitia si lazima tena shujaa au mhusika mkuu atoke familia ya tabaka la juu au tabaka tawala. Mhusika mkuu sasa anaweza kutoka tabaka lolote katika jamii yoyote.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"279 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-08-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"132512952","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe","authors":"Odhong’ Joseph Ondiek, D. Amukowa, B. Ambuyo","doi":"10.37284/jammk.6.1.1345","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1345","url":null,"abstract":"Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi. Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi. Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao. Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha. Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe. Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018). Riwaya tano za Habwe: Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu. Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii. Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa. Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu. Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa. Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti. Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"26 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-07-31","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128815803","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Milkah Wanjugu, J. N. Maitaria, Peter Kinyanjui Mwangi
{"title":"Matumizi ya Kinaya Kubainishia Maudhui katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Chozi la Heri na Tamthilia ya Kigogo","authors":"Milkah Wanjugu, J. N. Maitaria, Peter Kinyanjui Mwangi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1303","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1303","url":null,"abstract":"Mtunzi wa kazi ya kazi ya fasihi hususan riwaya na tamthilia, hutumia mbinu mahususi kuwasilishia matukio na mawazo yanavyoshuhudiwa katika jamii. Mbinu hizo huteuliwa na mtunzi kwa makusudi ili ujumbe unaokusudiwa kuwasilishwa na kueleweka kwa mwafaka na hadhira. Mbinu hizo ni zile zinazojibainisha katika kitengo cha tamathali za usemi. Katika utafiti huu, mbinu inayozingatiwa ni kinaya ambacho huwasilisha ujumbe kinyume na matarajio. Utafiti huu unatuonyesha matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri (2017) ambayo imeandikwa na Matei na tamthilia ya Kigogo (2015) ambayo imeandikwa na Kea. Wanakejeli uhuru katika mataifa yaliyopata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 barani Afrika. Mataifa haya ni yale ambayo baada ya kupigania uhuru na kuunyakua kutoka kwa wakoloni, bado raia wanahisi kuwa wanaendelea kuwa katika hali ya kudhulumiwa na hali ya maisha kuwa magumu kutokana na uongozi usioafiki maono ya matarajio yao. Utafiti huu utabainisha jinsi watunzi wa riwaya na tamthilia teule yaani Assumpta Matei na Pauline Kea mtawalia walivyowasilisha kazi zao kwa kuzingatia mbinu ya kinaya katika kubainishia na kuukejeli uongozi katika bara la Afrika. Malengo ya utafiti huu yatakuwa, kufafanua matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo, kujadili jinsi waandishi wa riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo wametumia kinaya katika kuendeleza maudhui na kueleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika usawiri wa wahusika viongozi katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhakiki wa mtindo na uchanganuzi wa data utaongozwa na mihimili ya nadharia hii kisha matokeo yatawasilishwa kwa njia ya maelezo.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"75 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-07-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"121641803","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Maumbo na Maana za Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo","authors":"Jemima Lenjima, Julius Edmund Frank","doi":"10.37284/jammk.6.1.1271","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1271","url":null,"abstract":"Makala haya yamechunguza maumbo na maana za majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo kwa kuchanganua vijenzi mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya ya Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma kwa ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za makala haya zimewasilishwa kwa majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo yamedhihirisha kuwa majina ya asili ya watu yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia na kuleta maana. Tofauti na baadhi ya wanaisimu wanaodai kuwa majina ya watu yameundwa na mzizi au mashina tu, makala haya yamedhihirisha kuwa vipo vipashio maalumu vinayounda majina ya asili ya watu na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"13 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-06-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"122486551","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Usawiri wa Mabadiliko ya Ujumi Mweusi katika Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1990-2000","authors":"Elihaki Yonazi, Julius Edmund Frank","doi":"10.37284/jammk.6.1.1255","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1255","url":null,"abstract":"Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Afrika huitwa ujumi mweusi. Ujumi wa jamii huweza kupaka mabadiliko kulingana na mpito wa wakati na mwingiliano wa jamii nyingine. Mabadiliko ya ujumi wa kijamii husawiriwa kwenye kazi za kifasihi za jamii hiyo. Makala haya yamechunguza usawiri wa mabadiliko ya ujumi mweusi kwenye nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Data ya maktabani ndiyo iliyotumika. Jumla ya nyimbo 20 za kuanzia mwaka 1990-2000 zilikusanywa, ambapo zimetumika nyimbo 5 tu, zilizoteuliwa kimakusudi, kwa kuangalia dhima kuu, na ya kipekee inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Nyimbo hizo ndizo zilizotumika katika mjadala wa makala haya. Nadharia ya Unegritudi na Uhalisia zimetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti. Nadharia ya Unegritudi ilituongoza katika kuchambua vipengele vya ujumi mweusi vinavyojitokeza kwenye nyimbo teule. Naharia ya Uhalisia ilituongoza katika kujadili uhalisia wa jamii ya Watanzania na nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Aidha, katika kubainisha mabadiliko ya ujumi mweusi, na jinsi mabadilko hayo yanavyosawiriwa kwenye nyimbo teule. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwepo kwa mabadiliko mengi ya ujumi mweusi yaliyosawiriwa na nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania kwa mawanda mapana. Mabadiliko hayo ni kama vile, kukosekana/kupungua kwa; maadili mema, umoja na ushirika, utu; heshima, na adabu na utii. Kutokana hayo, watunzi wa nyimbo hizi wanashauriwa kutunga nyimbo zinazosawiri ujumi mweusi, na kuepuka athari hasi za utamaduni wa nje, ili nyimbo hizo ziweze kukubalika na jamii yote, na kuwa na manufaa endelevu katika jamii yao.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"26 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-06-16","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123744594","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mikakati ya Ushawishi katika Jumbe za Kihalifu kwenye Facebook na Baruapepe","authors":"James Mwangi, Nabea Wendo, Sheila Wandera","doi":"10.37284/jammk.6.1.1252","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1252","url":null,"abstract":"Mawasiliano yameimarika sana katika karne ya ishirini na moja kufuatia uvumbuzi wa teknolojia ya mawasiliano. Namna uvumbuzi unavyoendelea kuwepo ndivyo visa vya uhalifu wa mitandaoni vinavyozidi kuongezeka. Wahalifu hutumia baruapepe, Instagram, Twitter, WhatsApp, Facebook na njia nyinginezo za mitandaoni kuwadanganya watu, kuwaibia watu hela, kusambaza jumbe chafu za kiponografia, kuingilia data za wenyewe bila ruhusa na kusambaza jumbe za vitisho kwa watumiaji wa mitandao hii. Wahalifu hutumia ushawishi kutuma jumbe kama vile za ushindi wa pesa, ugawaji urithi, masuala ya kibiashara, jumbe za uhusiano wa kimapenzi na udukuzi wa pesa katika benki huku lengo kuu likiwa kuwaibia watu hela. Utafiti huu ulilenga kuchanganua mikakati ya ushawishi inayotumiwa na wahalifu hawa wa mitandaoni ili kufaulisha uovu wao. Nadharia ya Ubalagha ya Ushawishi iliyoasisiwa na Aristotle kisha kuendelezwa na wasomi wengine ilitumiwa pamoja na nadharia ya Mawasiliano ya Kiupatanishi ya Kitarakilishi iliyoasisiwa na Herring (2001). Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimakusudi. Data ya utafiti ilikusanywa katika mitandao ya kijamii kwa njia ya upakuaji halafu kuhifadhiwa katika maandishi kisha ufafanuzi wake ulifanywa kwa njia ya maelezo. Mbinu ya uhakiki matini ilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulibainisha kuwa wahalifu wa mitandao ya kijamii hutumia mikakati ya imani na dini, hisia, utoaji wa hoja zenye mantiki ili kuwashawishi watumiaji wa mitandao. Utafiti huu ni wa manufaa kwa watafiti wa lugha hasa katika nyanja ya Isimu kwa kuwapa ari ya kuchambua diskosi na kauli tofauti tofauti kama zinavyotumiwa katika mitandao ya kijamii.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"40 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-06-15","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"129102030","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Majele Noah Munda, Eric W. Wamalwa, Simiyu Benson Sululu
{"title":"Mchango wa Mofofonolojia ya Kiduruma kwa Ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili","authors":"Majele Noah Munda, Eric W. Wamalwa, Simiyu Benson Sululu","doi":"10.37284/jammk.6.1.1227","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1227","url":null,"abstract":"Makala haya yamedadavua mchango wa mofofonolojia ya Kiduruma kwa ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Kwale nchini Kenya. Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na Joan Hooper (1971) iliongoza utafiti. Mkabala wa kithamano na muundo wa kiethinografia ulitumiwa katika uchunguzi. Data ilikusanywa kutokana na insha za wanafunzi kwa kutumia mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionesha kuwa kuna mwingiliano katika vipengele vya mofofonolojia ya Kiduruma na Kiswahili, hali inayoleta uwezekano wa kuendeleza ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kwa kutumia mofofonolojia ya Kiduruma. Imebainika kwamba ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kama vile fonimu, miundo ya silabi, ngeli, nyakati mbalimbali na mnyambuliko wa maneno unaweza kufaidi kutokana na mofofonolojia ya Kiduruma. Kutokana na matokeo hayo, uchunguzi huu unapendekeza kwamba, katika eneo la utafiti ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ni Waduruma, mofofonolojia ya Kiduruma inaweza kutumiwa kama wenzo wa ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"5 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-05-24","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"122374671","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}