East African Journal of Swahili Studies最新文献

筛选
英文 中文
Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-10-30 DOI: 10.37284/jammk.4.1.452
Mofart Onyoni Ayiega, Leonard Chacha Mwita
{"title":"Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano","authors":"Mofart Onyoni Ayiega, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.4.1.452","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.452","url":null,"abstract":"Makala hii inachanganua nomino ambatani za Kiswahili zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Kanuni hii huonesha utaratibu wa kujenga neno kamili kwa kutumia vijenzi. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa muundo wa maneno yaliyotokana na ngazi za awali. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Nomino ambatani ifuatayo inadhihirisha mabadiliko yanayotokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa; [mw [enyekiti]] → [we [enyeviti]]. Katika utafiti huu tulikusanya data kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano zilitumika kama data ya msingi. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia sifa bainifu za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Utafiti huu uliongozwa na mhimili mmoja wa nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky (1982) na kuendelezwa na Katamba na Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano. Nadharia ya Mofolojia Leksia iliibuka kufidia mtazamo wa Chomsky wa Sarufi Zalishi ambao haukutambua kiwango cha mofolojia kama kiwango mahususi cha lugha. Kimsingi nadharia hii inaonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo hayo yanavyotamkwa. Data iliyohusiana na mada ya utafiti ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala ambazo zilitumika katika utafiti huu ni tasnifu za awali, makala ya mtandaoni na majarida. Utafiti huu uliongozwa na usampulishaji kimakusudi ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyo na sifa bainifu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya michoro, majedwali na maelezo. Utafiti huu unachangia isimu hasa kupitia kuelewa na kueleza mbinu za mwambatano katika lugha ya Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, na kukuza mofolojia ya Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-10-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"124517051","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Ishara Bwege Katika Diwani ya Kichomi
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-10-26 DOI: 10.37284/jammk.4.1.446
Chibayi Jason Poyi
{"title":"Ishara Bwege Katika Diwani ya Kichomi","authors":"Chibayi Jason Poyi","doi":"10.37284/jammk.4.1.446","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.446","url":null,"abstract":"Wasomi na watafiti wanadai kwamba ishara ni sehemu muhimu ya mtindo. Wanakubaliana kwamba ishara ni kigezo muhimu katika kufasiri maisha bwege. Ishara huonyesha hali halisi ya maisha bwege ya binadamu. Kwa hivyo, makala haya yananuia kuhakiki ishara zilizotumika kuashiria ubwege wa maisha katika diwani ya Kichomi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Leech ambayo itasaidia katika kuhakiki ishara zilizotumika kuibua ubwege wa maisha katika mashairi teule ya diwani ya Kichomi.  Ishara zilifafanuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo yaliyoegemezwa kwenye mihimili teule ya nadharia ya Mtindo. Uchanganuzi wa ishara uliongozwa na mbinu ya uhakiki matini. Katika diwani ya Kichomi, Kezilahabi anaangazia ubwege kwa njia ya kifalsafa na usanii wa hali ya juu kwa kutumia ishara maalumu. Mtafiti alihakiki matumizi ya ishara kwa namna ambavyo yalitumika kuangazia ubwege. Makala haya yatawafaa waandishi wa fasihi hasa ushairi kwani yatawawezesha kuelewa mbinu mbalimbali za kuandika matini zenye mvuto wa kisanaa ili kuwasilishia jamii ujumbe kwa ubunifu mkubwa.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-10-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130181330","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Utumikizi wa Mwingilianotanzu katika Fasihi ya Watoto
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-10-15 DOI: 10.37284/jammk.4.1.439
Caroline Nyambura Muriithi, Boniface Ngugi
{"title":"Utumikizi wa Mwingilianotanzu katika Fasihi ya Watoto","authors":"Caroline Nyambura Muriithi, Boniface Ngugi","doi":"10.37284/jammk.4.1.439","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.439","url":null,"abstract":"Tanzu zimeendelea kujidhihirisha katika umbo la riwaya na kuifanya mseto wa mambo mbalimbali. Kutegemeana na kuathiriana kwa tanzu kunaitwa mwingilianotanzu. Fasihi ya watoto imeendelea kukua na kudhihirisha matumizi ya tanzu mbalimbali katika umbo lake na hivyo kuwa changamano. Uchangamano huu unatatiza upokeaji na uelewekaji wa dhima yake, hasa ikizingatiwa kuwa riwaya hizo zinatumika katika mtaala wa elimu nchini. Makala haya yananuia kufafanua ni vipi mwingilianotanzu unavyojisawiri katika vitabu vya fasihi ya watoto. Mifano itatokana na baadhi ya vitabu teule vya fasihi ya watoto ni Habari za Mawio (Masoud Nassor) na Maskini Bibi Yangu! (Said A Mohamed). Mwishowe itapendekeza namna mwingilianotanzu unavyoweza kutumiwa kwa ufaafu zaidi katika uelekezaji wa usomaji na kuuwasilisha ujumbe katika fasihi ya watoto.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"171 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-10-15","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123363431","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Taswira ya Mwanamke katika Kipindi cha Bi. Msafwari Runinga ya Citizen Nchini Kenya.
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-10-05 DOI: 10.37284/jammk.3.1.430
Janet Jepkurui Kibet, Rebecca Wanjiru Omollo, Rose Mavisi
{"title":"Taswira ya Mwanamke katika Kipindi cha Bi. Msafwari Runinga ya Citizen Nchini Kenya.","authors":"Janet Jepkurui Kibet, Rebecca Wanjiru Omollo, Rose Mavisi","doi":"10.37284/jammk.3.1.430","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.430","url":null,"abstract":"Utafiti huu unalenga kuchunguza na kutathmini taswira ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen nchini Kenya kwa mtazamo wa kifasihi. Utafiti huu uliongozwa na lengo lifuatalo: Kueleza nafasi ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen nchini Kenya. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi mathalani Ufeministi wa Kiafrika na nadharia ya mtindo. Nadharia ya Ufeministi ilifaa utafiti huu kwa kuwa inashughulika na masuala ya kijinsia hasa jinsia ya kike. Muundo wa kimfano ulitumika katika uchanganuzi wa utafiti huu. Utafiti huu ulijikita katika maktabani ili kupata maandishi yanayohusiana na mada iliyoshughulikiwa. Kutokana na maelezo haya, kundi lengwa la utafiti ni kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen. Sampuli iliyotumika ni sampuli ya kimaksudi ambayo kipindi cha Bi. Msafwari kiliteuliwa.  Utafiti huu ulitumia mbinu ya kutazama, kusikiliza na kurekodi vipindi katika kukusanya data yake. Matokeo ya utafiti yalijitokeza wazi kuwa, nafasi ya mwanamke ni: kumfurahisha mume wake, kumsaidia mume wake, kutii, kumheshimu na kunyenyekea mbele ya mume. Pia ana nafasi ya kudumisha amani katika ndoa. Ukusanyaji na uchanganuzi wa data, uwasilishaji wa matokeo ulifanywa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliofanywa utawafaa watafiti wengine watakaojishughulisha na mada inayohusu mwanamke kwani wataweza kurejelea kazi hii ili kupata habari kuhusu nafasi ya mwanamke. Kwa ujumla, utafiti uliyofanywa ulichunguza taswira ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-10-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"129195013","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-09-16 DOI: 10.37284/jammk.3.1.413
Grace Adhiambo Onyango, O. Ntiba, Rocha M. Chimerah
{"title":"Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.","authors":"Grace Adhiambo Onyango, O. Ntiba, Rocha M. Chimerah","doi":"10.37284/jammk.3.1.413","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.413","url":null,"abstract":"Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia. Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe. Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed. Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka. Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini. Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni. Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu. Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika. Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya. Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili. Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa. Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"66 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-09-16","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130706839","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Jinsi Watoto Wanavyokabiliana na changamoto kwenye vitabu vya fasihi
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-09-08 DOI: 10.37284/jammk.3.1.405
Viola Jepkemboi Kiplagat, Rebecca Wanjiku Omolo, Margan Adero
{"title":"Jinsi Watoto Wanavyokabiliana na changamoto kwenye vitabu vya fasihi","authors":"Viola Jepkemboi Kiplagat, Rebecca Wanjiku Omolo, Margan Adero","doi":"10.37284/jammk.3.1.405","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.405","url":null,"abstract":"Watoto wengi wanapitia changamoto nyingi miongoni mwa walezi wao na wanajamii. Kutokana na yale wanayoyapitia pamoja na mazingira duni wanamoishi, watoto wengi hukosa mwelekeo dhabiti wa kimaadili hivyo basi kukosa mahitaji yao ya kuwawezesha kuwa na hulka zinazokubalika katika jamii. Mtafiti alinuia kuchanganua vitabu vya fasihi ya watoto ili kubainisha iwapo vitabu hivi vinaweza kutekeleza mahitaji ya watoto kupitia migogoro au changamoto vitabuni. Vitabu teule vilivyotumiwa katika utafiti vilikuwa Ahaa! Roda (2017) kilichoandikwa na Tom Nyambeka na Mwisho wa Ujambazi (2017) naye Yahya Mutuku. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Maadili na nadharia ya Uhalisia. Njia za utafiti zilizotumiwa ni hojaji na upekuzi wa yaliyomo kwenye vitabu teule vya fasihi ya watoto. Data iliyokusanywa ilipangwa kulingana na maswali ya utafiti na kuchanganuliwa kwa kuzingatia mkabala mseto ambapo, muundo wa QUAL-QUAN ulitumika. Mtafiti alichanganua vitabu teule vya fasihi kimaelezo akiongozwa na maswali ya utafiti. Mtafiti alikusanya data nyanjani kupitia hojaji zilizosambazwa kwa sampuli ya asilimia kumi ya watoto mia mbili kutoka darasa la saba, shule ya msingi ya Langas, Kaunti ya Uasin Gishu. Shule hii ya Langas ni shule iliyoko katika mazingira duni hivyo basi watoto wengi wanapitia changamoto nyingi za kijamii. Matokeo yalibainisha kuwa vitabu vya fasihi vinaweza kutekeleza  mahitaji ya watoto kupitia migogoro vitabuni na kwamba vitabu vya fasihi ya watoto vinaweza kutoa mwelekeo kwa watoto kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto katika hali halisi. Watoto 50% waliotafitiwa walikubali kuwa vitabu walivyovisoma vilikuwa changamoto ambazo waliweza kufananisha na hali halisi. Changamoto kwenye vitabu teule zilioana na changamoto halisi za watoto. Utafiti huu ulitoa mapendekezo kwa taasisi ya KICD na wizara ya elimu watumie utafiti huu kufanya tafiti zaidi ili kuchangia zaidi mitaala kwa lengo la kutekeleza mahitaji ya watoto. Walezi, walimu, wakuu wa shule watumie utafiti huu kuwalea watoto wao kwa njia mbadala na wenye manufaa. Utafiti zaidi uweze kufanywa kuhusu fasihi ya watoto kutekeleza mahitaji ya watoto kupitia changamoto zinazotokana na migogoro vitabuni. Waandishi wa vitabu pia watumie utafiti huu kuandika vitabu vilivyo na maudhui tofauti tofauti yanayoguza changamoto za watoto na hali halisi ya watoto","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"101 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-09-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"125962115","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-09-08 DOI: 10.37284/jammk.3.1.404
A. Odhiambo, Kineene Wa Mutiso, K. W. Wamitila
{"title":"Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi","authors":"A. Odhiambo, Kineene Wa Mutiso, K. W. Wamitila","doi":"10.37284/jammk.3.1.404","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.404","url":null,"abstract":"Katika makala haya, tumechunguza aina na mchango wa urudiaji wa kisarufi katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, tumeongozwa na nadharia ya Umtindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Hii ni kwa sababu uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hauwezi kujisimamia. Nadharia ya Umtindo inahusishwa na Geoffrey Leech katika mwaka wa 1969 kutokana na kazi yake ya kwanza ya ushairi alioandika huku akizingatia mawazo ya nadharia hii. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za urudiaji wa kisarufi zilizotumiwa katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Baada ya uhakiki wetu, tumegundua kuwa urudiaji wa kisarufi unachangia maudhui, wahusika, vipengele vya kimtindo na vipengele vingine vya fani kwa ujumla katika utungo huu. Isitoshe, urudiaji huu wa kisarufi umekuwa na umuhimu katika kuleta mwangwi na usisitizaji. Tumetumia maelezo na ufafanuzi kutoka katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi kama njia ya kubainisha haya.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"7 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-09-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"134047089","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-08-02 DOI: 10.37284/jammk.3.1.373
Simiyu Benson Sululu, R. M. Wafula, J. N. Maitaria
{"title":"Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana","authors":"Simiyu Benson Sululu, R. M. Wafula, J. N. Maitaria","doi":"10.37284/jammk.3.1.373","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.373","url":null,"abstract":"Usomaji wa fasihi katika kipindi cha sasa unabainisha idadi kubwa ya waandishi kutoka jamii zisizo Waswahili ambao wameandika kazi katika tanzu mahsusi za fasihi simulizi ya Kiswahili. Waandishi hawa wameendelea kutumia maudhui, ploti na vipengele vingine vya utamaduni wa fasihi simulizi za jamii zao katika kubuni kazi zao za fasihi andishi ya Kiswahili. Vipengele vya fasihi simulizi za jamii za waandishi hawa, wasiokuwa Waswahili, vimeingizwa katika riwaya ya Kiswahili na kuwa sehemu ya riwaya hii. Makala hii imechunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unaifanya riwaya hii kuwa ya kimahuluti. Mahsusi, makala hii imedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano wa riwaya ya Kufa Kuzikana (2003) iliyoandikwa na Ken Walibora. Tathmini hii imetumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi mbalimbali ambao ni bora na imara zaidi kuliko tamaduni asilia. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii za watunzi wake teule wasiokuwa Waswahili. Katika kufanya hivyo, makala hii imebainisha jinsi kuingizwa kwa vipengele hivi vya fasihi simulizi za jamii za waandishi teule katika riwaya ya Kiswahili kumeirutubisha riwaya hii kwa kuifanya kuwa changamano na nyumbufu kwa ambavyo inameza tanzu kutoka tamaduni tofauti na kujiimarisha kupitia kwazo bila kupoteza sura yake asilia.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"14 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-08-02","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"127751260","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-07-27 DOI: 10.37284/jammk.3.1.367
F. Miima, Vincent Ferrel Kawoya
{"title":"Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda","authors":"F. Miima, Vincent Ferrel Kawoya","doi":"10.37284/jammk.3.1.367","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.367","url":null,"abstract":"Kiswahili ni lugha ya kimataifa na ni mojawapo ya lugha rasmi za Muungano wa Nchi za Afrika. Vilevile, katika nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili kina hadhi ya aina ya kipekee kikilinganishwa na lugha zingine zenye asili ya Kiafrika. Nchini Kenya na Tanzania ni lugha ya taifa na rasmi. Kwa upande mwingine, nchini Uganda, Kiswahili kinatambulika kikatiba kama lugha ya pili rasmi. Hali kadhalika katika kanda ya maziwa makuu kinategemewa sana kama chombo muhimu cha kufanikisha harakati za kibiashara. Kutokana na ukweli huu kuhusu hadhi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili, ingetarajiwa kuwa Kiswahili kingetumiwa kwa mawasiliano rasmi na katika ngazi mbalimbali za kimataifa. Hata hivyo, ni wazi kwamba kinakabiliwa na changamoto chungu nzima hasa zaidi nchini Uganda kiasi kwamba hatima yake haijulikani. Makala hii itaangazia hali ya lugha ya Kiswahili, changamoto zinazoikabili na hatima yake nchini Uganda. Itatoa mapendekezo kuhusu mikakati inayoweza kutumiwa ili kutamanisha wananchi wa Uganda kukienzi Kiswahili, kuinua hadhi yake na kukistawisha ipasavyo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-07-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"114145174","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2021-07-27 DOI: 10.37284/jammk.3.1.368
M. Karama
{"title":"Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya","authors":"M. Karama","doi":"10.37284/jammk.3.1.368","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.368","url":null,"abstract":"Miji yot̪ʰe ulimwenguni imepawa majina ili kuitambulisha. Majina haya ni hazina ya mapisi na ut̪amad̪uni kuwahusu wakaaji wa miji hiyo. Namna inavoitwa, fasiri na fasili za majina hayo husema mengi kuhusu maana na nyusuli zake. Makala haya yamechunguza toponimi ya baadhi ya mitʰaa ya mji wa Mambasa, Kenya. Madhumuni yalikuwa ni kuchanganuwa nyusuli za majina kwa kubainisha t̪afaut̪i za kimat̪amshi ya majina hayo, kuthibit̪isha kuwa t̪afaut̪i hizi zaleta t̪afaut̪i ya maana ya majina, na kwamba toponimi za mitʰaa hiyo imeelemeya kwelezeya maumbile ya mazingira ya mahali hapo jambo linaloshuhud̪iwa katika jamii nyengine za Kibantu, Kenya. Tulitumiya T̪arat̪ibu za Ulinganisho na Toponimi Kina ili kuchanganuliya data yetu. Data yetu tuliipata kwa kuwauliza wazee wa miyaka 50 na zaidi ambao wana maelezo simulizi kuhusu fasili za majina hayo na data ya upili. Kwa kulinganisha na lugha za jamii zinazokaribiyana za Kimvit̪a, Kimijikenra, Kipokomo na lugha za Kibantu kut̪oka bara Kenya tuliweza kung’amuwa kuwa majina haya ya Mambasa yanashabihiyana na yale ya lugha nyengine hivo kutupa ufunuwo mpya kuhusu maana za majina hayo. Tumepata kuwa ut̪amkaji wa majina unaleta t̪afaut̪i ya maana na hivo usuli wao piya ni t̪afaut̪i na ilivozoweleka. Tumepata kuwa majina ya kale yaliitwa kutegemeya maumbile ya mazingira na majina ya mitʰaa ya kisasa yameelemeya zaidi vitu au majengo yaliyoko hapo. Kupitiya makala haya tunaamini tumet̪owa fasili mpya kuhusu mitʰaa hii na hivo kuwapa fikira nyengine wataalamu wa Chimbo, Ut̪alii na Isimu kuhusu majina haya na historiya inayobebwa na majina haya.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"60 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-07-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123134461","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
相关产品
×
本文献相关产品
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信