{"title":"Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano","authors":"Mofart Onyoni Ayiega, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.4.1.452","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala hii inachanganua nomino ambatani za Kiswahili zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Kanuni hii huonesha utaratibu wa kujenga neno kamili kwa kutumia vijenzi. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa muundo wa maneno yaliyotokana na ngazi za awali. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Nomino ambatani ifuatayo inadhihirisha mabadiliko yanayotokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa; [mw [enyekiti]] → [we [enyeviti]]. Katika utafiti huu tulikusanya data kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano zilitumika kama data ya msingi. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia sifa bainifu za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Utafiti huu uliongozwa na mhimili mmoja wa nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky (1982) na kuendelezwa na Katamba na Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano. Nadharia ya Mofolojia Leksia iliibuka kufidia mtazamo wa Chomsky wa Sarufi Zalishi ambao haukutambua kiwango cha mofolojia kama kiwango mahususi cha lugha. Kimsingi nadharia hii inaonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo hayo yanavyotamkwa. Data iliyohusiana na mada ya utafiti ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala ambazo zilitumika katika utafiti huu ni tasnifu za awali, makala ya mtandaoni na majarida. Utafiti huu uliongozwa na usampulishaji kimakusudi ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyo na sifa bainifu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya michoro, majedwali na maelezo. Utafiti huu unachangia isimu hasa kupitia kuelewa na kueleza mbinu za mwambatano katika lugha ya Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, na kukuza mofolojia ya Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2021-10-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.452","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala hii inachanganua nomino ambatani za Kiswahili zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Kanuni hii huonesha utaratibu wa kujenga neno kamili kwa kutumia vijenzi. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa muundo wa maneno yaliyotokana na ngazi za awali. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Nomino ambatani ifuatayo inadhihirisha mabadiliko yanayotokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa; [mw [enyekiti]] → [we [enyeviti]]. Katika utafiti huu tulikusanya data kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano zilitumika kama data ya msingi. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia sifa bainifu za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Utafiti huu uliongozwa na mhimili mmoja wa nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky (1982) na kuendelezwa na Katamba na Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano. Nadharia ya Mofolojia Leksia iliibuka kufidia mtazamo wa Chomsky wa Sarufi Zalishi ambao haukutambua kiwango cha mofolojia kama kiwango mahususi cha lugha. Kimsingi nadharia hii inaonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo hayo yanavyotamkwa. Data iliyohusiana na mada ya utafiti ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala ambazo zilitumika katika utafiti huu ni tasnifu za awali, makala ya mtandaoni na majarida. Utafiti huu uliongozwa na usampulishaji kimakusudi ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyo na sifa bainifu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya michoro, majedwali na maelezo. Utafiti huu unachangia isimu hasa kupitia kuelewa na kueleza mbinu za mwambatano katika lugha ya Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, na kukuza mofolojia ya Kiswahili.