Gideon K Ipyegon Rono, C. Kitetu, Abdulrahim Hussein Taib Ali
{"title":"Muundo wa Mazungumzo ya Uuzaji na Ununuzi wa Nguo za Mitumba katika Soko Mjinga Kaptembwo","authors":"Gideon K Ipyegon Rono, C. Kitetu, Abdulrahim Hussein Taib Ali","doi":"10.37284/jammk.5.1.664","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.664","url":null,"abstract":"Mazungumzo ndio njia mojawapo ya kuchochea maingiliano baina ya watu. Lugha ya mazungumzo hutokea katika miktadha mbalimbali kama vile shuleni, hospitalini na hata nyumbani. Utafiti huu uliangazia mpangilio na nafasi ya muundo wa mazungumzo. Wanaojihusisha na mazungumzo haya ni muuzaji na mnunuzi. Lengo la makala haya ni kubainisha namna matumizi ya lugha ya kuafikiana bei wakati wa kuuza na kununua huathiri muundo wa mazungumzo. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni Uchanganuzi wa Mazungumzo iliyoasisiwa na Sacks (1960). Kuonyesha kuwa, mazungumzo yanayotekelezwa na binadamu huwa na mpangilio maalum. Utafiti huu ulichunguza muundo wa mazungumzo katika soko la mtumba. Matokeo yake yalibainisha kuwa muundo wa mazungumzo haukuweza kufuatwa kwa wakati mwingi kikamilifu, kupashana zamu katika mazungumzo kulipewa kipau mbele, nguo za wanawake na watoto zilinunuliwa sana zikilinganishwa na za kiume na tabia za wanunuzi kutoka katika jamii na kabila tofauti kimazungumzo zilijikita katika utamaduni aliolelewa nayo.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"249 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-16","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"116164701","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma","authors":"Martin Barasa Mulwale, F. Indede, B. Ambuyo","doi":"10.37284/jammk.5.1.665","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.665","url":null,"abstract":"Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi yoyote ile. Nchini Kenya, vipengele katika katiba ya 2010, vinavyohusu lugha vilipandisha hadhi lugha ya Kiswahili ili iweze kutumika kama lugha ya taifa na rasmi sambamba na Kiingereza. Hata hivyo, katiba hii haijaweka kanuni zinazolenga kuimarisha na kudumisha uanuwai wa lugha za kiasili kote nchini Kenya. Machukulio ni kwamba, vipengele vya katiba vinasheheni sifa stahilifu kama vile, usawa wa kimatumizi, utekelezwaji, mikao ya kieneo, matakwa, pamoja na hiari za wananchi. Kwa kuangazia hali ya kiisimu-jamii katika Kaunti ya Bungoma, utata upo katika udumishaji wa mfumo ‘rasmi’ wa sera ya lugha Kitaifa, na utekelezwaji wa sera ya lugha kupitia asasi za serikali na zile za umma. Kazi hii inalenga kuchanganua uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu kupitia ruwaza zinazodhihirika katika mawanda mbalimbali ya lugha katika Kaunti ya Bungoma. Mihimili ya nadharia ya sera ya lugha iliyoendelezwa na Spolsky (2004, 2007) ambayo ni Usimamizi wa lugha na Ikolojia ya lugha pamoja na ruwaza za lugha ilivyoelezwa na Paltridge (2001) ndiyo nguzo ya kuchanganua utafiti huu. Aidha, mtazamo wa Haugen (1972) unaohusu Ikolojia ya lugha umetumika katika kudhihirisha michakato baina ya lugha na mazingira inamotumika. Muundo mseto uliojumuisha, muundo wa kimaelezo, kiupelelezi na wa kiiktisadi ulitumiwa. Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kuteua matumizi ya lugha ya KS, KB na KS/KB katika ruwaza za lugha zilizodhihirika katika mawanda ya biashara, kanisani na utawala hasa kwenye mikutano ya umma au baraza za Chifu katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Bungoma. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunzaji usio-shirikishi na ya kiiktisadi ilikusanywa kwa kuhesabu hali ambazo lugha za KS, KB au KS/KB zilitumiwa. Ilibainika kuwa lugha ya KS na KB hukamilishana kiuamilifu katika mawanda mbalimbali ya kijamii katika Kaunti ya Bungoma.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"388 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-16","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"133166895","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari za Tofauti za Mazingira ya Ujifunzaji wa Kiswahili kati ya Wanafunzi wenye Ulemavu wa Macho wa Shule Jumuishi ya Menengai na Joel Omino","authors":"Lilian Muguche Abunga, Peter Githinji","doi":"10.37284/jammk.5.1.661","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.661","url":null,"abstract":"Makala hii ililenga kulinganisha athari za tofauti za mazingira ya ujifunzaji wa Kiswahili kati ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho wa shule jumuishi ya Menengai na Joel Omino. Pembejeo wanayopata wanafunzi katika shule ya Menengai inayopatikana mjini Nakuru ambapo kuna wingi lugha ililinganishwa na ile ya wanafunzi wa shule ya Joel Omino inayopatikana katika vitongoji vya mji wa Kisumu ambako pembejeo kwa kiasi kikubwa inatokana na lugha moja kuu. Ulinganishaji wetu uliangazia stadi za lugha ambazo huathiriwa zaidi na tofauti za mazingira ya ujifunzaji katika juhudi za kuimarisha ujifunzaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho. Data ilikusanywa kwa kuhoji wanafunzi wote wenye ulemavu wa macho na baadhi ya walimu wa Kiswahili ilhali hojaji ilijazwa na wanafunzi wote wenye ulemavu wa macho na baadhi ya wanafunzi wasio na ulemavu wa macho. Data nyingine ilitokana na uchunzaji kupitia uhudhuriaji wa vipindi vya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na mihimili miwili ya nadharia ya Usomi Tendaji ya Bruner (1966). Mhimili wa kwanza unadai kuwa kujifunza lazima kuanze na masuala yanayopatikana katika mazingira ya wanafunzi wanayojaribu kikamilifu kuunda maana nao mhimili wa pili unadai kuwa, watu huweza kujifunza zaidi wakati wanajifunza na watu wengine kuliko wakati wanajifunza peke yao. Sampuli maksudi ilitumiwa katika kukusanya data nyanjani. Matokeo ya utafiti yalibaini tofauti tano za mazingira kati ya shule ya Menengai na Joel Omino. Tunapendekeza serikali iwaajiri walimu zaidi walio na mafunzo ya kuwashughulikia wanafunzi wenye ulemavu ili kuboresha ujifunzaji wa Kiswahili. Vilevile, shule zinahitaji kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuboresha upatikanaji wa vifaa vya ujifunzaji. Pia, serikali inapaswa kuhakikisha kuwa wazazi wanapewa mafunzo kuhusu umuhimu wa elimu ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho ili kuhakikisha kuwa wanaimarisha mazingira ya nyumbani yatakayowafaa wanafunzi wao katika somo la Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"21 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-11","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"127164980","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji","authors":"Abdu Salim Rais, Jacktone O. Onyango, I. Mbaabu","doi":"10.37284/jammk.5.1.641","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.641","url":null,"abstract":"Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004). Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana kwa wingi miongoni mwa Waafrika waliotawaliwa, na kinyume chake kikiwa sivyo (Buliba et al., 2014). Upeo wa utafiti huu ulikuwa Uchapishaji baina ya mwaka 2011 na 2018. Uchapishaji ni utoaji wa vitabu na kuvitawanya kwa kuviuzia watu (Bakita et al., 2012). Kihistoria, uchapishaji ulianzishwa nchini Uganda mnamo mwaka 1879 na Mmishonari Alexander Mackay wa ‘Church Missionary Society’ kwa madhumuni ya kufundisha Ukristo (Mbaabu, 1996). Kwa njia hiyo, uchapishaji wa kamusi na vitabu vya tafsiri za Biblia ulianzishwa kwa ajili ya kutaka kukidhi ufundishaji wake (Mbaabu, 2007). Ueneaji wa matumizi ya Kiswahili ulikadiriwa kutokana na ongezeko la Watumiaji wake nchini Uganda. Kwani ongezeko lilikomaa kiasi cha kuvuka mipaka ya awali (Myelimu, 2015). Taratibu za kithamano na kiwingi idadi zilitumika kwa kuzingatia mkabala wa pembe tatu kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data, iliyotokana na nyaraka za Wachapishaji pamoja na maoni ya Wahojiwa nyanjani. Data ilielezwa kwa kutumia asilimia za maratokezi za maoni ya Wahojiwa. Sampuli ya Wahojiwa wa hojaji ilitokana na Wadau wa Kiswahili wasiozidi 100 jijini Kampala. Sampuli ","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"31 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-04-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"114715112","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Utomilisi wa Lugha kama Chanzo cha Ubadilishanaji Msimbo Miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu katika Kaunti ya Kiambu","authors":"Beatrice Njambi Mwai, Leonard Chacha","doi":"10.37284/jammk.5.1.627","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.627","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza swala la kubadili msimbo miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu Kaunti ya Kiambu. Fikra kuu iliyoongoza utafiti huu ni kuwa wanafunzi hao hubadili msimbo kwa sababu ya utomilisi wa lugha. Hawana umilisiwa lugha mojaKwa mfanoutafiti huu umeangazia lugha za Kiingereza na Kiswahili. Tumedhihirisha kuwa hawa ni wanafunzi wa chuo kikuu lakini hawawezi kuwasiliana kwa lugha moja kwa ufasahalazima waingie katika lugha nyingine ili kufanikisha mawasiliano. Kwaanokama wanatumia lugha ya Kiswahili wanabadilisha na kuingia katika lugha ya Kiingereza kwa sababu wameshindwa kuendeleza mazungumzo katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umeongozwa na nadharia tambulishi iliyopendekezwa na Myers-Scotton (1983). Kulingana na Myers-Scottonkatika mawasiliano yoyote, kuna hali ya alama inayotambulika na isiyotambulika. Katika kuchagua alamamzungumzaji huchagua alama kulingana na mahitaji ya kijamii. Pia huonyesha kuwa kubadili msimbo ni kwa sababu ya ugumu wa watu kutumia lugha moja na ugumu huo uko akilini mwa mzungumzaji. Utafiti huu umeegemea maktabani na nyanjani. Maktabaniutafiti huu umenufaika kwa kupata data kutoka kwa machapisho, vitabu na majarida kuhusu dhana ya kubadili msimbo, uwili lugha na misingi ya nadharia. Nyanjaniutafiti huu umefanywa katika Kaunti ya Kiambu, Utafiti huu umehusisha matumizi ya vifaa kama vile mwongozo wa mahojiano na kuhudhuria vikao rasmi ambavyo vijana wanawasiliana. Data iliyochanganuliwa kwa mujibu wa nadharia tambulishi imewasilishwa kwa njia ya maelezo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"72 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-04-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123958462","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uchambuzi wa Hali ya Ukatili wa Wanyama Katika Mashamba Nchini Kenya","authors":"Maureen K. Luvanda","doi":"10.37284/jammk.5.1.626","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.626","url":null,"abstract":"Hati hii imetayarishwa kushughulikia maswala ya ustawi wa mifugo nchini Kenya na kuongezeka kwa ujuzi wa wafanyikazi wa mstari wa mbele kuhusiana na swala la viwango na sheria zinazoongoza ustawi wa wanyama. Lengo kuu lilikuwa kutathmini vipengele vya utunzaji wa wanyama, matibabu na ujuzi wa ustawi wa wanyama miongoni mwa wakulima nchini Kenya. Tuligundua ya kwamba wakulima wengi hawaelewi kimsingi ustawi wa wanyama kwa kuwa wengi wao hawajapata mafunzo maalum na wengi wao hawajui sheria zilizopo kuhusu mada hiyo. Wadau wengine walitathminiwa pia kwa madhumuni ya kulinganisha na madaktari wa mifugo na kama ilivyotarajiwa walikuwa na ujuzi zaidi kuhusu ustawi wa wanyama na desturi zinazoikuza. Hata hivyo, kadhaa walionelea kwamba serikali haikuweka juhudi za kutosha katika kukuza ufahamu wa umma au hata kuhamasisha jamii dhidi ya ukatili wa wanyama. Kulingana na maelezo yaliyopatikana, hati hii iliundwa ili kutoa suluhisho ya vitendo linapohusu swala la kuongeza ustawi wa wanyama nchini Kenya. Mapendekezo haya ni pamoja na kuishinikiza serikali kuanzisha sera madhubuti dhidi ya ukatili wa wanyama, kuwahimiza maafisa wa sheria kutekeleza sheria za sasa kwa kutumia mifumo ambayo tayari iko na kuhimiza mazungumzo ya jamii na ushiriki wa moja kwa moja wa watu walio mstari wa mbele.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"59 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-04-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"126157493","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Utekelezaji wa Mitalaa ya Kiswahili Vyuoni na Namna Unavyoathiri Utendakazi wa Walimu Wanaofundisha katika Shule za Upili","authors":"Jackline Mwanzi, Odeo Isaac Ipara, K. I. Simala","doi":"10.37284/jammk.5.1.556","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.556","url":null,"abstract":"Walimu wanaofundisha katika shule za upili hupata mafunzo yao ya kitaaluma kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali. Wanapoandaliwa vyuoni, walimu hawa hupewa mafunzo kwa kutumia mitalaa tofauti inayoandaliwa katika vyuo vikuu hivyo. Baada ya kuhitimu, wao hutarajiwa kuutekeleza mtalaa mmoja unaoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa nchini Kenya (TUMIKE) ili ufundishwe katika shule zote za upili. Utafiti ulifanywa ili kudhihirisha iwapo mafunzo ya kitaaluma yanayotolewa vyuoni kuwaandaa walimu wa somo la Kiswahili yanawapa maarifa na stadi wanazohitaji kufundisha katika shule za upili baada ya kuhitimu. Makala haya yametokana na utafiti uliofanywa ili Kutathmini uhusiano baina ya mitalaa ya Kiswahili inayotumika katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya na mtalaa ambao umeandaliwa na TUMIKE ili kutekelezwa katika shule za upili. Utafiti ulifanyika katika vyuo vikuu vitano vya umma nchini Kenya. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya elezi. Data ilikusanywa kwa njia ya usaili, uchanganuzi wa nyaraka na hojaji. Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kitakwimu na kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa uhusiano baina ya mitalaa rasmi ya Kiswahili ya vyuo vikuu vya umma na mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili siyo wa moja kwa moja. Hali hii iliathiri utendakazi wa walimu walipotekeleza mtalaa wa shule za upili. Uhusiano mdogo uliopo baina ya mitalaa rasmi ya vyuo vikuu na mtalaa rasmi wa TUMIKE ulidhihirika kwa kuchunguza vipengele vikuu vya mtalaa ambavyo ni: malengo, mada, utekelezaji na tathmini. Utafiti unapendekeza pafanyike marekebisho ya mara kwa mara ya mtalaa wa TUMIKE kwa kuwahusisha walimu na waandalizi wao ili wakadirie malengo, mada, mbinu za utekelezaji na tathmini mintarafu maandalizi yanayotolewa kwa walimu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-02-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128815873","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi","authors":"Cheruiyot Evans Kiplimo, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.5.1.527","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.527","url":null,"abstract":"Kiswahili ni lugha mojawapo ya Kiafrika inayochangia ujifunzaji wa fonolojia. Wanaisimu wamejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kiswahili bila kugusia swala la athari zake katika vipashio vikubwa kuliko fonimu. Hata hivyo, siyo mifanyiko yote ya kifonolojia ndio huathiri fonolojia arudhi ya lugha husika. Fonimu zinapoungana ili kuunda vipashio vikubwa vya lugha kama vile silabi na neno, zinaathiriana katika viwango mbalimbali. Athari zingine huwa ndogo kiasi kwamba hazionekani bayana ilhali athari zingine huwa kubwa kiasi cha kuonekana bayana. Mfanyiko wa kifonolojia unaohusishwa na utowekaji wa fonimu ni udondoshaji. Fonimu inapotoweka katika neno, vipashio vikubwa kuliko fonimu yenyewe hupokea athari katika mfumo wa lugha. Makala hii inaonyesha jinsi mabadiliko ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi huathiri fonolojia arudhi ya Kiswahili. Hili liliwezekana kwa kujenga umbo la awali la neno kisha kuonyesha jinsi kudondoshwa kwa fonimu kuliathiri fonolojia arudhi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi iliyoasisiwa na Chomsky na Halle (1968). Makala hii, imetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kwa kusoma, kudondoa na kunakili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"68 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-01-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"133632753","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Uchanganuzi wa Kimofosintaksia wa Viangami katika Lugha ya Kiswahili.","authors":"Naomi Ndumba Kimonye, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.5.1.519","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.519","url":null,"abstract":"Dhamira ya makala haya ni kuonyesha sheria zinazozingatiwa wakati wa kuambisha viangami katika lugha ya Kiswahili. Viangami ni mofimu zinazojisimamia kisintaksia lakini kifonolojia ni tegemezi. Uchunguzi huu umeongozwa na nadharia Boreshaji. Kwa mujibu wa Nadharia Boreshaji, lugha yoyote ile ulimwenguni ina maumbo ya ndani na maumbo ya nje (Prince na Smolensky,1993). Maumbo haya hutumika kuzalisha maumbo tokeo tofauti. Umbo la nje hutokea baada ya umbo la ndani kubadilishwa. Data iliyotumika katika utafiti huu ilipatikana maktabani. Vitabu mbalimbali vya kisarufi na isimu vilitumika. Usampulishaji wa kimakusudi ulitumika. Vitabu vilivyochapishwa kwa lugha ya Kiswahili viliteuliwa kimakusudi. Vitabu hivi ni pamoja na riwaya, tamthilia, mashairi na vitabu vya kiada. Data ilikusanywa kwa mbinu ya kusoma na kunukuu. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Baada ya utafiti, imebainika kuwa shughuli ya kuambisha vipashio vya kisarufi hufanywa kwa uangalifu mkubwa sana. Data iliyopatikana inaweka wazi uambishaji wa viangami katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu utawafaa walimu, wanafunzi na wataalamu wa isimu. Pia waandishi wa kazi za isimu na fasihi watafaidika.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"82 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-01-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"132393758","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Furaha J Masatu, Venancia F Hyera, Osmunda R Ndunguru
{"title":"Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba","authors":"Furaha J Masatu, Venancia F Hyera, Osmunda R Ndunguru","doi":"10.37284/jammk.4.1.512","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.512","url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"19 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2021-12-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"124725747","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}