Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba

Furaha J Masatu, Venancia F Hyera, Osmunda R Ndunguru
{"title":"Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba","authors":"Furaha J Masatu, Venancia F Hyera, Osmunda R Ndunguru","doi":"10.37284/jammk.4.1.512","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"19 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2021-12-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.512","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0

Abstract

Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.
求助全文
约1分钟内获得全文 求助全文
来源期刊
自引率
0.00%
发文量
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
copy
已复制链接
快去分享给好友吧!
我知道了
右上角分享
点击右上角分享
0
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信