{"title":"Uchambuzi wa Hali ya Ukatili wa Wanyama Katika Mashamba Nchini Kenya","authors":"Maureen K. Luvanda","doi":"10.37284/jammk.5.1.626","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Hati hii imetayarishwa kushughulikia maswala ya ustawi wa mifugo nchini Kenya na kuongezeka kwa ujuzi wa wafanyikazi wa mstari wa mbele kuhusiana na swala la viwango na sheria zinazoongoza ustawi wa wanyama. Lengo kuu lilikuwa kutathmini vipengele vya utunzaji wa wanyama, matibabu na ujuzi wa ustawi wa wanyama miongoni mwa wakulima nchini Kenya. Tuligundua ya kwamba wakulima wengi hawaelewi kimsingi ustawi wa wanyama kwa kuwa wengi wao hawajapata mafunzo maalum na wengi wao hawajui sheria zilizopo kuhusu mada hiyo. Wadau wengine walitathminiwa pia kwa madhumuni ya kulinganisha na madaktari wa mifugo na kama ilivyotarajiwa walikuwa na ujuzi zaidi kuhusu ustawi wa wanyama na desturi zinazoikuza. Hata hivyo, kadhaa walionelea kwamba serikali haikuweka juhudi za kutosha katika kukuza ufahamu wa umma au hata kuhamasisha jamii dhidi ya ukatili wa wanyama. Kulingana na maelezo yaliyopatikana, hati hii iliundwa ili kutoa suluhisho ya vitendo linapohusu swala la kuongeza ustawi wa wanyama nchini Kenya. Mapendekezo haya ni pamoja na kuishinikiza serikali kuanzisha sera madhubuti dhidi ya ukatili wa wanyama, kuwahimiza maafisa wa sheria kutekeleza sheria za sasa kwa kutumia mifumo ambayo tayari iko na kuhimiza mazungumzo ya jamii na ushiriki wa moja kwa moja wa watu walio mstari wa mbele.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"59 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-04-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.626","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Hati hii imetayarishwa kushughulikia maswala ya ustawi wa mifugo nchini Kenya na kuongezeka kwa ujuzi wa wafanyikazi wa mstari wa mbele kuhusiana na swala la viwango na sheria zinazoongoza ustawi wa wanyama. Lengo kuu lilikuwa kutathmini vipengele vya utunzaji wa wanyama, matibabu na ujuzi wa ustawi wa wanyama miongoni mwa wakulima nchini Kenya. Tuligundua ya kwamba wakulima wengi hawaelewi kimsingi ustawi wa wanyama kwa kuwa wengi wao hawajapata mafunzo maalum na wengi wao hawajui sheria zilizopo kuhusu mada hiyo. Wadau wengine walitathminiwa pia kwa madhumuni ya kulinganisha na madaktari wa mifugo na kama ilivyotarajiwa walikuwa na ujuzi zaidi kuhusu ustawi wa wanyama na desturi zinazoikuza. Hata hivyo, kadhaa walionelea kwamba serikali haikuweka juhudi za kutosha katika kukuza ufahamu wa umma au hata kuhamasisha jamii dhidi ya ukatili wa wanyama. Kulingana na maelezo yaliyopatikana, hati hii iliundwa ili kutoa suluhisho ya vitendo linapohusu swala la kuongeza ustawi wa wanyama nchini Kenya. Mapendekezo haya ni pamoja na kuishinikiza serikali kuanzisha sera madhubuti dhidi ya ukatili wa wanyama, kuwahimiza maafisa wa sheria kutekeleza sheria za sasa kwa kutumia mifumo ambayo tayari iko na kuhimiza mazungumzo ya jamii na ushiriki wa moja kwa moja wa watu walio mstari wa mbele.