East African Journal of Swahili Studies最新文献

筛选
英文 中文
Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-08-08 DOI: 10.37284/jammk.5.1.781
Daniel Kiprugut Ng’etich, R. M. Wafula, J. N. Maitaria
{"title":"Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili","authors":"Daniel Kiprugut Ng’etich, R. M. Wafula, J. N. Maitaria","doi":"10.37284/jammk.5.1.781","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.781","url":null,"abstract":"Makala hii inaangazia dhima ya maongezi katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ni mojawapo wa tanzu muhimu za fasihi ya Kiswahili ambayo inaendelea kukua kwa upande wa wahusika, dhamira, maudhui, mtindo na upeo. Utanzu wa riwaya ya Kiswahili ulianza mwanzo wa karne ya ishirini wakati James Juma Mbotela alipoandika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Ukuaji wake umeshika kasi zaidi katika mwongo wa mwisho wa karne ya ishirini na mwanzo wa karne ya ishirini na moja. Ni muhimu pia kutambua kuwa, utungaji wa riwaya umeendelea kukua sambamba na uhakiki wake. Katika karne ya ishirini na moja, riwaya ya Kiswahili imefikia utungaji wa kimajaribio (Mwamzandi, 2013:48-66 na Mohamed 2003:78-79). Katika riwaya za kimajaribio, watunzi hujumuisha nadharia, visasili pamoja na kuzungumzia masuala ya utandawazi na soko huru. Ni riwaya ambazo hukiuka miundo ya riwaya iliyozoeleka. Kwa upande wa maongezi, usemaji wa wahusika katika riwaya umekua kutoka sahili hadi changamano kutokana na masuala yanayojadiliwa katika riwaya mahususi. Ni maoni ya waandishi wa makala hii kuwa, usemaji wa wahusika unaweza kuathirika na vipindi vya kihistoria hivyo basi kuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya riwaya. Madhumuni ya makala hii ilikuwa ni kuainisha maongezi katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ambazo zilichanganuliwa kwa mujibu wa makala hii ni Kusadikika (1951), Mafuta (1984) na Kufa Kuzikana (2003). Riwaya hizo ziliteuliwa kuwakilisha vipindi mahususi vya ukuaji na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Usemi Hakiki. Kutokana na uchanganuzi huo, makala hii imebainisha mchango wa maongezi kwa ukuaji, maendeleo na uumbufu wa utanzu wa riwaya kwa ujumla.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"7 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"127817727","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-07-28 DOI: 10.37284/jammk.5.1.769
Peris Mwihaki Ndung’u, Raphael Mwaura Gacheiya, C. Kitetu
{"title":"Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ","authors":"Peris Mwihaki Ndung’u, Raphael Mwaura Gacheiya, C. Kitetu","doi":"10.37284/jammk.5.1.769","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.769","url":null,"abstract":"Lugha ni kipengele muhimu cha utambulisho ambacho huweza kuwaunganisha, kuwatenganisha au kuwabagua wazungumzaji katika jamii. Utambulisho ni mtazamo wa kibinafsi wa mtu, yeye ni nani na vibainishi vinavyoashiria ushirika wake katika kikundi fulani cha kijamii. Mitazamo au maoni ya wazungumzaji kuhusu wao ni akina nani au utambulisho wao katika jamii, yanaweza kutofautiana na ushahidi wa kiisimu ambao huweka makundi ya wazungumzaji wanaozungumza lahaja mbalimbali kama wanajamii wa lugha moja. Dhana hii hudhihirika kwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ ambao huchukuliwa kuwa wao si Wakikuyu hata ingawa kiisimu wameainishwa na kuwekwa katika kundi moja kama Wakikuyu. Makala haya yanaazimia kuchunguza mitazamo wanayoendeleza wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ kuhusu utambulisho wao wa kijamii katika jamii. Mtazamo ni tathmini, chanya au hasi, kuelekea kitu au mtu, ambayo hujidhihirisha kwa imani, hisia au nia ya mtu mwenyewe. Kuna wakati wazungumzaji huweza kujinasibisha na kikundi fulani cha kijamii na wakati mwingine kukana utambulisho huo kutokana na sababu mbalimbali. Hii hutokana na wao kuendeleza mitazamo mbalimbali kuhusu utambulisho huo. Utafiti wa makala haya uliongozwa na nadharia ya Tajfel na Turner (1979). Data ilikusanywa kupitia mahojiano na kuchanganuliwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kuwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ wana mitazamo hasi na chanya kuhusu utambulisho wao wa kijamii. Mitazamo hasi ya kubaguliwa na kudhalilishwa ilichangia watafitiwa kukana utambulisho wao na jamiilugha ya Wakikuyu na kujitambulisha kama Wakĩrĩnyaga.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"28 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-07-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123086542","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Muwala katika Vikatuni vya Shujaaz: Mtazamo wa Kiuchanganuzi Makinifu wa Diskosi
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-07-19 DOI: 10.37284/jammk.5.1.759
Dimbu Sammy Liana, John M. Kobia, Allan Mugambi
{"title":"Muwala katika Vikatuni vya Shujaaz: Mtazamo wa Kiuchanganuzi Makinifu wa Diskosi","authors":"Dimbu Sammy Liana, John M. Kobia, Allan Mugambi","doi":"10.37284/jammk.5.1.759","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.759","url":null,"abstract":"Vikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Kumekuwepo na tafiti nyingi kuhusu muwala katika uwanja wa kiusomi. Tafiti za awali zilijikita kwenye muwala katika makala, magazeti, tasnifu, vitabu na vikatuni. Hata hivyo, hakuna utafiti kuhusu muwala katika vikatuni wa Shujaaz. Makala hii inalenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika diskosi ya vikatuni vya Shujaaz. Diskosi hii ni jarida linalowasilishwa kupitia msimbo wa Sheng ambalo hulenga vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 35. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Mojawapo wa madhumuni ya nadharia hii ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za ukweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ni kuwa muwala hukuzwa kupitia: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi panelini na maelezo ya mwandishi. Aina ya muwala uliokuzwa ulitokana na msuko wa hadithi, muwala wa jumla na mada. Utafiti huu unaweka wazi namna kampuni ya WellTold Story ilivyotumia maarifa ya kiusuli katika jamii kukuza muwala wa jumla kama mkakati wa kuendeleza na kuwawekea vijana vizingiti ili kuwadhibiti. Hivyo serikali na mashirika ya kijamii yanaweza kutumia mkakati huu katika kuwaelimisha vijana kuhusu magonjwa ya majanga makubwa kama njia moja ya kupunguza athari zake kwa jamii.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-07-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"127870581","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015)
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-07-04 DOI: 10.37284/jammk.5.1.733
Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi
{"title":"Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015)","authors":"Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.733","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.733","url":null,"abstract":"Suala la ukame limeanza kupata umakini mwingi kwa sababu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa marudio na makali yake. Mathalani, ni mwanzo wa maafa yanayoaminika kuwa chanzo cha kimsingi cha baa la njaa kwa ajili ya uharibifu wa mazao. Kadhalika, ni kutokana na makali ya ukame katika mataifa mbalimbali Barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla, ambapo kumeibuka mijadala mizito miongoni mwa washikadau mbalimbali wa masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tangu kuvumbuliwa kwa uwanja wa fasihi mazingira miaka ya tisini, waandishi wa kifasihi wamejihusisha katika masuala ya kimazingira ili kuchangia katika utatuzi wa matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira. Kwa msingi huu, makala hii inajadili namna watunzi wa tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015) wamesawiri motifu ya ukame kama suala mojawapo la kimazingira kwa lengo la kuweka wazi chanzo na athari zake katika jamii. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti ulifanyiwa maktabani ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule. Kutokana na matokeo ya makala hii, ilibainika kwamba, waandishi wa tamthilia teule wamesawiri suala la ukame kwa namna mbalimbali kwa kuangazia chanzo na athari zake. Hivyo, makala hii imethibitisha kwamba, fasihi ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambayo inaweza kutumika katika kuangazia masuala yanayoathiri jamii. Vilevile, utafiti huu ni muhimu kwa washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu kwa jumla.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"139 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-07-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"116416825","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na Ujifunzaji
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-06-27 DOI: 10.37284/jammk.5.1.724
Edwine Atukunda, Owen McOnyango, D. Amukowa
{"title":"Mchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na Ujifunzaji","authors":"Edwine Atukunda, Owen McOnyango, D. Amukowa","doi":"10.37284/jammk.5.1.724","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.724","url":null,"abstract":"Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa vizuri katika mtihani wa kitaifa. Upande wa Kiswahili, kuna ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na ugumu huu umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda. Wanafunzi hawa wanasomea katika mandhari sawa, kwa hivyo utendaji wao kwenye mtihani unastahili kuwa sawa. Kwa hivyo, makala hii imechanganua mchango wa ushairi wa Kiganda katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili kimuundo. Madhumuni ya makala hii ni: Kufafanua jinsi muundo wa ushairi wa Kiganda unavyoweza kuendeleza muundo wa ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji. Kudadavua jinsi muundo wa ushairi wa Kiswahili unavyoweza kuvunja mipaka iliyowekwa na kupanuka. Makala hii imeongozwa na nadharia ya umuundo ambayo iliasisiwa na Ferdinanda De Saussure (1909) Mihimili ya nadharia hii ni fasihi inastahili kuchunguzwa kama muundo mmoja uliojengwa kwa vipengele tofauti vinavyoshirikiana kukiunda kitu kizima. Pili, huchunguza vipengele mbalimbali vya mfumo wa fasihi kwa kuchunguza jinsi vinavyohusiana na kuchangiana katika kukamilisha kazi husika. Tatu, hulenga maana katika matini ya kifasihi na kupuuza maswala mengine ya nje kama muktadha. Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda. Mashairi 60 yalikusanywa; yaani, 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila diwani kwa kutumia uteuzi nasibu. Mashairi yatatolewa kwenye diwani za Kiswahili; “Malenga wa ziwa kuu” na “Malenga wa karne moja” na za Kiganda; “Ab’Oluganda ab’Enda emu” na “Balya n’ensekeezi”. Kundi lengwa ni walimu watano wa Kiganda na watano wa Kiswahili ambao walichaguliwa kimakusudi na kushiriki katika uchambuzi ambao uliandamana na maoni yao kuhusu ujifunzaji na ufunzaji wa ushairi. Makala hii ilifafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"80 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-06-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"117247444","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Usawiri wa Motifu za Kimazingira Katika Tamthilia ya Kiswahili: Tathmini ya Majira ya Utasa (Arege, 2015)
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-06-10 DOI: 10.37284/jammk.5.1.699
Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi
{"title":"Usawiri wa Motifu za Kimazingira Katika Tamthilia ya Kiswahili: Tathmini ya Majira ya Utasa (Arege, 2015)","authors":"Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.699","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.699","url":null,"abstract":"Suala la kuongezeka kwa viwango vya halijoto na mabadiliko ya tabianchi limeibua mijadala ya kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia na athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira.  Makala hii ilikusudia kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi mwandishi wa tamthilia teule amesawiri motifu za kimazingira ili kuonyesha uharibifu wa mazingira pamoja na matatizo yanayotokana na uharibifu huo. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Kwa hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Kimsingi, nadharia ya uhakiki wa kiekolojia hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Tamthilia iliyohakikiwa iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule. Matokeo ya makala hii yalithibitisha kuwa mwandishi wa tamthilia ya Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira kwa namna mbalimbali kwa kuonyesha njia za uharibifu wa mazingira na athari zake. Hivyo, kushadidia kuwa fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"164 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-06-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"126063017","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab: Uchunguzi wa Kipengele cha Wakati
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-06-10 DOI: 10.37284/jammk.5.1.702
Dorcas Misoi, R. M. Wafula
{"title":"Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab: Uchunguzi wa Kipengele cha Wakati","authors":"Dorcas Misoi, R. M. Wafula","doi":"10.37284/jammk.5.1.702","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.702","url":null,"abstract":"Taarab ni aina ya nyimbo yenye asili katika Pwani ya Afrika Mashariki. Nyimbo hizi kama zilivyo nyimbo zingine, ni zao la shughuli na hisia za binadamu. Hivyo, ujumbe katika nyimbo hizo hujikita katika miktadha mbalimbali ya jamii. Ntarangwi (2001) anasema, mbali na kuwa nyimbo za taarab huimbwa sana katika harusi za Waswahili, nyingi ya nyimbo hizo hugusia masuala mengine ya maisha kama vile uongozi, dini, urembo wa wanawake, mabadiliko ya kisiasa au hata kuhusu uchungu wa kumpoteza mpenzi. Masuala haya huwasilishwa na watribu kwa kutumia mbinu za lugha kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Makala haya yamechunguza dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa nyimbo za taarab kwa kuzingatia kipengele mahsusi cha wakati. Kazi hii imeongozwa na nadharia ya naratolojia inayohusishwa na mwanafalsafa wa Kiyunani aitwaye Plato na kuendelezwa na wataalamu kama vile Genette, Stanzel, Manfred Jan na Mieke Bal. Nadharia hii inahusu usimuliaji wa hadithi. Misingi yake ni kuwa usimulizi lazima uwe na msimulizi, kitendo kinachosimuliwa, usemi kuhusu kinachofanyika, wahusika na dhamira ya usimulizi wowote hubainika kupitia kwa mtazamo wa msimulizi. Kipengele cha usimulizi cha wakati kimetumiwa kuonyesha dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa maudhui na mtindo wa uwasilishi katika nyimbo za taarab. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha kuwa kipengele cha usimulizi cha wakati kimedhihirika katika nyimbo teule za taarab na kimechangia kukuza maudhui na mtindo wa uwasilishi kwa kuonyesha kuwa wimbo wa taarab ni utanzu telezi unaosheheni usimulizi","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"22 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-06-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"121617676","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
‘Huyu Mtu Hasimami’: Uhuishi katika Mazungumzo ya Daktari na Wanaume katika Kliniki ya Afya ya Uzazi, Kenya
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-05-30 DOI: 10.37284/jammk.5.1.685
Melvin Atieno Ouma, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu
{"title":"‘Huyu Mtu Hasimami’: Uhuishi katika Mazungumzo ya Daktari na Wanaume katika Kliniki ya Afya ya Uzazi, Kenya","authors":"Melvin Atieno Ouma, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu","doi":"10.37284/jammk.5.1.685","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.685","url":null,"abstract":"Lugha ni kiungo muhimu katika mawasiliano kati ya daktari na mgonjwa. Katika kliniki ya afya ya uzazi, kutaja sehemu za mwili kwa majina yao ni kigezo muhimu katika utoaji na upokeaji wa huduma za afya. Ujinaishaji ni jambo la zamani kama ilivyo ubinadamu. Ujinaishaji wa sehemu za siri ina historia ndefu kutoka karne ya zamani sana. Ujinaishaji wa sehemu hizi ni jambo linalofanyika katika mataifa yote ulimwenguni. Makala haya yanaangazia uhuishi unavyotumiwa na wanaume kama mkakati wa mazungumzo katika kliniki ya afya ya uzazi. Kuafikia hili, makala haya yatashughulikia majina ambayo wanaume wanayapa sehemu zao za siri katika kliniki ya afya ya uzazi. Pia yatafafanua sifa na tabia za kibinadamu zinazopewa sehemu za siri katika mazungumzo ya wanaume na daktari kuhusu matatizo ya afya ya uzazi. Majina kama vile dick, mwanaume, uume, mkuki, chuma na huyu mtu ni baadhi ya majina wanaume walitumia kutaja sehemu zao za siri. Sehemu za siri ya wanaume ilipewa sifa na tabia za kibinadamu kupitia urejeleo kwa ngeli ya A-WA. Matumizi ya ngeli ya A-WA ni idhibati kuwa dhakari ni kama binadamu na wala si sehemu ya mwili ya kawaida kama inavyodhaniwa. Uhuishi ulijitokeza katika mazungumzo kupitia maneno kama vile anakataa, hakubali, hasimami, anajikunja. Semi za wanaume zinaonyesha kuwa dhakari ina uwezo wa kuamuka na kufanya kazi. Dhakari ina uwezo wa kutoa adhabu. Ina uwezo wa kusimama. Ina uwezo wa kuwa imara na ina uwezo wa kuenda. Sehemu za siri za mwanamume zina maisha yake na fahamu zake kando na yule mwanamume anayemiliki sehemu hizo. Kupitia mazungumzo ya daktari na mgonjwa, sehemu za siri (dhakari) ndio sehemu ya mwili inayothaminiwa zaidi miongoni mwa wanaume.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"89 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"132714078","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-05-30 DOI: 10.37284/jammk.5.1.686
Harrison Onyango Ogutu
{"title":"Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi","authors":"Harrison Onyango Ogutu","doi":"10.37284/jammk.5.1.686","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.686","url":null,"abstract":"Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule. Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu. Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia. Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa. Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu. Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii. Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi. Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"31 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123064325","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Uhakiki wa Nafasi ya TEKNOHAMA katika Kukuza Maudhui katika Tamthilia ya Kigogo
East African Journal of Swahili Studies Pub Date : 2022-05-18 DOI: 10.37284/jammk.5.1.671
John Kennedy Mwangi
{"title":"Uhakiki wa Nafasi ya TEKNOHAMA katika Kukuza Maudhui katika Tamthilia ya Kigogo","authors":"John Kennedy Mwangi","doi":"10.37284/jammk.5.1.671","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.671","url":null,"abstract":"Fasihi ni zao la jamii na hubadilika kila uchao. Uwakilishi wa suala la TEKNOHAMA katika tamthilia za kisasa umechukua mkondo mpya. Hii ni kwa sababu, kutokana na jinsi dunia inavyobadilika ndivyo masuala ya kiteknolojia pia yanavyoathiri fasihi ya sasa na kuipa mguso na taathira mpya. Licha ya uwakilishi wa TEKNOHAMA kuwa na umuhimu katika kukuza fani na maudhui katika fasihi, mchango wake katika tamthilia ya Kigogo haujafanyiwa utafiti, suala linalomchochea mtafiti kulitafiti. Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini mchango wa TEKNOHAMA katika kukuza maudhui katika tamthilia ya Kigogo ya Pauline Kea (2016). Utafiti huu unaongozwa na Nadharia ya Uhalisia. Uteuzi wa sampuli utafanywa kimakusudi na utafiti wenyewe ni wa muundo wa kiudhamano. Mtafiti atasoma makala mbali mbali kuhusiana na mada na kisha kuichanganua data kwa njia ya kimaelezo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-05-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130799392","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
相关产品
×
本文献相关产品
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信