{"title":"Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000","authors":"Elihaki Yonazi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1395","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika. Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi. Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake. Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika. Makala hii imetumia data za maktabani. Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika. Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule. Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule. Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili. Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura. Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"342 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-08-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1395","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika. Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi. Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake. Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika. Makala hii imetumia data za maktabani. Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika. Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule. Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule. Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili. Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura. Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo