Majele Noah Munda, Eric W. Wamalwa, Simiyu Benson Sululu
{"title":"Mchango wa Mofofonolojia ya Kiduruma kwa Ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili","authors":"Majele Noah Munda, Eric W. Wamalwa, Simiyu Benson Sululu","doi":"10.37284/jammk.6.1.1227","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yamedadavua mchango wa mofofonolojia ya Kiduruma kwa ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Kwale nchini Kenya. Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na Joan Hooper (1971) iliongoza utafiti. Mkabala wa kithamano na muundo wa kiethinografia ulitumiwa katika uchunguzi. Data ilikusanywa kutokana na insha za wanafunzi kwa kutumia mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionesha kuwa kuna mwingiliano katika vipengele vya mofofonolojia ya Kiduruma na Kiswahili, hali inayoleta uwezekano wa kuendeleza ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kwa kutumia mofofonolojia ya Kiduruma. Imebainika kwamba ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kama vile fonimu, miundo ya silabi, ngeli, nyakati mbalimbali na mnyambuliko wa maneno unaweza kufaidi kutokana na mofofonolojia ya Kiduruma. Kutokana na matokeo hayo, uchunguzi huu unapendekeza kwamba, katika eneo la utafiti ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ni Waduruma, mofofonolojia ya Kiduruma inaweza kutumiwa kama wenzo wa ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"5 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-05-24","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1227","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala haya yamedadavua mchango wa mofofonolojia ya Kiduruma kwa ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Kwale nchini Kenya. Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na Joan Hooper (1971) iliongoza utafiti. Mkabala wa kithamano na muundo wa kiethinografia ulitumiwa katika uchunguzi. Data ilikusanywa kutokana na insha za wanafunzi kwa kutumia mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionesha kuwa kuna mwingiliano katika vipengele vya mofofonolojia ya Kiduruma na Kiswahili, hali inayoleta uwezekano wa kuendeleza ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kwa kutumia mofofonolojia ya Kiduruma. Imebainika kwamba ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kama vile fonimu, miundo ya silabi, ngeli, nyakati mbalimbali na mnyambuliko wa maneno unaweza kufaidi kutokana na mofofonolojia ya Kiduruma. Kutokana na matokeo hayo, uchunguzi huu unapendekeza kwamba, katika eneo la utafiti ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ni Waduruma, mofofonolojia ya Kiduruma inaweza kutumiwa kama wenzo wa ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili.