{"title":"Mikabala Tofauti ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada kuhusu Kipengele cha Mtindo wa Uandishi Insha za Kiswahili Nchini Kenya","authors":"Nester Ateya, Eric W. Wamalwa, S. A. Kevogo","doi":"10.37284/jammk.7.1.1803","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yanabainisha mikabala ya waandishi wa vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili kwa shule za upili nchini Kenya. Mikabala tofauti ya waandishi aghalabu huwa chanzo cha utata miongoni mwa walimu na wanafunzi na hivyo kuathiri matokeo ya mtihani wa kitaifa. Uchunguzi huu umekitwa kwa mihimili ya Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Louis Tonko Milic. Nadharia hii inashikilia kuwa mtindo hutegemea mtu binafsi. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo, mkabala wa kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ni walimu wa somo la Kiswahili 73, wanafunzi 2,000 na vitabu vya kiada 7 vya shule za upili. Kwa hivyo, usampulishaji wa kimakusudi ulitumiwa kuteua walimu 22, wanafunzi 320 na vitabu vya kiada 6. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo, mahojiano na hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia asilimia, majedwali na kuwasilishwa kiufafanuzi. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kwamba, matumizi ya vitabu vya kiada tofauti tofauti yanazua mikabala tofauti katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha. Hali hii inatokana na waandishi wa vitabu kiada kuwa na mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha za Kiswahili. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, viwango vingine vya elimu na wakuza mitaala pamoja na waandishi wa vitabu vya kiada. Wizara ya Elimu pamoja na vyuo vya walimu kupitia warsha na maarifa zaidi ya yale ya vitabu vya kiada, watafaidi mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa somo la insha","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"94 12","pages":""},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2024-03-06","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1803","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala haya yanabainisha mikabala ya waandishi wa vitabu vya kiada katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili kwa shule za upili nchini Kenya. Mikabala tofauti ya waandishi aghalabu huwa chanzo cha utata miongoni mwa walimu na wanafunzi na hivyo kuathiri matokeo ya mtihani wa kitaifa. Uchunguzi huu umekitwa kwa mihimili ya Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Louis Tonko Milic. Nadharia hii inashikilia kuwa mtindo hutegemea mtu binafsi. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo, mkabala wa kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ni walimu wa somo la Kiswahili 73, wanafunzi 2,000 na vitabu vya kiada 7 vya shule za upili. Kwa hivyo, usampulishaji wa kimakusudi ulitumiwa kuteua walimu 22, wanafunzi 320 na vitabu vya kiada 6. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo, mahojiano na hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia asilimia, majedwali na kuwasilishwa kiufafanuzi. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kwamba, matumizi ya vitabu vya kiada tofauti tofauti yanazua mikabala tofauti katika ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha. Hali hii inatokana na waandishi wa vitabu kiada kuwa na mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha za Kiswahili. Matokeo ya uchunguzi huu ni muhimu kwa walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, viwango vingine vya elimu na wakuza mitaala pamoja na waandishi wa vitabu vya kiada. Wizara ya Elimu pamoja na vyuo vya walimu kupitia warsha na maarifa zaidi ya yale ya vitabu vya kiada, watafaidi mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa somo la insha