{"title":"Wingilugha na Maendeleo Endelevu katika Kaunti Nchini Kenya: Hali Halisi katika Kaunti ya Machako","authors":"Peter Willington Kilonzo, Nabeta K. N. Sangili","doi":"10.37284/jammk.5.2.991","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Ulimwenguni kote, lugha imekuwa na bado inaendelea kuwa raslimali muhimu katika maendeleo ya sehemu yoyote ile. Kwa watu wengine, lugha ni mtaji katika shughuli zozote za kimaendeleo kwa sababu bila lugha inayoeleweka na washiriki husika hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na iwapo yatafanyika, kasi yake itakuwa ya chini sana. Katiba ya 2010 ilifanya mabadiliko mengi na mojawapo ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi sawa na Kiingereza. Katiba hii pia ilitengeneza serikali 47 za magatuzi ambazo zina upekee wake wa utamaduni, lugha ikiwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kaunti hizi. Hivyo, angalau kila Kaunti ina lugha tatu zinazozungumzwa humo. Zaidi ya lugha husika tatu, shughuli tofauti zimechangia watu wa jamii mbalimbali kuhamia na kutagusana katika Kaunti tofauti na za kwao, jambo linalosababisha wingilugha dhahiri katika Kaunti zote nchini Kenya. Katika hali hii, swali kuu linakuwa ni: je, lugha ikiwa ni raslimali na mtaji muhimu katika maendeleo, wingilugha unaweza kutumika vipi katika muktadha wa Kaunti ili kuhakikisha maendeleo endelevu? Swali hili linakuwa msingi mkuu wa makala haya kuangazia jinsi wingilugha (Kiswahili, Kiingereza, Lugha asili, na lugha nyinginezo) unavyoweza kutumika katika muktadha wa Kaunti nchini Kenya ili kuhakikisha maendeleo endelevu katika kila Kaunti. Utafiti umejikita katika Kaunti ya Machakos.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-12-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.991","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Ulimwenguni kote, lugha imekuwa na bado inaendelea kuwa raslimali muhimu katika maendeleo ya sehemu yoyote ile. Kwa watu wengine, lugha ni mtaji katika shughuli zozote za kimaendeleo kwa sababu bila lugha inayoeleweka na washiriki husika hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na iwapo yatafanyika, kasi yake itakuwa ya chini sana. Katiba ya 2010 ilifanya mabadiliko mengi na mojawapo ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi sawa na Kiingereza. Katiba hii pia ilitengeneza serikali 47 za magatuzi ambazo zina upekee wake wa utamaduni, lugha ikiwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kaunti hizi. Hivyo, angalau kila Kaunti ina lugha tatu zinazozungumzwa humo. Zaidi ya lugha husika tatu, shughuli tofauti zimechangia watu wa jamii mbalimbali kuhamia na kutagusana katika Kaunti tofauti na za kwao, jambo linalosababisha wingilugha dhahiri katika Kaunti zote nchini Kenya. Katika hali hii, swali kuu linakuwa ni: je, lugha ikiwa ni raslimali na mtaji muhimu katika maendeleo, wingilugha unaweza kutumika vipi katika muktadha wa Kaunti ili kuhakikisha maendeleo endelevu? Swali hili linakuwa msingi mkuu wa makala haya kuangazia jinsi wingilugha (Kiswahili, Kiingereza, Lugha asili, na lugha nyinginezo) unavyoweza kutumika katika muktadha wa Kaunti nchini Kenya ili kuhakikisha maendeleo endelevu katika kila Kaunti. Utafiti umejikita katika Kaunti ya Machakos.