{"title":"Usawiri Chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria","authors":"Maroa Dunstan Sospeter, Catherine Ndungo","doi":"10.37284/jammk.7.1.2048","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2048","url":null,"abstract":"Makala hii imechunguza usawiri chanya wa hadhi ya mwanamke katika methali za Igikuria. Swala la usawiri wa mwanamke limeshughulikiwa na watafiti wa awali huku tafiti zao zikiibua usawiri hasi wa mwanamke. Tafiti hizi za awali kama za Matteru (1993) na Ndungo (1998) zilifanywa kuhusu vipera vya fasihi simulizi kama vile; nyimbo na methali zilidhihirisha namna tofauti mwanamke anavyodunishwa katika jamii za Kiafrika. Udunishwaji huu unatokana mifumo tawala inayompendelea mwanamume. Mifumo hii imejificha katika mila na desturi potovu za jamii mbalimbali. Aidha, ingawa jamii huweza kumdunisha mwanajamii yeyote yule kwa kutegemea matendo yake, kuna miktadha mbalimbali ambayo humfanya mtu kupata sifa nzuri kulingana na matendo yake mazuri. Mwanamke anapochangia katika shughuli mbalimbali za jamii hupewa sifa si haba. Kutokana na haya, panaibuka haja ya kuchunguza usawiri chanya wa mwanamke katika methali za Igikuria kwa kudhihirisha anavyotukuzwa katika jamii, miktadha inayompelekea kusifiwa na mchango anaotoa katika kuendeleza asasi mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Ufeministi ambayo iliwekewa misingi na Wollstonecraft (1992), Woolf (1929) na Beauvoir (1994). Mihimili ya Ufeministi iliyotuongoza ni usawazishaji wanadamu kwa upande wa utamaduni na uana, utumiaji wa fasihi kama jukwaa la kueleza kwa uyakinifu hali inayomkumba mwanamke ili iweze kueleweka na watu wengi na kuhamasisha watumiaji wa sanaa wawe na wahusika wa kike ambao ni vielelezo wenye uwezo na wanaoweza kuigwa. Data iliyotumika katika Makala hii ilitolewa maktabani na nyanjani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Nyanjani, data ya methali za kumtukuza mwanamke ilikusanywa kwa njia ya hojaji. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonyesha kuwa katika methali za Igikuria, mwanamke amesawiriwa kama mfadhili katika ukoo anaotoka, mshauri wa jamii, kiongozi katika shughuli muhimu za jamii (sherehe), mtetezi wa jamii, mlezi, mjenzi wa familia na msingi thabiti katika jamii. Pia mwanamke amejitokeza kuwa chemchemi katika maisha ya Wakuria. Hidaya na uwezo wa kipekee aliotunukiwa mwanamke na Jalali katika kuendeleza jamii kupitia kwa njia ya uzazi, unamfanya kusifiwa kiasi kuwa mji usio na mwanamke hulinganishwa na chaka lisiloingilika. Aidha, miktadha ya kijamii ambayo inapelekea mwanamke kutukuzwa ni ya sherehe za kitamaduni, shughuli za kilimo na uzalishaji mali, shughuli za uzazi na malezi","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"22 5","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-07-15","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141645840","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika Upya wa Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’","authors":"Gladys Kinara, P. Ngugi, R. M. Wafula","doi":"10.37284/jammk.7.1.2043","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2043","url":null,"abstract":"Makala hii inalenga kuchunguza mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika upya wa tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’ Robert (1967). Mapokeo yanaweza kuelezwa kama mila, desturi, fikra na hisia za kihistoria zinazohusu mtazamo sio tu wa yaliyopita zamani lakini pia uwepo wa mambo ya kihistoria na ya sasa kwa lengo la kuyapitisha kwa jamii (Sangi na wengine, 2012). Uchambuzi wa kazi hii umeegemezwa katika mihimili ya nadharia ya Bakhtin (1981) inayoshikilia kwamba lugha huwa na nguvu za Kani Kitovu na Kani Pewa. Kiwango cha Kani Kitovu huhusu nguvu za kisheria zinazotambulisha lugha. Hizi ni sheria za kisarufi na hazibadiliki. Katika muktadha wa fasihi, nguvu hizi zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kiwango cha Kani Pewa nacho kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanatofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Kitovu zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kwa upande mwingine, kiwango cha Kani Pewa kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanayotofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Pewa zinawakilisha upya na katika muktadha huu Utenzi wa Mwana Kupona katika tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’. Utafiti ulikuwa wa kimaelezo na ulifanywa maktabani na nyanjani. Sampuli ya maktabani na nyanjani iliteuliwa kimakusudi. Maktabani, mtafiti alisoma kwa kina matini iliyochapishwa kwa lengo la kupata data ya msingi. Nyanjani, mtafiti alifanya mahojiano na majadiliano na wanajamii walioteuliwa katika kukusanya data. Data kutoka katika tenzi zilizoteuliwa, maandishi yaliyohusu utafiti, data ya nyanjani zilichambuliwa kulingana na lengo la makala haya na mihimili ya nadharia kwa lengo la kuonyesha namna mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona yalivyobainika katika upya wa maandishi ya tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kwamba Shaaban Robert (1967) katika kuandika ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’ aliazima pakubwa kutoka katika Utenzi wa Mwana Kupona mbali na kuongeza upya kwa mujibu wa hali ya kijamii ya wakati wake","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"22 6","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-07-11","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141658934","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Usawiri Wa Vyanzo Vya Dhuluma Za Kijinsia Katika Riwaya Teule Za Kiswahili","authors":"Pamella Tsiyeli Ngeleso, Alex Umbima Kevogo","doi":"10.37284/jammk.7.1.2024","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2024","url":null,"abstract":"Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya 2020 inatoa takwimu za kusikitisha kuhusu idadi ya waathiriwa wa dhuluma za kijinsia duniani. Data hii ilichochea utafiti huu kuhusu dhuluma za kijinsia na zinavyosawiriwa katika kazi za fasihi. Kimsingi utafiti huu ulikuwa wa maktabani; ambapo watafiti walisoma na kuhakiki riwaya teule za ‘Nyuso za Mwanamke’ ya Said Ahmed Mohamed na ‘Unaitwa Nani?’ ya Kyalo Wadi Wamitila. Uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumika ili kuchagua riwaya moja ya kila mwandishi kwa mujibu wa mada ya dhuluma za kijinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ufeministi Mamboleo iliyoasisiwa na Jacques J. Zephire mwaka wa 1982. Aidha, utafiti huu ulizingatia pia Nadharia ya Hegemonia ya Ubabedume iliyoasisiwa na Raewyn Connell mnamo 1987. Kimsingi, utafiti huu ulilenga kubainisha vyanzo vya dhuluma ya kijinsia na namna vinavyosawiriwa katika riwaya ‘Nyuso za Mwanamke’ na ‘Unaitwa Nani?’. Matokeo ya utafiti yanayohusu data ya kiuthamano yaliwasilishwa kupitia kwa maelezo na ufafanuzi unaotolewa kwa kuegemea mihimili ya Nadharia ya Ufeministi Mamboleo na Nadharia ya Hegemonia ya Ubabedume. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa riwaya hizi zinasawiri wahusika mbalimbali wanaokuza maudhui ya dhuluma ya kijinsia. Utafiti huu utawafaa wahakiki wengine wa kazi za fasihi kupata maarifa mapya yanayohusu masuala ya kijinsia. Aidha, wanaharakati wanaopambana na suala la dhuluma za kijinsia watapata mapendekezo ya waandishi na watafiti kuhusu njia za kupambana na tatizo hili. Isitoshe, serikali na vyombo visivyo vya kiserikali vinavyoshughulikia suala la dhuluma za kijinsia vitashauriwa kuhusu njia mwafaka za kudumisha utangamano na mahusiano ya kijinsia duniani, Afrika, Afrika Mashariki na hata nchini Kenya","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":" 10","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-07-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141676981","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Upembezwaji wa Mwanamke kama Kihunzi cha Ufanisi wa Ujenzi wa Ujitambuzinafsia Katika Baadhi ya Bunilizi za Clara Momanyi","authors":"Kawira Kamwara","doi":"10.37284/jammk.7.1.1978","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1978","url":null,"abstract":"Jamii nyingi za Kiafrika ni za kuumeni na humpembeza mwanamke kwa kumweka katika ngazi za chini akilinganishwa na mwanamume. Upembezwaji wa mwanamke katika tungo za kifasihi na katika maendeleo ya jamii ni matokeo ya mwingiliano wa fahamu tambuzi na fahamu bwete za mtunzi hasa kwa mujibu wa utamaduni wa jamii lengwa. Mwingiliano huu wa ufahamu tambuzi na ufahamu bwete unaekezwa kwa makusudi katika utunzi wa tungo mahususi kama ilivyo kwenye tungo za Momanyi ‘Ngome ya Nafsi’ katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Tumaini (2006) na Nakuruto (2010). Nadharia tuliyotumia ni ya Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Steady (1981). Mwanaufeministi huyu alisema kuwa Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika huweka masuala pamoja ya kijinsia, ubaguzi, mielekeo ya kiutamaduni na tabaka ili kumwangalia mwanamke kama kiumbe mtegamewa bali sio mtegemezi. Data ya usomi huu ilitokana na usomaji wa bunilizi hizi maktabani. Tuliweza vilevile kutumia mitandao kurutubisha utafiti wetu. Hivyo, ni kwa jinsi gani ambavyo utamaduni unatinga ufanisi wa mwanamke kisanii katika jamii? Ni mikakati ipi ambayo jamii imeweka kupigania ufanisi wa mwanamke? Mwanamke anachangia vipi upembezwaji wa kijinsia? Maswali haya ndiyo tulipania kuyajibu katika Makala haya.","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":" 16","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-06-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141365891","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Nafasi Ya Fasihi Andishi Ya Watoto Kama Chombo Cha Malezi Kwa Watoto Wa Kisasa","authors":"N. N. Musembi, Peter Karanja","doi":"10.37284/jammk.7.1.1924","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1924","url":null,"abstract":"Fasihi andishi ya watoto ina nafasi kubwa ya kuwasaidia watoto kuelewa mazingira yao pamoja na kujenga mwonoulimwengu wao kulingana na wanachosoma. Hii ni kutokana na sababu kwamba watoto hubwia wasomacho kuwa kiwakilishi cha uhalisia katika jamii. Fasihi ya watoto huchokoza fikra zao na kuwachochea kufikiria, kuimarisha msamiati wao, na pia huwasaidia kujifahamu kando na kuwafahamu watu wengine. Fasihi hii hivyo basi inajitokeza kama kioo ambacho watoto wanajiona kwacho na pia dirisha la kuwawezesha kuutalii ulimwengu unaowazunguka. Fasihi andishi ya watoto vilevile ina uwezo wa kuonyesha kuwa, watu tofauti wanaweza kufanya kazi pamoja bila ubaguzi wa aina yoyote. Waandishi wa fasihi ya watoto hivyo basi hubuni ulimwengu ambao watoto wanaweza kuutambua kwa urahisi na kujinasibisha nao. Kwa msomaji mtoto, hali hii hurahisisha uvushaji wa maarifa na kuifanya fasihi andishi yao kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha mtagusano wa kijamii pamoja na uvushaji wa maarifa ya kiakademia. Lengo la makala hii ni kubainisha kuwa, kupitia fasihi andishi ya watoto ya Kiswahili, msomaji mtoto anaweza kufafanukiwa na hali halisi ya maisha yake na wakati huo huo kupata suluhu ya kutatua matatizo yanayomkumba na ya jamii yake. Kazi hii itafanya hivyo kwa kuhakiki vitabu vya fasihi andishi ya watoto vifuatavyo: Momanyi, C (2006) Tumaini, Momanyi, C. (2005), Siku ya Wajinga, Musembi, N. (2009) Nipe Sababu, Musembi, N. (2019) Dhiki Yangu Ngugi, P. (2003) Usicheze na Moto Mdari, A. (2001) Alitoroka kwao. Ndoto ya Mwanafunzi, Manji, M (2013), na Safari ya Sungura Omusikoyo T, ( 2021). Makala hii inatoa mwito kwa waandishi wa fasihi ya watoto watunge vitabu vitakavyo wasaidia watoto kukabiliana na hali zote za maisha yao wanapoendelea kukua katika dunia hii inayobadilika kila uchao","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"28 14","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140982932","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Chanzo cha Makosa ya Kiisimu Miongoni mwa Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili","authors":"Nancy Wanja Njagi, David Kihara","doi":"10.37284/jammk.7.1.1912","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1912","url":null,"abstract":"Kiswahili kimekuwa muhimu sana hata kabla ya ujio wa wakoloni nchini Kenya hasa katika kuendeleza mawasiliano. Kabla ya wakoloni, Kiswahili kilitumika katika maeneo ya Pwani kuendeleza mawasiliano ya kibiashara miongoni mwa wakaazi wa Pwani na Waarabu. Biashara ilipoendelea kunoga na watu kutoka maeneo ya bara kuanza kushiriki katika biashara ya pale pwani, Kiswahili kilienea na matumizi yake yakapanuka. Licha ya kupanuka kimatumizi Kiswahili kimekubwa na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa ni kuwepo kwa makosa ya kiisimu hasa kwa wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Hivyo basi utafiti huu ulikusudia kubaini chanzo cha makosa ya kiisimu miongoni mwa wanafunzi hasa wanaozungumza lahaja ya Kigichugu wanapojifunza kiswahili kama lugha ya pili. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu zilizoteuliwa kwa kutumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Wanafunzi walioshiriki katika shule hizi walichaguliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji wa kinasibu pale ambapo walipatiwa nambari kinasibu na waliopata nambari moja hadi sita kuteuliwa. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji, na masimulizi na kuwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa wengi wa wanafunzi katika shule za upili za kutwa katika eneo la Gichugu hujifunza Kigichugu kama lugha yao ya kwanza. Isitoshe, wengi huanza kutumia Kiswahili wanapojiunga na shule. Isitoshe, utafiti huu ulidhihirisha makosa mengi ya kiisimu (yaliyovunja kanuni za nadharia ya Sintaksia Finyizi) yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Vyanzo vya makosa haya ambavyo vinaegemea kwa kiasi kikubwa kwa L1 ni : uhamishaji wa mifumo ya kiisimu, tafsiri sisisi, na ujumlishaji mno","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"19 2","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-07","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141004178","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Makosa ya Kiisimu Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili","authors":"Nancy Wanja Njagi, David Kihara","doi":"10.37284/jammk.7.1.1842","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1842","url":null,"abstract":"Binadamu wanahitaji lugha ili kuwasiliana na mojawapo ya lugha maarufu ulimwenguni ni Kiswahili. Kiswahili kimetafitiwa na wataalamu wengi ili kutafuta suluhisho la baadhi ya changamoto zinazokumba lugha hii na kuiboresha. Mojawapo ya changamoto na suala ambalo halijatafitiwa na utafiti huu ulikusudia kubaini ni makosa ya kiisimu ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili : Uchunguzi kuhusiana na lahaja ya Kigichugu.Utafiti huu ulitumikiza kanuni na mihimili ya nadharia ya Sintaksia Finyizi ili kuweka wazi makosa ya kisintaksia na kisemantiki yanayofanywa na wanagenzi wa Kigichugu wanapojifunza Kiswahili kama L2. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu kwa sababu ndiko kuna wazungumzaji asilia wa Kigichugu. Katika utafiti huu tulipaswa kuteua shule,na wanafunzi wa kufanyia utafiti. Katika uchaguzi wa shule za kutwa za kufanyia utafiti tulitumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Katika uteuzi wa wanafunzi tulitumia usampulishaji wa kinasibu pale ambapo tulipatia wanafunzi nambari kinasibu na kuteua waliopata nambari moja hadi sita. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji , insha na masimulizi . Data ya utafiti iliwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makosa mengi ya kisintaksia na kisemantiki yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Makosa haya ni kama vile: makosa ya wanafunzi wagichugu katika matumizi ya nomino, vitenzi, vipatanishi, vivumishi, vibainishi, vielezi, vihusishi na vishamirishi. Makosa haya yalipelekea si tu kuibuka kwa muundo wa sentensi usiokubalika(sintaksia) bali hata kuwepo kwa maana, tofauti na iliyokusudiwa na wanafunzi hawa au isiyoeleweka, hivyo basi kuwepo kwa makosa ya kisemantiki (semantiki leksika na semantiki mantiki). Makosa haya yalichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sintaksia Finyizi na kudhihirisha ukiukaji wa kanuni za nadharia hii","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"4 9","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140375219","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili","authors":"Daniel Mburu Mwangi","doi":"10.37284/jammk.7.1.1843","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1843","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, utafiti huu umechunguza changamoto au ugumu wanaokumbana nao wanukuzi wa maandishi haya na athari yake kwa wanafunzi wasioona katika elimu. Utafiti wa nyanjani ndio uliofaa kazi hii, nazo mbinu za kukusanya data zilizozofaa ni hojaji na mahojiano. Wanafunzi walipewa kazi ya kuandika insha zilizopewa wanukuzi walizozinukuu ili kuchanganuliwa. Uchunguzi huu ulikusudiwa kufanywa katika vyuo vya elimu kama vile Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Maseno, Taasisi ya Elimu ya Machakos, Taasisi ya Wasioona ya Kenya na Taasisi ya Elimu ya Kagumo kwa sababu vyuo hivi ndivyo vilivyo na wahadhiri wengi wasiojua kusoma breili na mara nyingi husaidiwa na wanukuzi kunukuu kazi za breili katika maandishi ya kawaida ili wakapate kusoma na kuelewa. Kutokana na utafiti huu ni wazi kuwa tafsiri ya breili ya Kiswahili hadi maandishi ya kawaida imepungukiwa katika kuwasilisha maana iliyokusudiwa kwa sababu ya ukosefu wa breili sanifu ya Kiswahili, kuwepo kwa changamoto zilizofafanuliwa katika tasnifu hii na ukosefu wa umilisi katika breili ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na wanukuzi huathiri pakubwa tafsiri ya maandishi haya. Utafiti huu utawanufaisha wanaotumia breili, walimu wao na wanukuzi wa maandishi haya ya breili","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"26 15","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-03-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140375542","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Polisemi Ambazo Zimeundwa Kutokana Na Sitiari Na Metonimu Katika Kiswahili","authors":"Mark Elphas Masika, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.7.1.1769","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1769","url":null,"abstract":"Makala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili. Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi . Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu. Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"58 9","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-02-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140440126","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mwingilianomatini kama Upekee wa Mtindo wa Emmanuel Mbogo: Mifano Kutoka Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo","authors":"H. Jilala","doi":"10.37284/jammk.7.1.1770","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1770","url":null,"abstract":"Makala haya yanahusu mwingilianomatini kama upekee wa mtindo wa Emmanuel Mbogo kwa kurejelea tamthiliya zake mbili: Ngoma ya Ng’wanamalundi (1988) na Fumo Liongo (2009). Lengo la Makala haya ni kuibua upekee wa kimtindo wa Emmanuel Mbogo kupitia matumizi ya mwingilianomatini kwa kuangazia tamthiliya zake mbili alizoandika kwa kupishana muongo mmoja. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu mbili za ukusanyaji data ambazo ni usomaji makini na usaili. Aidha, nadharia ya mwingilianomatini imetumika katika kuchambua na kujadili data. Makala haya yanajadili kuwa matumizi ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo yanadhihirisha upekee wake wa kimtindo katika utunzi wake. Hili linajidhihirisha katika matumizi ya hadithi, ngoma, nyimbo, majigambo, wahusika wa fasihi simulizi, ushairi na nguvu za sihiri. Hivyo, makala haya yanahitimisha kuwa kila mtunzi ana upekee wake katika utunzi na uandishi wa kazi za fasihi, upekee huu hujidhihirisha katika uteuzi wa mtindo ambao unajirudiarudia katika kazi zake","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"5 5","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-02-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140441208","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}