{"title":"Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya","authors":"Alexander Rotich","doi":"10.37284/jammk.7.1.1754","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754","url":null,"abstract":"Madhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-02-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139781160","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya","authors":"Alexander Rotich","doi":"10.37284/jammk.7.1.1754","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754","url":null,"abstract":"Madhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-02-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139840925","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu","authors":"Daniel Mburu Mwangi","doi":"10.37284/jammk.7.1.1712","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1712","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia lengo la tatu na la nne. Mbinu za utafiti zifuatazo ndizo zilizotumiwa kukusanya data; uchunzaji, hojaji na mahojiano. Utafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139608801","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Mercy Moraa Motanya, Stephen Njihia Kamau, Boniface Ngugi
{"title":"Athari za Mtagusano wa Lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa Lugha ya Kishona","authors":"Mercy Moraa Motanya, Stephen Njihia Kamau, Boniface Ngugi","doi":"10.37284/jammk.7.1.1703","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1703","url":null,"abstract":"Utafiti huu unalenga kuchunguza athari zinazotokana na mtagusano wa lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa lugha ya Kishona. Shona ni kabila mojawapo la Wabantu ambao asili yao ni nchini Zimbabwe na walifika nchini Kenya zaidi ya miaka sitini iliyopita kama wamishenari. Kufikia sasa, Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya katika Kaunti ya Kiambu inayojulikana kwa wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai. Mtagusano wa lugha unapotokea, lugha husika huathirika kwa viwango mbalimbali kama vile kwenye fonetiki, kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na hata kisemantiki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uthabiti wa kiisimujamii wa lugha iliyoasisiwa na Giles, Bourhis na Taylor (1977) na kuendelezwa na Landweer (2000) na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977). Mawanda mawili yalihusishwa ambayo ni utafiti wa maktabani na wa nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyika katika makazi ya wanajamiilugha ya Kishona ili kupata data ya moja kwa moja iliyojibu swali la utafiti. Jumuiya ya utafiti ilikuwa kabila la Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu.Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji data ni pamoja na hojaji, mahojiano, uchunzaji, mijadala ya vikundi vidogovidogo na maswali mepesi yaliyoandaliwa kimbele. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo, takwimu na asilimia huku yakiongozwa na nadharia mbili za utafiti. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ulikuwa wa manufaa kwa taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi utamaduni wa Washona na mwelekeo wa udumishaji kwa lugha za kabila mbalimbali","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139608027","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Athari ya Rasimu za Breili katika Usimilishaji wa Ishara Za Isimu","authors":"Daniel Mburu Mwangi","doi":"10.37284/jammk.7.1.1714","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1714","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yatashughulikia lengo la kwanza. Mbinu za utafiti zifuatazo ndizo zilizotumiwa kukusanya data; uchunzaji, hojaji na mahojiano. Utafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139605914","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili","authors":"Daniel Mburu Mwangi","doi":"10.37284/jammk.7.1.1699","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1699","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia vikwazo vya usimilishaji wa ishara za isimu katika breili. Mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano katika kukusanya dataUtafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139616127","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Ambrose Ngesa Kang’e, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi
{"title":"Matumizi ya Usohalisia wa Kihistografia katika Nyimbo Teule za Kisasa za Injili za Kikamba","authors":"Ambrose Ngesa Kang’e, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.6.2.1663","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1663","url":null,"abstract":"Usohalisia ni kipengele muhimu kinachodhihirika katika tungo za kisasa za fasihi. Watunzi wa fasihi ya kisasa hutumia mtindo wa usohalisia kwa namna mbili kuu ambazo ni ujirejelezi wa mtunzi na usohalisia wa kihistografia. Makala haya yamefafanua jinsi usohalisia wa kihistografia ulivyotumika katika nyimbo teule za kisasa za injili za Kikamba. Nyimbo za kisasa za injili za Kikamba zimerejelewa ili kuwakilisha nyimbo za kisasa za injili zilizoimbwa kwa lugha yoyote nchini Kenya. Utanzu wa nyimbo za injili umeteuliwa kwa sababu kutoka miaka ya elfu mbili umedhihirisha mabadiliko si haba ya kuuwasilisha kwa hadhira bali na kuwa utanzu pendwa. Makala haya yametumia mtazamo wa kiusasaleo kuchanganua matini za nyimbo teule za kisasa za injili za Kikamba. Mtazamo wa kiusasaleo hushuku na kupinga mitazamo ya kijadi na kupendekeza mitindo mipya ya kuwasilisha tungo za fasihi ya kisasa. Kutokana na uchanganuzi, iligunduliwa kuwa matumizi ya mtindo wa usohalisia wa kihistografia yalidhihirika kwa namna kadhaa katika nyimbo za injili za kisasa za Kikamba zilizoteuliwa kuchunguzwa. Matumizi ya mtindo wa usohalisia yalidhihirika kupitia utumiaji wa mbinu mbalimbali ambazo zimefafanuliwa na makala haya","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-12-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139149495","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili","authors":"Jemimah Kwamboka Ongwae, Peter Githinji","doi":"10.37284/jammk.6.2.1596","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1596","url":null,"abstract":"Makala haya yalidhamiria kubaini ukiukaji wa baadhi ya kanuni bia za Greenberg katika miundo ya tungo zenye vihusishi vya Kiswahili. Katika utafiti wake, Greenberg (1963), alipendekeza kanuni bia 45 na kutafiti lugha 30 ili kuchunguza mpangilio wa vipashio vya kiisimu katika makundi mbalimbali ya lugha. Lugha ya Kiswahili ilikuwepo mojawapo ya sampuli alizoteua. Hata hivyo, katika kuzingatia uwekaji vihusishi, inaonekana kukiuka baadhi ya kanuni hizo. Kwa hivyo, mkabala wa Greenberg (1963) ulitumika. Kanuni bia za Greenberg hasa zile zinazozungumzia vihusishi pekee zilitumika kuchanganua miundo na mazingira ya kiisimu yanayosababisha ukiukaji wa baadhi ya kanuni za Greenberg katika uwekaji wa vihusishi vya Kiswahili. Data iliyotumika ilikuwa ni tungo zenye vihusishi. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuteua vihusishi hivi na vilikusanywa kwa kusoma vitabu vya sarufi na makala kutoka kwenye majarida na makala ya mtandaoni. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia mkabala wa kanuni bia za Greenberg kupitia ufafanuzi wa data kwa njia ya maelezo na unukuzi wa kanuni bia za Greenberg. Ilijidhihirisha kuwa baadhi ya kanuni bia za Greenberg zina ukiushi katika lugha ya Kiswahili. Ukiushi hasa ulitokea kwa sababu sifa A haikumiliki sifa B kwa kuzingatia sheria ya uchanganuzi iliyopeanwa. Haya yalibainika hasa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inamiliki aina mbili za vihusishi; vihusishi vya kabla ya nomino na vihusishi vya baada ya nomino katika umbo lake la nje. Hata hivyo, baadhi ya kanuni bia zingine zilionyesha utiifu. Aidha baadhi ya kanuni hizi zina utata ambao unaleta changamoto katika juhudi za kutoa kauli jumlishi. Makala haya yatachangia katika kongoo ya utaratibu wa vipashio katika sentensi, taipolojia ya lugha na sintaksia ya Kiswahili","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-25","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139238243","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
David Micheni Mutegi, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi
{"title":"Dhima ya Toponemia kama Utambulisho wa Jamii: mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara Nchini Kenya","authors":"David Micheni Mutegi, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi","doi":"10.37284/jammk.6.2.1581","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1581","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulikuwa wa kionomastiki uliolenga kubainisha dhima ya toponemia za shule za msingi kama utambulisho wa jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na Muthambi Jimboni dogo la Maara. Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini ndizo zilizotumiwa kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala kwa hivyo wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu dhima ya toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Kimuthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia huwa na dhima mbalimbali katika jamii","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139251004","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"Mofolojia Isoshikanisho katika Kiswahili","authors":"Deogratias Ngonyani","doi":"10.37284/jammk.6.2.1580","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1580","url":null,"abstract":"Makala hii inafafanua na kujadili mofolojia isoshikanisho katika Kiswahili na dhana ya mofimu. Baada ya kuelezea sifa bainifu za mofolojia mshikanisho na isoshikanisho, mifano kadha ya mofolojia hiyo katika Kiswahili inafafanuliwa. Mifano hiyo ni katika vionyeshi, uradidi, na ufupishaji wa majina na nomino. Violezo na ruwaza vinaelezwa kuwa muhimu katika fasili ya mofimu katika mofolojia isoshikanisho. Makala inabainisha mofimu za Kiswahili zinaundwa na vipandesauti na violezo. Kwa upande mwingine, violezo hivyo na mifano ya vifupisho vya majina kuwa silabi mbili inabainisha dhima kubwa ya arudhi na katika kuunda maneno ya Kiswahili","PeriodicalId":504864,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":null,"pages":null},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-11-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139254365","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}