{"title":"MABADILIKO YA KIMAANA KATIKA METHALI ZA KIJINSIA: MIFANO KUTOKA JAMII YA WANYANKOLE","authors":"Arinaitwe Annensia, Mosol Kandagor, Magdaline Wafula","doi":"10.58721/jkal.v1i1.94","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.94","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza mabadiliko ya kimaana katika methali za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Lengo kuu la makala hii ni kubaini athari ya mabadiliko katika jamii katika ufasiri wa maana na matumizi ya methali za kijinsia miongoni mwa Wanyankole nchini Uganda. Mbinu za mahojiano zilitumika katika ukusanyaji wa data. Utafiti huu ulihusisha methali kumi na tano za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Uteuzi huo ulifanywa kimaksudi kwa sababu utafiti ulilenga kuchanganua methali zilizohusu jinsia za kike na kiume katika jamii ya Wanyankole. Nadharia ya Udenguzi ilitumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kadri ulimwengu unavyobadilika ndivyo jamii ya Wanyankole inavyobadilika hivyo basi mabadiliko haya yameathiri ufasiri wa maana katika methali za kijinsia za Wanyankole. Vilevile ilibainika kuwa jamii ya jadi inafasiri na kuzitumia baadhi ya methali tofauti na jamii ya kisasa. Makala hii inapendekeza kuwa baadhi ya methali zinafaa kurejelewa upya kiufasiri, kimuundo na kimatumizi ili uamilifu wake uwiane na jamii ya kisasa.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"356 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"122805376","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
{"title":"USOMAJI-HAKIKI: MKAKATI WA UELEKEZAJI WA MBINU ZA UANDISHI KATIKA RIWAYA","authors":"J. N. Maitaria","doi":"10.58721/jkal.v1i1.96","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.96","url":null,"abstract":"Usomaji-hakiki ni mbinu muhimu kwa watunzi-watarajiwa, wanagenzi na watunzi watajika katika ulingo wa utunzi wa riwaya ya Kiswahili. Usomaji huu unaweza kumsaidia mwenye aria ya kutunga na kuwasilisha miswada yao kwa nia ya kuchapishwa. Aidha, usomaji huu unahitaji mkakati wa kujitolea kwa hiari. Ingawa kuna aina mbalmbali za usomaji wa riwaya kuna baadhi ambao ni wa kijumla mno na wenye viwingu vya matatizo. Kwa maana hii, hauwezi kumfunulia kumsaidia msomaji mwenye azma ya kujifunza au kuimarisha zaidi mbinu na taratibu za utunzi wa riwaya kusudiwa. Usomaji-hakiki wa riwaya za Kiswahili unaweza kusaidia katika kuwaelekeza wanagenzi na hata vigogowanaweza kujifunza na kunoa kunga zao za uwasilishaji wa riwaya. Makala hii inajaribu kudokeza namna usomaji-hakiki unavyoweza usomaji wa dhati kwa malengo ya kujenga ari ya kutunga, Kuwasilisha na hatimaye uchapishaji wa miswada ya riwaya ya Kiswahili. Isitoshe, Makala hii itapendekezwa namna usomaji-hakiki unaweza kama mbinu ya usomaji wa tanzu nyingine kifasihi kama hadithi fupi, tamthila na ushairi wa Kiswahili.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"23 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"124633208","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Kenneth Kinyua Thuranira, Jim Ontieri, Nancy Ayodi
{"title":"RUWAZA YA VIVUMISHI KATIKA LUGHA AMBISHI BAINISHI: MIFANO KUTOKA LAHAJA YA KIIMENTI","authors":"Kenneth Kinyua Thuranira, Jim Ontieri, Nancy Ayodi","doi":"10.58721/jkal.v1i1.95","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.95","url":null,"abstract":"Kivumishi ni kipashio muhimu katika lugha yoyote ile. Kinatumika pamoja na kategoria nyingine za maneno katika sentensi ili kufanikisha mawasiliano. Utafiti kuhusu kategoria mbalimbali za maneno umewahi kufanywa. Hata hivyo, hatujakumbana na utafiti unaoangazia ruwaza za kivumishi cha Kiimenti katika tungo za lahaja husika. Hivyo basi nia kuu ya makala haya ni kuthibitisha jinsi kivumishi katika lahaja hii hudhihirisha ruwaza mbalimbali kinapotumika katika sentensi za lahaja hiyo. Data iliyochanganuliwa na kuwasilishwa katika makala haya ilikusanywa maktabani na nyanjani. Maktabani tulirejelea kazi mbalimbali kuhusu ruwaza za vivumishi hasa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Aidha, tulisoma vitabu vya hadithi za Kiimenti ili kupata data ya kuchanganuliwa katika makala haya. Nyanjani tulikusanya data kutoka tarafa ya Abothuguchi ya Magharibi, kaunti ndogo ya Meru katika kaunti ya Meru. Kwa kutumia sampuli maksudi tuliteua miktadha ya mikutano ya kanisa, shule, soko na ile ya chifu ambapo tulikusanya data. Tunatarajia kuwa makala haya yatasaidia katika uandishi wa sarufi ya lahaja ya Kiimenti na pia kuchangia katika uhifadhi wake ili kuendeleza usomi. Kwa sasa lahaja ya Kiimenti haina maandishi mengi na haijatiliwa maanani sana katika mfumo wa elimu nchini Kenya.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"60 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"126568073","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}