Journal of Kiswahili and Other African Languages最新文献

筛选
英文 中文
Viashiria vya Kujiua: Uchunguzi wa Mhusika Kazimoto katika Riwaya ya Kichwamaji Viashiria vya Kujiua:风本木须贺与吉祥寺的联系
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-05-19 DOI: 10.58721/jkal.v2i1.548
Adria Fuluge
{"title":"Viashiria vya Kujiua: Uchunguzi wa Mhusika Kazimoto katika Riwaya ya Kichwamaji","authors":"Adria Fuluge","doi":"10.58721/jkal.v2i1.548","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.548","url":null,"abstract":"Wahusika katika kazi za fasihi huumbwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba tafakuri na fikra za mtunzi kuhusu maisha ya jamii. Katika uumbaji huo, aghalabu, binadamu husawiriwa kama kiumbe anayeteseka na anayeishi katika ulimwengu usiomjali, aliyezungukwa na mateso na ubwege[1], na anayeshindwa kukabiliana vyema na uhalisia wake (Wamitila, 2002). Mambo hayo, ndiyo huweza kusababisha afanye maamuzi fulani kama vile kujiua. Hivi ndivyo anavyofanya Euphrase Kezilahabi katika riwaya ya Kichwamaji (1974) anapomuumba mhusika anayejiua. Hata hivyo, kwa kuwa kujiua huambatana na viashiria mbalimbali, makala haya yanajadili viashiria vya kujiua kwa mhusika mkuu katika riwaya teule tu. Riwaya hiyo imeteuliwa kwa sababu ina mawanda ya kutosha yaliyowezesha kupata data zilizolengwa katika makala haya. Pia, riwaya hiyo imeteuliwa kama sampuli ya kuwakilisha riwaya nyingine zenye viashiria vya kujiua. Misingi ya Nadharia ya Udhanaishi imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Mjadala umebainisha kwamba katika riwaya ya Kichwamaji vipo viashiria vinne vya kujiua vilivyomkumba Kazimoto kabla ya kujiua kwake. Viashiria hivyo ni kukata tamaa, kujitenga kijamii, kuzungumzia masuala ya kujiua na mabadiliko ya tabia. Makala yanahitimisha kwamba jamii inahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu kujiua kwa wahusika pamoja na viashiria vyake ili iweze kumtambua na kumsaidia mtu mwenye viashiria vya kujiua. \u0000  \u0000[1]Mtazamo wa kidhanaishi unaopinga kuwepo kwa maana na ufahamu katika maisha ya binadamu, kutokana na kukata tamaa na kukosa tumaini la kuishi. Kwa mujibu wa Esslin (2001), ubwege ni hali ya kukosa nia ya kufanya jambo fulani na kutengwa katika imani za kidini, tabia za kiungu na mizizi ya akili na mawazo ya mtu. Hii ina maana kwamba ubwege ni kitendo cha kudadisi hali ya binadamu ya kuendelea kuishi ilhali maisha hayana maana tena.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"116 17","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141124262","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Epistemolojia ya Waafrika katika Semi Zilizoandikwa kwenye Vazi la Kanga za Waswahili 从瓦夫里卡语的 "半自力更生 "到瓦西里语的 "语言 "的认识论
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-05-04 DOI: 10.58721/jkal.v2i2.522
Martina Duwe
{"title":"Epistemolojia ya Waafrika katika Semi Zilizoandikwa kwenye Vazi la Kanga za Waswahili","authors":"Martina Duwe","doi":"10.58721/jkal.v2i2.522","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.522","url":null,"abstract":"Epistemolojia ya Waafrika, wakiwamo Waswahili hubainika kupitia sanaa inayobeba mitazamo inayozingatiwa katika jamii yao. Moja kati ya mambo yanayobainisha sanaa ya Waswahili ni vazi la kanga. Kwa jumla, usanaa katika vazi hilo hudhihirika kupitia maumbo au michoro na lugha ya kiufundi ambayo hubeba semi kama vile, mafumbo, methali na misemo. Vazi la kanga huthaminiwa na hutumiwa kwa namna mbalimbali katika maisha ya Waswahili, mathalani, kufunga kiunoni, kichwani, kujifunika na kama pambo (Hanby na Bygott, 1984). Kwa jumla, semi zilizoandikwa kwenye vazi la kanga zimefafanuliwa zaidi katika muktadha wa dhamira na dhima pasipo kumakinikiwa kwa kina katika muktadha wa kiepistemolojia kulingana na kaida za Waswahili wenyewe. Hivyo, makala haya yanafafanua namna semi hizo zinavyobeba na kuhifadhi maarifa ya kiepistemolojia yanayosawiri maisha halisi ya Waswahili. Matokeo haya yaliyopatikana kupitia mbinu ya uchambuzi matini za kanga zinazotumiwa na Waswahili. Vilevile, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika kama mwegamo mkuu katika kuchunguza, kuchanganua na kuwasilisha data husika. Matokeo yanaonesha kuwa maandishi yaliyopo katika vazi la kanga yanahifadhi fasihi ya Waswahili, hususani semi ambazo hubainisha maarifa mbalimbali, yakiwemo ya kiepistemolojia. Hivyo, makala haya yanajadili baadhi ya vipengele hivyo ambavyo ni: maarifa kuhusu kuwapo kwa kani kuu, thamani ya kazi, heshima na utiifu na uvumilivu.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"58 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141013978","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-05-01 DOI: 10.58721/jkal.v2i2.518
H. Jilala
{"title":"Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili","authors":"H. Jilala","doi":"10.58721/jkal.v2i2.518","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.518","url":null,"abstract":"Dhana ya akili unde au akili bandia inarejelea mwigo au ukadiriaji wa akili ya binadamu katika mashine. Lengo la akili unde ni pamoja na matumizi ya kompyuta yaliyoboreshwa kuhoji na kutambua mambo anuwai unde na ya tasnia mbalimbali (Jurafsky na Martin, 2020). Makala hii inalenga kutathmini matumizi ya akili unde kama nyenzo ya kutafsiri matini za Kiingereza kwenda Kiswahili. Data ya makala hii imekusanywa maktabani kwa kupitia maandiko na pia uwandani kwa kuwahoji wanataaluma mbalimbali. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya makala hii umeongozwa na Mkabala wa Uchambuzi wa Maudhui ya Krippendorff (2004). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa akili unde ina ubora kwa vile hufanya kazi kwa kasi, gharama ni nafuu, urahisi, kutafsiri lugha nyingi na unyumbufu wa kuunganishwa na teknolojia nyingine. Kwa upande mwingine makala hii imebainisha udhaifu wa matumizi ya akili unde kama vile kutozingatia muktadha, kukosa ubunifu, tofauti za kiisimu, kukosa usalama na upinzani wa wanaisimu. Kutokana na udhaifu huo, Makala hii inapendekeza kuwa uwekwe uangalizi wa binadamu katika mifumo, kushughulikia utata, kuboresha mifumo kila muda, kuwekwe sehemu ya maoni ya mtumiaji na matumizi ya mbinu msetu. Hivyo, ni muhimu kuweka usawa kati ya ufanisi wa mashine na uelewa wa watafsiri wa kibinadamu katika uendelezaji na utekelezaji wa akili unde katika tafsiri.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"21 7","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-05-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"141044719","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Mtazamo wa Ki-Afrika katika Nadharia za Tafsiri 关于非洲土著人与塔夫西里土著人的讨论
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-04-14 DOI: 10.58721/jkal.v2i1.491
H. Jilala
{"title":"Mtazamo wa Ki-Afrika katika Nadharia za Tafsiri","authors":"H. Jilala","doi":"10.58721/jkal.v2i1.491","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.491","url":null,"abstract":"Makala haya yanahusu Mtazamo wa Ki-Afrika katika Nadharia za Tafsiri. Inafahamika kuwa chimbuko la nadharia za tafsiri zilizopo ni nchi za Kimagharibi. Hata hivyo,  katika nchi za Afrika taaluma ya tafsiri imepiga hatua kubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwa na wataalamu na wanataaluma wengi wa tafsiri, kufundishwa katika shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Pamoja na maendeleo hayo, mpaka sasa hakuna nadharia ya tafsiri iliyobuliwa kupitia mazingira, muktadha na utamaduni wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya Ki-Afrika. Hivyo, makala haya yanalenga kujadili umuhimu wa kuunda nadharia za tafsiri kwa kutumia muktadha wa lugha za Ki-Afrika na kupendekeza hatua zitakazochukuliwa katika mchakato wa kuunda nadharia za tafsiri za Kiswahili. Makala yanajadili kwamba, pamoja na kuwapo kwa nadharia zilizoibuliwa na wanazuoni wa Kimagharibi, kuna umuhimu wa kuunda nadharia za tafsiri ambazo zimefungamana na muktadha, mazingira, mila, desturi, historia, lugha na utamaduni wa Ki-Afrika. Hii ni kwa sababu tafsiri hushughulika na lugha ambayo ni mali ya jamii yenye utamaduni mahususi. Hivyo, nadharia za tafsiri zilizofumbata mtazamo wa Ki-Afrika zitakuwa msingi, dira na mwongozo wa kinadharia na kivitendo katika kushughulikia tafsiri za matini mbalimbali za lugha za Ki-Afrika, hasa zinazohusu dhana za kiutamaduni na fasihi. Vilevile nadharia hizo zitakuwa ni suluhisho la matatizo na changamoto za tafsiri kiisimu, kisemantiki, kiutamaduni na kifasihi. Makala haya yanapendekeza kuwa nadharia za tafsiri zinaweza kuundwa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kuunda nadharia mpya, kuasili nadharia zilizopo na kuziboresha nadharia hizo.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"136 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-04-14","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140706671","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-01-28 DOI: 10.58721/jkal.v2i1.410
Dinah Sungu Osango, M. Mbatiah, Rayya Timammy
{"title":"Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili","authors":"Dinah Sungu Osango, M. Mbatiah, Rayya Timammy","doi":"10.58721/jkal.v2i1.410","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.410","url":null,"abstract":"Makala haya yanachunguza ngazi ya utambuzi na uamilifu wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa makusudi kwa uchunguzi huu.  Riwaya hizo ni; Nyuso za Mwanamke (S. Mohamed, 2010), Harufu ya Mapera (K. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F. Kagwa, 2018), Haini (A. Shafi, 2002), na Ndoto ya Almasi (K. Walibora, 2006). Ngazi ya utambuzi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi zilizopendekezwa na wananaratolojia. Kimsingi, ufokasi ni mtazamo ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi kwa ujumla. Data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala wetu imetolewa katika riwaya teule.  Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi za ufokasi na wakati huo huo kudhihirisha uamilifu wa ngazi hizo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na kuongozwa na madai ya teneti za kimsingi za nadharia ya naratolojia ambayo inatambua ufokasi na uhusika kama vipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"405 28","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140490453","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010)
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-01-27 DOI: 10.58721/jkal.v2i1.409
Mary Njambi Muigai, I. Mwamzandi, Robert Oduori
{"title":"Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010)","authors":"Mary Njambi Muigai, I. Mwamzandi, Robert Oduori","doi":"10.58721/jkal.v2i1.409","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.409","url":null,"abstract":"Makala haya yanachunguza matumizi ya uchopekaji wa vipande vya simulizi katika riwaya mbili za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa ambayo hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za binadamu, au simulizi kuu. Uchanganuzi umedhihirisha kuwa mwandishi wa riwaya hizi alitumia kimakusudi vipengele vya kibaadausasa ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya hizi zilitumia uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga urazini, mshikamano, na muumano wa usimulizi wa riwaya za kimapokeo. Kimaudhui, riwaya hizi zinasaili mwelekeo chanya uliohusishwa na uhuru. Zinaonyesha kuwa mataifa mengi ya Afrika yametawaliwa na hali ya utamauishi baada ya uhuru. Vilevile, misaada inayotolewa na mataifa ya ulaya hutumika kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo katika mataifa ya Afrika. Hali kadhalika, riwaya hizi zinaonyesha changamoto ambazo wahamiaji hupitia wanapohamia ughaibuni kutafuta maisha bora. Ni bayana kuwa mwandishi wa riwaya hizi ametumia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa kama mbinu ya kiumbuji inayokaidi uandishi wa kimapokeo. Vilevile, riwaya hizi zimetumika kudhihirisha fujo, ghasia, na ukosefu wa mshikamano katika ulimwengu wa karne ya ishirini na moja.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"167 6","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"140492581","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Hali ya Lugha ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu nchini Tanzania: Mifano kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Hali ya Lugha ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu nchini Tanzania:Mifano kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2024-01-08 DOI: 10.58721/jkal.v1i2.394
Sauda Uba Juma, Editha Adolph
{"title":"Hali ya Lugha ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu nchini Tanzania: Mifano kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere","authors":"Sauda Uba Juma, Editha Adolph","doi":"10.58721/jkal.v1i2.394","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i2.394","url":null,"abstract":"Watafiti wa makaka hii wanaangazia hali ya lugha ya Kiswahili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA[1] kuanzia sasa). Azma ya uchunguzi huo ni kutaka kubaini endapo lugha ya Kiswahili inapewa nafasi stahiki katika Chuo hicho au la. Hii inatokana na ukweli kwamba kuna baadhi ya taasisi ambazo zinaithamini sana lugha ya Kiswahili na kuipa nafasi sawa na lugha nyingine za kigeni. Hata hivyo, zipo baadhi ya taasisi ambazo zinaibeza lugha hii na kuiona kama kwamba haina nafasi yoyote kitaaluma na kimawasiliano. Data ya makala hii imekusanywa kupitia njia tatu: upitiaji wa nyaraka mbalimbali kutoka maktabani, usaili na ushuhudiaji. Hivyo, njia zote hizo kwa pamoja zimetusaidia kupata data faafu na ya kutosha kulingana na malengo ya makala hii. Vilevile, uchambuzi wa data katika utafiti huu, umetumia mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu za kimaelezo na kiufafanuzi zimetumika katika kudadavua vipengele mbalimbali ambavyo vimebainishwa. Sanjari na mkabala huo, tumetumia pia mkabala wa kitakwimu ambao kimsingi umejikita katika uchambuzi wa data kwa kutumia namba. Mkabala huu ulitumika pale tu ilipobidi kufanya hivyo ili kuonesha idadi ya baadhi ya vipengele vilivyokuwa na uhitaji huo. Aidha, matokeo yameonesha kwamba, kuna mabadiliko na mafanikio makubwa MNMA katika kuikuza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili, tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Tunadiriki kusema hivyo kwa kuwa tumebaini juhudi lukuki za makusudi zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa kwa minajili ya kuikuza na kuiendeleza lugha hii ya Kiswahili. \u0000  \u0000[1] The Mwalimu Nyerere Memorial Academy.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"9 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2024-01-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"139445287","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Kufanana na Kutofautiana kwa Msamiati katika Lahaja za Lugha ya Kihaya: Mifano kutoka Kihamba na Kiziba
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2023-06-07 DOI: 10.58721/jkal.v1i2.231
Editha Adolph
{"title":"Kufanana na Kutofautiana kwa Msamiati katika Lahaja za Lugha ya Kihaya: Mifano kutoka Kihamba na Kiziba","authors":"Editha Adolph","doi":"10.58721/jkal.v1i2.231","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i2.231","url":null,"abstract":"Makala hii inafafanua dhana za kufanana na kutofautiana kwa msamiati wa lahaja ya Kihamba na Kiziba katika lugha ya Kihaya. Vipengele vinavyohusika katika kuchunguza kufanana na kutofautiana huko ni vipengele vya tahajia na matamshi. Lengo la ulinganishi na ulinganuzi huo ni kubainisha ikiwa kuna ufanano na utofauti wa kimsamiati unaojitokeza katika lahaja hizi mbili za lugha ya Kihaya yaani Kihamba na Kiziba. Kwa mujibu wa makala hii, eneo hili halijapewa aula na hivyo kumpa mtafiti laghba ya kulishughulikia. Data ya makala hii imekusanywa uwandani katika eneo la Kyamutwala inakozungumzwa lahaja ya Kihamba. Kwa upande wa Kyamutwala, mtafiti amekusanya data katika kata za Kamachumu, Ibuga, Muhutwe na Izigo. Katika eneo la Kiziba data imekusanywa kutoka kata za Buyango, Bugandika, Ruzinga na Bwanjai inakozungumzwa lahaja ya Kiziba. Data hii ya uwandani imepatikana kwa mbinu ya ushuhudiaji, hojaji, usaili na uchanganuzi wa matini za maktabani. Mtafiti alishuhudia namna mbalimbali za kitahajia/hijai na kimatamshi kuhusiana na msamiati wa Kihaya katika lahaja ya Kihamba na Kiziba. Aidha, data ilikusanywa kupitia hojaji ambapo watafitiwa 80 waligawiwa dodoso na kuzijaza kikamilifu. Kupitia mbinu ya usaili, mtafiti alifanya mahojiano ya ana kwa ana na watafitiwa wa makala hii na kuweza kubaini ulinganifu na usiganifu uliopo baina ya msamiati wa lahaja zinazoshughulikiwa katika makala hii. Data ya maktabani ilipatikana kwa mapitio ya matini mbalimbali zinazohusiana na mada inayoshughulikiwa katika makala hii. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba baadhi ya msamiati wa Kihamba na Kiziba hurandana na baadhi husigana. Pia zimetolewa sababau za kufanana na kutofautiana kwa msamiati wa lahaja hizo. Mtafiti wa makala hii anapendekeza tafiti fuatizi zifafanue kwa kina sababu za kutofautiana na kufanana kwa msamiati wa lahaja hizi tofauti na ilivyoelezewa katika makala hii kwani sababu ni nyingi. Aidha, makala hii itatoa hamasa kwa watafiti kufanya tafiti juu ya lahaja za lugha mbalimbali. Vilevile, makala hii inatoa mchango katika kukuza na kuendeleza lugha za Kibantu na taaluma ya isimu kwa ujumla. Pia itaongeza marejeleo faafu kwa watafiti wa isimu.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2023-06-07","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"128703453","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2022-11-28 DOI: 10.58721/jkal.v1i1.93
G. A. Kasiga
{"title":"UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA","authors":"G. A. Kasiga","doi":"10.58721/jkal.v1i1.93","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.93","url":null,"abstract":"Imebainika kuwa tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022). Athari zake zimebainika katika vipengele kadhaa vya kibunifu (Kasiga, 2021). Pia, misukumo mbalimbali inayowasukuma wasanii kutumia U-Nigeria imebainishwa (Kasiga, 2022). Kimsingi, hali hii inatishia utambulisho wa Kitanzania katika sanaa. Hivyo, makala hii imetoa mapendekezo ya kiuboreshaji dhidi ya U-Nigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Mapendekezo yalitolewa yamehusisha kufanyika uwekezaji wa muziki wa asili wa Kitanzania, kufanyika kwa usimamizi maalumu katika vyombo vya habari, kuwepo kwa sheria na kanuni za kulinda uasili wa muziki wa kizazi kipya, na uanizhwaji wa semina, warsha pamoja na madarasa maalumu kwa wasanii. Pia, makala imependekeza kuwepo kwa agenda mahususi ya kitaifa kujenga uzalendo, kumakinikia mitindo ya sanaa za Kitanzania katika utengenezaji wa muziki, kuharakisha upatikanaji wa vazi la taifa, kuanzishwa kwa vipindi vya uchambuzi wa nyimbo, na wasanii kushawishiwa kutumia mandhari ya Kitanzania katika video zao. Vilevile, imependekezwa kuanzishwa kwa matamasha na tuzo za muziki, asasi za elimu kutengeneza mitaala ya biashara, lugha ya Kiswahili, na utamaduni wa Kitanzania, na kuwe na muumano kati ya biashara, utamaduni na teknolojia.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"32 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"122213939","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
VYANZO VYA MISIMU KWA WANAFUNZI KATIKA KISWAHILI
Journal of Kiswahili and Other African Languages Pub Date : 2022-11-28 DOI: 10.58721/jkal.v1i1.92
Editha Adolph
{"title":"VYANZO VYA MISIMU KWA WANAFUNZI KATIKA KISWAHILI","authors":"Editha Adolph","doi":"10.58721/jkal.v1i1.92","DOIUrl":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.92","url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza vyanzo vya misimu kwa wanafunzi katika Kiswahili. Mtafiti ametumia mbinu za hojaji, usaili na uchambuzi wa matini. Mtafiti aligawa hojaji 15 kwa wanachuo 15 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Chuo hiki kinapatikana katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania. Aidha, mtafiti alisoma nyaraka zinazohusiana na mada husika kama vile: majarida na tasinifu. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972). Data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Matokeo ya makala hii yamebainisha kuwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kutumia msamiati sanifu pia hutumia misimu kutoka katika nyanja tofautitofauti katika mawasiliano yao ya kila siku. Mtafiti amechunguza misimu inayotokana na uwanja wa sanaa, siasa na michezo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha misimu mbalimbali inayotumiwa na wanachuo wa chuo husika. Pia misimu tofautitofauti inayohusiana na nyanja za utani, soka na sanaa. Hii itatoa msukumo kwa wasanifishaji wa lugha ya Kiswahili kusanifisha misimu husika. Makala inapendekeza kuwa watafiti wa lugha wachunguze misimu inayotokana na mitandao ya kijamii, aina mbalimbali za misimu, misimu inayotumika katika maeneo mbalimbali kama vile shuleni, vijiweni, hospitalini na maofini.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"51 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"116353078","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
相关产品
×
本文献相关产品
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信