{"title":"Uamilifu wa Kipragmatiki wa Kirai Nomino (KN) Katika Kiswahili","authors":"Chege Joel Ngari","doi":"10.37284/jammk.5.1.853","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yalitalii uamilifu wa kipragmatiki wa kirai nomino katika sintaksia ya Kiswahili. Pragmatiki hujihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na hali halisi ya mawasiliano. Hivyo basi, pragmatiki ni taaluma inayochunguza maana kulingana na muktadha fulani. Miongoni mwa maana za kimuktadha zilizoshughulikiwa ni pamoja na: maana dhanishi, maana tagusanishi na maana matinishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyopendekezwa na Halliday. Umuhimu wake ni kwamba inaeleza jinsi lugha inavyotumika katika hali halisi ya mawasiliano. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni mahojiano na uchunzaji. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu hizi zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikisawazisha mapungufu ya nyingine. Data ya maktabani ilitumika kuweka misingi ya ukusanyaji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kwa maswali ya mahojiano. Data katika makala haya ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na maelezo. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Makala haya yaliweka bayana namna kirai nomino kinavyoweza kutumika kufumba ujumbe kipragmatiki katika mawasiliano. Makala haya yanatoa nafasi ya kupigiwa mfano ya kuchangia katika taaluma ya pragmatiki na isimu kwa jumla.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"56 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-09-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.853","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala haya yalitalii uamilifu wa kipragmatiki wa kirai nomino katika sintaksia ya Kiswahili. Pragmatiki hujihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na hali halisi ya mawasiliano. Hivyo basi, pragmatiki ni taaluma inayochunguza maana kulingana na muktadha fulani. Miongoni mwa maana za kimuktadha zilizoshughulikiwa ni pamoja na: maana dhanishi, maana tagusanishi na maana matinishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyopendekezwa na Halliday. Umuhimu wake ni kwamba inaeleza jinsi lugha inavyotumika katika hali halisi ya mawasiliano. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni mahojiano na uchunzaji. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu hizi zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikisawazisha mapungufu ya nyingine. Data ya maktabani ilitumika kuweka misingi ya ukusanyaji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kwa maswali ya mahojiano. Data katika makala haya ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na maelezo. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Makala haya yaliweka bayana namna kirai nomino kinavyoweza kutumika kufumba ujumbe kipragmatiki katika mawasiliano. Makala haya yanatoa nafasi ya kupigiwa mfano ya kuchangia katika taaluma ya pragmatiki na isimu kwa jumla.