Aina za Uongozi wa Kisiasa katika Riwaya za Kiswahili: Uchambuzi Linganishi wa Kusadikika na Rais Anampenda Mke Wangu

Daniel Kotey, Felix Kwame Sosoo
{"title":"Aina za Uongozi wa Kisiasa katika Riwaya za Kiswahili: Uchambuzi Linganishi wa Kusadikika na Rais Anampenda Mke Wangu","authors":"Daniel Kotey, Felix Kwame Sosoo","doi":"10.56279/jk.v85i1.5","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala hii inahusu uongozi wa kisiasa katika riwaya za Kiswahili. Riwaya zilizochaguliwa ni Kusadikika (1952), na Rais Anampenda Mke Wangu (2003). Hali ya uongozi wa kisiasa kabla ya uhuru inaelezwa kuwa ni tofauti na hali ya baada ya uhuru. Hii inamaanisha kwamba uongozi wa kisiasa kabla ya uhuru inawezekana kuwa tofauti na uongozi wa kisiasa baada ya uhuru. Kwa upande mwingine, inaelezwa kwamba hali ya uongozi haijabadilika toka kabla ya uhuru mpaka baada ya uhuru. Lengo la makala hii ni kubainisha aina za uongozi wa kisiasa zinazosawiriwa katika riwaya teule. Hii ni kwa sababu fasihi ni zao la jamii inayozungumza masuala mbalimbali ya jamii. Aidha, katika uandishi wa kazi za fasihi waandishi huakisi yale yanayotokea katika jamii ikiwamo suala la kisiasa. Ikiwa kulikuwa na tofauti au tofauti hizo hazikuwapo, je, ni kwa namna gani waandishi wa fasihi ya Kiswahili wameuonesha uongozi wa kisiasa katika vipindi tofauti. Hili ni wazo la msingi lililotuchochea kujadili suala la uongozi wa kisiasa katika riwaya teule. Aidha, riwaya hizi zilichapishwa katika vipindi mahususi vya uongozi, yaani kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Uchunguzi huu ulijikita katika aina za uongozi wa kisiasa zilizoshughulikiwa na waandishi katika riwaya teule. Nadharia ya Ubaadaukoloni iliyoasisiwa na Edward Said mwaka 1978 imetumika katika uchambuzi wa data. Msingi wake unaeleza kuwa uhusiano kati ya jamii mbili, yaani watawaliwa na watawala ulianzisha jamii ya ubaadaukoloni na historia inaeleza vizuri kuhusu jamii hizi. Tuliongozwa na msingi huu kubainisha aina za uongozi wa kisiasa katika riwaya teule ambazo ni uongozi wa kisiasa wa kijadi na uongozi wa kisiasa wa kisasa.","PeriodicalId":411809,"journal":{"name":"Jarida la Kiswahili","volume":"7 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-06-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"Jarida la Kiswahili","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.56279/jk.v85i1.5","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0

Abstract

Makala hii inahusu uongozi wa kisiasa katika riwaya za Kiswahili. Riwaya zilizochaguliwa ni Kusadikika (1952), na Rais Anampenda Mke Wangu (2003). Hali ya uongozi wa kisiasa kabla ya uhuru inaelezwa kuwa ni tofauti na hali ya baada ya uhuru. Hii inamaanisha kwamba uongozi wa kisiasa kabla ya uhuru inawezekana kuwa tofauti na uongozi wa kisiasa baada ya uhuru. Kwa upande mwingine, inaelezwa kwamba hali ya uongozi haijabadilika toka kabla ya uhuru mpaka baada ya uhuru. Lengo la makala hii ni kubainisha aina za uongozi wa kisiasa zinazosawiriwa katika riwaya teule. Hii ni kwa sababu fasihi ni zao la jamii inayozungumza masuala mbalimbali ya jamii. Aidha, katika uandishi wa kazi za fasihi waandishi huakisi yale yanayotokea katika jamii ikiwamo suala la kisiasa. Ikiwa kulikuwa na tofauti au tofauti hizo hazikuwapo, je, ni kwa namna gani waandishi wa fasihi ya Kiswahili wameuonesha uongozi wa kisiasa katika vipindi tofauti. Hili ni wazo la msingi lililotuchochea kujadili suala la uongozi wa kisiasa katika riwaya teule. Aidha, riwaya hizi zilichapishwa katika vipindi mahususi vya uongozi, yaani kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Uchunguzi huu ulijikita katika aina za uongozi wa kisiasa zilizoshughulikiwa na waandishi katika riwaya teule. Nadharia ya Ubaadaukoloni iliyoasisiwa na Edward Said mwaka 1978 imetumika katika uchambuzi wa data. Msingi wake unaeleza kuwa uhusiano kati ya jamii mbili, yaani watawaliwa na watawala ulianzisha jamii ya ubaadaukoloni na historia inaeleza vizuri kuhusu jamii hizi. Tuliongozwa na msingi huu kubainisha aina za uongozi wa kisiasa katika riwaya teule ambazo ni uongozi wa kisiasa wa kijadi na uongozi wa kisiasa wa kisasa.
求助全文
约1分钟内获得全文 求助全文
来源期刊
自引率
0.00%
发文量
0
×
引用
GB/T 7714-2015
复制
MLA
复制
APA
复制
导出至
BibTeX EndNote RefMan NoteFirst NoteExpress
×
提示
您的信息不完整,为了账户安全,请先补充。
现在去补充
×
提示
您因"违规操作"
具体请查看互助需知
我知道了
×
提示
确定
请完成安全验证×
copy
已复制链接
快去分享给好友吧!
我知道了
右上角分享
点击右上角分享
0
联系我们:info@booksci.cn Book学术提供免费学术资源搜索服务,方便国内外学者检索中英文文献。致力于提供最便捷和优质的服务体验。 Copyright © 2023 布克学术 All rights reserved.
京ICP备2023020795号-1
ghs 京公网安备 11010802042870号
Book学术文献互助
Book学术文献互助群
群 号:481959085
Book学术官方微信