Asca Monica Koko, Juliet Akinyi Jagero, N. N. Musembi
{"title":"Matamko Tendi na Athari Zake kwa Wahusika katika Riwaya za Ken Walibora","authors":"Asca Monica Koko, Juliet Akinyi Jagero, N. N. Musembi","doi":"10.37284/jammk.5.1.799","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Matamko tendi (MT) ni vitendo vinavyotekelezwa kwa kuvitamka tu kwa sauti. Katika matamko tendi msemaji huwa ametenda kupitia kuzungumza. Riwaya inatarajiwa kuwa na usimulizi hata hivyo dayolojia huweza kutokea katika riwaya. Kutokana na hayo, makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Makala hii inalenga kuchanganua matamko tendi na athari zake katika riwaya za Walibora. Makala iliongozwa na Nadharia ya Vitendo usemi. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya nne za Walibora huku sampuli dabwadabwa ikitumika kuteua MT kutoka riwaya hizo. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kudondoa sehemu za matini na kuwekwa kwenye jedwali la matukio. Data zilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo kulingana na madhumuni ya makala na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Makala ilionyesha kwamba wahusika waliathiriwa na matamko kwa njia chanya hasa matamko ya furaha na kujenga mahusiano katika jamii. Uchanganuzi wa MT una umuhimu katika usomaji, uchanganuzi na ufasiriaji wa mazungumzo ya wahusika na maana anayonuia mwandishi wa Riwaya.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"29 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-08-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.799","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Matamko tendi (MT) ni vitendo vinavyotekelezwa kwa kuvitamka tu kwa sauti. Katika matamko tendi msemaji huwa ametenda kupitia kuzungumza. Riwaya inatarajiwa kuwa na usimulizi hata hivyo dayolojia huweza kutokea katika riwaya. Kutokana na hayo, makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Makala hii inalenga kuchanganua matamko tendi na athari zake katika riwaya za Walibora. Makala iliongozwa na Nadharia ya Vitendo usemi. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya nne za Walibora huku sampuli dabwadabwa ikitumika kuteua MT kutoka riwaya hizo. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kudondoa sehemu za matini na kuwekwa kwenye jedwali la matukio. Data zilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo kulingana na madhumuni ya makala na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Makala ilionyesha kwamba wahusika waliathiriwa na matamko kwa njia chanya hasa matamko ya furaha na kujenga mahusiano katika jamii. Uchanganuzi wa MT una umuhimu katika usomaji, uchanganuzi na ufasiriaji wa mazungumzo ya wahusika na maana anayonuia mwandishi wa Riwaya.