{"title":"Utathmini wa Ujenzi wa Motifu ya Mgogoro wa Ardhi Kupitia Wahusika: Mfano Kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni","authors":"Mercy Karimi Nthia, O. Ntiba","doi":"10.37284/jammk.5.2.1019","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Suala la ardhi limekuwa nyeti tangu jadi. Wahusika hutumiwa na wasanii kubainisha suala hili. Tafiti za awali zilijikita katika motifu ya safari, siri na maisha ya dunia. Hata hivyo, hakuna utafiti umefanywa kutathmini ujenzi wa motifu ya mgogoro wa ardhi kupitia wahusika. Makala hii imelenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kutathmini ujenzi wa motifu ya suala la mgogoro wa ardhi kupitia wahusika; mfano kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni. Motifu hii ni kurudiwarudiwa kwa suala la mgogoro wa ardhi baina ya wahusika katika matini teule. Makala hii iliongozwa na nadharia mbili; Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa na Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi. Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa iliwaongoza watafiti kuweza kubainisha suala la ardhi kama lilivyoangaziwa na waandishi katika uhalisia wake. Hata hivyo, nadharia hii ilipungukiwa kubainisha jinsi matabaka katika jamii huendeleza suala la ardhi. Nadharia iliyofidia pengo hili ni Sosholojia ya Fasihi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo matini teule ziliteuliwa kimaksudi. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ya makala hii ni kuwa motifu ya mgogoro wa ardhi imekuzwa kupitia kwa wahusika antagonisti, protagonisti, tuli na bui. Kwa hivyo, utachangia katika uhakiki wa kazi za baadaye za nathari za fasihi ya Kiswahili. Aidha, walimu na wanafunzi wataelewa namna wahusika hujengwa. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadaye zifanywe kutathmini motifu ya wahusika katika sekta ya uchumi na siasa.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"282 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-12-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1019","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Suala la ardhi limekuwa nyeti tangu jadi. Wahusika hutumiwa na wasanii kubainisha suala hili. Tafiti za awali zilijikita katika motifu ya safari, siri na maisha ya dunia. Hata hivyo, hakuna utafiti umefanywa kutathmini ujenzi wa motifu ya mgogoro wa ardhi kupitia wahusika. Makala hii imelenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kutathmini ujenzi wa motifu ya suala la mgogoro wa ardhi kupitia wahusika; mfano kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni. Motifu hii ni kurudiwarudiwa kwa suala la mgogoro wa ardhi baina ya wahusika katika matini teule. Makala hii iliongozwa na nadharia mbili; Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa na Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi. Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa iliwaongoza watafiti kuweza kubainisha suala la ardhi kama lilivyoangaziwa na waandishi katika uhalisia wake. Hata hivyo, nadharia hii ilipungukiwa kubainisha jinsi matabaka katika jamii huendeleza suala la ardhi. Nadharia iliyofidia pengo hili ni Sosholojia ya Fasihi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo matini teule ziliteuliwa kimaksudi. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ya makala hii ni kuwa motifu ya mgogoro wa ardhi imekuzwa kupitia kwa wahusika antagonisti, protagonisti, tuli na bui. Kwa hivyo, utachangia katika uhakiki wa kazi za baadaye za nathari za fasihi ya Kiswahili. Aidha, walimu na wanafunzi wataelewa namna wahusika hujengwa. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadaye zifanywe kutathmini motifu ya wahusika katika sekta ya uchumi na siasa.