Beatrice Nyambura Njeru, John M. Kobia, Allan Mugambi
{"title":"Wahusika na Motifu ya Siri katika Nathari Teule za Fasihi za Kiswahili","authors":"Beatrice Nyambura Njeru, John M. Kobia, Allan Mugambi","doi":"10.37284/jammk.5.1.782","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Wahusika ni viumbe muhimu katika ujenzi wa kazi ya fasihi. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu. Ni picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vipya, dhamira na mada katika fasihi. Kwa hivyo, wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuni. Mwandishi huchora viumbe anaowatwika majukumu ya kutenda na kusema kama binadamu na kupitia kwao huwasilisha dhamira yake. Dhamira hii hukuzwa na kuwepo kwa masuala makuu ambayo huwasilishwa kwa hadhira lengwa na kufanikisha lengo kuu la utunzi wa kazi ya fasihi. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ambavyo wahusika huingiliana kutoka kwa matini moja hadi nyingine katika nathari teule za fasihi ya Kiswahili. Mwingilianomatini hubainisha kuwa matini moja inaweza kuhusiana na matini nyingine katika viwango mbalimbali kama vile usawiri wa wahusika, usawiri wa mandhari, maudhui na mtindo wa uandishi. Sampuli maksudi ilitumika kuteua vitabu saba kwa msingi kuwa vina dhana ya siri katika uteuzi wa mada. Vitabu hivi ambavyo ni Nataka Iwe Siri, Sitaki Iwe Siri, Siri Ya Baba Yangu Kitabu 1, Siri Ya Baba Yangu 2, Siri Sirini 1, Siri Sirini 2 na Siri Sirini 3 vimedhihirisha kuwa kuna siri ambazo zimejengwa na wahusika katika bunilizi teule na kufanikisha motifu ya siri. Uchanganuzi na uwasilishwaji wa data itakayopatikana kutokana na usomaji wa kazi teule utakuwa wa kimaelezo. Makala haya yatawafaa wahakiki kwa kuwapa mwanga wa namna ya kuhakiki kazi zinazohusiana na siri na kuchunguza namna wahusika wanavyoweza kuingiliana kwa namna tofauti na kufanikisha ujenzi wa motifu ya siri. Aidha walimu na wanafunzi wa viwango vyote watafaidika kwa sababu wataelewa kazi teule zaidi. Waandishi nao watafaidika kutokana na makala haya kwa sababu watayatumia kama kifaa cha kutunga kazi za baadaye za kiwango cha juu zaidi kuhusiana na motifu ya siri. Vilevile makala haya yatatoa mchango mkubwa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuwa yataongeza maarifa mapya kuhusu namna wahusika wanaweza kuingiliana na kukuza kazi za kibunilizi zilizo na motifu mbalimbali.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"2 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-08-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.782","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Wahusika ni viumbe muhimu katika ujenzi wa kazi ya fasihi. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu. Ni picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vipya, dhamira na mada katika fasihi. Kwa hivyo, wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuni. Mwandishi huchora viumbe anaowatwika majukumu ya kutenda na kusema kama binadamu na kupitia kwao huwasilisha dhamira yake. Dhamira hii hukuzwa na kuwepo kwa masuala makuu ambayo huwasilishwa kwa hadhira lengwa na kufanikisha lengo kuu la utunzi wa kazi ya fasihi. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ambavyo wahusika huingiliana kutoka kwa matini moja hadi nyingine katika nathari teule za fasihi ya Kiswahili. Mwingilianomatini hubainisha kuwa matini moja inaweza kuhusiana na matini nyingine katika viwango mbalimbali kama vile usawiri wa wahusika, usawiri wa mandhari, maudhui na mtindo wa uandishi. Sampuli maksudi ilitumika kuteua vitabu saba kwa msingi kuwa vina dhana ya siri katika uteuzi wa mada. Vitabu hivi ambavyo ni Nataka Iwe Siri, Sitaki Iwe Siri, Siri Ya Baba Yangu Kitabu 1, Siri Ya Baba Yangu 2, Siri Sirini 1, Siri Sirini 2 na Siri Sirini 3 vimedhihirisha kuwa kuna siri ambazo zimejengwa na wahusika katika bunilizi teule na kufanikisha motifu ya siri. Uchanganuzi na uwasilishwaji wa data itakayopatikana kutokana na usomaji wa kazi teule utakuwa wa kimaelezo. Makala haya yatawafaa wahakiki kwa kuwapa mwanga wa namna ya kuhakiki kazi zinazohusiana na siri na kuchunguza namna wahusika wanavyoweza kuingiliana kwa namna tofauti na kufanikisha ujenzi wa motifu ya siri. Aidha walimu na wanafunzi wa viwango vyote watafaidika kwa sababu wataelewa kazi teule zaidi. Waandishi nao watafaidika kutokana na makala haya kwa sababu watayatumia kama kifaa cha kutunga kazi za baadaye za kiwango cha juu zaidi kuhusiana na motifu ya siri. Vilevile makala haya yatatoa mchango mkubwa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuwa yataongeza maarifa mapya kuhusu namna wahusika wanaweza kuingiliana na kukuza kazi za kibunilizi zilizo na motifu mbalimbali.