Eliud Miriti Josphat, N. Gitonga, Dorcas M. Musyimi
{"title":"Maudhui Katika Nyimbo za Tohara Zilizodenguliwa na Nyimbo za Dini za Kiigembe katika Kuafikia Maendeleo Endelevu kwa Waigembe","authors":"Eliud Miriti Josphat, N. Gitonga, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.813","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Waigembe wana utamaduni ambao unafungamana na nyimbo ambazo zinaimbwa katika hafla tofauti tofauti. Nyimbo za tohara pamoja na nyimbo za kidini za Kikristo ni baadhi ya zile zinaimbwa. Nyimbo za tohara zinaimbwa wakati wa kutahiri wavulana na za kidini wakati wa shughuli za kidini ya Kikristo. Hata hivyo, hatua ya waimbaji wa nyimbo za dini ya Kikristo kubadilisha nyimbo za tohara kimaudhui, kimtindo na kiutendakazi ili kuzitumia upya katika mazingira ya kidini ili kusaidia katika maenezi ya injili ya Kikristo kwa wengi na kutumika katika hafla zingine za kijamii kando na tohara ni jambo ambalo ni mpya katika jamii ya Waigembe. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti udenguzi wa nyimbo za tohara za Waigembe na nyimbo za dini ya Kikristo ili kuweza kutumika katika hafla tofauti kando na tohara. Makala haya yalilenga kubainisha maudhui ambayo nyimbo za tohara zilizodenguliwa na nyimbo za dini ya Kikristo huwa nayo katika jamii ya Waigembe. Watafiti waliongozwa na nadharia ya udenguzi. Data ya nyimbo kumi na nane imetumika katika makala haya. Awamu tatu ambazo nyimbo hizo hufuata zilichanganuliwa na kuwasilisha maudhui kwa njia ya maelezo. Makala haya yanachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu nyimbo zilizodenguliwa za tohara za Kiigembe, pamoja na kuhifadhi fasihi simulizi ya Kiafrika ili itumike na vizazi vijavyo katika kuafikia maendeleo endelevu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"26 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-08-25","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.813","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Waigembe wana utamaduni ambao unafungamana na nyimbo ambazo zinaimbwa katika hafla tofauti tofauti. Nyimbo za tohara pamoja na nyimbo za kidini za Kikristo ni baadhi ya zile zinaimbwa. Nyimbo za tohara zinaimbwa wakati wa kutahiri wavulana na za kidini wakati wa shughuli za kidini ya Kikristo. Hata hivyo, hatua ya waimbaji wa nyimbo za dini ya Kikristo kubadilisha nyimbo za tohara kimaudhui, kimtindo na kiutendakazi ili kuzitumia upya katika mazingira ya kidini ili kusaidia katika maenezi ya injili ya Kikristo kwa wengi na kutumika katika hafla zingine za kijamii kando na tohara ni jambo ambalo ni mpya katika jamii ya Waigembe. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti udenguzi wa nyimbo za tohara za Waigembe na nyimbo za dini ya Kikristo ili kuweza kutumika katika hafla tofauti kando na tohara. Makala haya yalilenga kubainisha maudhui ambayo nyimbo za tohara zilizodenguliwa na nyimbo za dini ya Kikristo huwa nayo katika jamii ya Waigembe. Watafiti waliongozwa na nadharia ya udenguzi. Data ya nyimbo kumi na nane imetumika katika makala haya. Awamu tatu ambazo nyimbo hizo hufuata zilichanganuliwa na kuwasilisha maudhui kwa njia ya maelezo. Makala haya yanachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu nyimbo zilizodenguliwa za tohara za Kiigembe, pamoja na kuhifadhi fasihi simulizi ya Kiafrika ili itumike na vizazi vijavyo katika kuafikia maendeleo endelevu.