{"title":"Lugha ya Kiswahili na Ukombozi wa Kifikra katika Afrika: Mkabala wa Kimapinduzi wa Frantz Fanon","authors":"A. Mutembei","doi":"10.1163/26836408-15020047","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"\nUchaguzi wa mtu kuitumia lugha yake kama njia ya ukombozi huanza na uamuzi wa kifikra. Uamuzi huo wa kifikra ni hatua ya ukombozi. Ni uamuzi ambao hatimaye humpa mtumiaji wa lugha mamlaka ya kuchukua hatua zaidi za kujitegemea. Ni ukombozi wa kiisimu ambao, hatimaye humpatia mtumiaji wa lugha nguvu binafsi. Lugha ni mamlaka; na wakati mwingi mamlaka huzaa nguvu. Ingawa hapa ‘nguvu’ inamaanisha uwezo wa mtu binafsi; na ‘mamlaka’ ni dhana ya kisheria, lakini dhana hizi mbili zinahusiana katika uchambuzi huu wa kujenga uwezeshaji kupitia matumizi ya lugha. Katika kuchunguza mawazo ya Frantz Fanon kuhusu dhana ya ukombozi wa fikra kwa Waafrika kama inavyojitokeza kupitia Lugha ya Kiswahili, nadharia ya Bobby Wright ya fikraufu inatoa nafasi kuangalia namna utambulisho wa watu unavyoweza kubomolewa kupitia matumizi ya lugha isiyokuwa ya asili kwao.","PeriodicalId":85828,"journal":{"name":"Utafiti","volume":"2014 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2021-10-29","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"Utafiti","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.1163/26836408-15020047","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Uchaguzi wa mtu kuitumia lugha yake kama njia ya ukombozi huanza na uamuzi wa kifikra. Uamuzi huo wa kifikra ni hatua ya ukombozi. Ni uamuzi ambao hatimaye humpa mtumiaji wa lugha mamlaka ya kuchukua hatua zaidi za kujitegemea. Ni ukombozi wa kiisimu ambao, hatimaye humpatia mtumiaji wa lugha nguvu binafsi. Lugha ni mamlaka; na wakati mwingi mamlaka huzaa nguvu. Ingawa hapa ‘nguvu’ inamaanisha uwezo wa mtu binafsi; na ‘mamlaka’ ni dhana ya kisheria, lakini dhana hizi mbili zinahusiana katika uchambuzi huu wa kujenga uwezeshaji kupitia matumizi ya lugha. Katika kuchunguza mawazo ya Frantz Fanon kuhusu dhana ya ukombozi wa fikra kwa Waafrika kama inavyojitokeza kupitia Lugha ya Kiswahili, nadharia ya Bobby Wright ya fikraufu inatoa nafasi kuangalia namna utambulisho wa watu unavyoweza kubomolewa kupitia matumizi ya lugha isiyokuwa ya asili kwao.