{"title":"Ufanano wa Mtoto wa Laana Kumuua Babaye katika Nyakiiru Kibi na Mfalme Edipode: Dhihiriko la Umageuko au Msambao?","authors":"A. Mnenuka","doi":"10.1163/26836408-15020071","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"\nKisa kinachoelezwa katika simulizi ya Edipode katika tamthilia ya Mfalme Edipode (Sofokile, 1971) kinafanana kwa karibu sana na kisa kinachosimuliwa katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi (Mulokozi, 1998). Sababu kubwa zilizochangia kufanana kwa simulizi hizi mbili zinaweza kuelezwa kwa kuzingatia misingi ya kinadharia, hususan Nadharia ya Mageuko na Nadharia ya Msambao. Wakati Nadharia ya Mageuko ikidai kuwa simulizi yoyote ile ni matokeo ya mabadiliko ya ndani ya jamii yanayochagizwa na mazingira, Nadharia ya Msambao inasisitiza kuwa simulizi huenea kutoka sehemu moja hadi nyingine; kamwe haiwezekani simulizi mbili zinazofanana kuibuka katika jamii mbili ambazo hazijawahi kukutana. Makala hii imechunguza sababu za kufanana kwa visa katika simulizi teule kwa kutumia misingi ya nadharia hizo mbili. Kwa kuzingatia hoja mbalimbali, imehitimishwa kuwa simulizi ya Nyakiiru Kibi, pamoja na kutungwa takribani karne 24 baada ya ile ya Edipode, si kiatani cha Edipode. Simulizi hii imechimbuka katika eneo la Maziwa Makuu na inaonekana ni tukio linalofungamana na historia ya jamii husika huku ikijumuisha visakale hapa na pale.","PeriodicalId":85828,"journal":{"name":"Utafiti","volume":"22 1","pages":""},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-05-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"Utafiti","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.1163/26836408-15020071","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Kisa kinachoelezwa katika simulizi ya Edipode katika tamthilia ya Mfalme Edipode (Sofokile, 1971) kinafanana kwa karibu sana na kisa kinachosimuliwa katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi (Mulokozi, 1998). Sababu kubwa zilizochangia kufanana kwa simulizi hizi mbili zinaweza kuelezwa kwa kuzingatia misingi ya kinadharia, hususan Nadharia ya Mageuko na Nadharia ya Msambao. Wakati Nadharia ya Mageuko ikidai kuwa simulizi yoyote ile ni matokeo ya mabadiliko ya ndani ya jamii yanayochagizwa na mazingira, Nadharia ya Msambao inasisitiza kuwa simulizi huenea kutoka sehemu moja hadi nyingine; kamwe haiwezekani simulizi mbili zinazofanana kuibuka katika jamii mbili ambazo hazijawahi kukutana. Makala hii imechunguza sababu za kufanana kwa visa katika simulizi teule kwa kutumia misingi ya nadharia hizo mbili. Kwa kuzingatia hoja mbalimbali, imehitimishwa kuwa simulizi ya Nyakiiru Kibi, pamoja na kutungwa takribani karne 24 baada ya ile ya Edipode, si kiatani cha Edipode. Simulizi hii imechimbuka katika eneo la Maziwa Makuu na inaonekana ni tukio linalofungamana na historia ya jamii husika huku ikijumuisha visakale hapa na pale.